yahooo
Senior Member
- Apr 8, 2015
- 126
- 276
Ijumaa iliyopita Rafiki yangu wa karibu mkoani Mara, wilaya ya Tarime alikwenda nyumbani Kwa wazazi wa mke wake. Alienda huko kushawishi mke wake arudi nyumbani kutokana na mgogoro wao wa muda mrefu, lakini kukatokea na kutoelewana na wenyeji wake wakiwemo wazazi na mashemeji kuhusiana na hilo. Mke wake huyo alikuwa yupo hapo kwa muda mrefu tu kutokana na migogoro yao, so kutokana na hilo akataka arudishiwe mahari au aondoke na mkewe wakaendelee na maisha.
Basi yakatokea mabishano pale, kwa kuwa imeshindikana kupewa mke , jamaa akataka apewe mtoto wake lakini nalo likashindikana, ilikuwa Mzozo mkubwa pale, jamaa mwisho wa siku akachachamaa anataka mtoto, ndugu wa mke wakawa hawataki, tena mtoto yule akafungiwa chumbani
Jamaa akaamua kubeba mtoto yeyote aliyekuwa pale ambaye siyo Mwanae akaondoka naye akawaambia hatotoa mtoto hadi apewe mtoto wake.
Basi jamaa akampeleka yule mtoto kwa dada yake, halafu yeye akaenda kwake .
Huku Nyuma ndugu wa ile familia ya mwanamke wakaenda kuripoti polisi kwamba mtoto wao ametekwa na mwizi wa watoto.
Lakini pia mashemeji na ndugu wakavamia nyumbani kwa yule rafiki wakimfosi atoe mtoto, jamaa naye akagoma akidai mtoto wake kwanza ndo wapewe mtoto wao. Mara polisi nao wakatia timu wakijua kweli ni mwizi wa watoto wakaanza kumshambulia jamaa kwa mapanga, ndugu na mashemeji nao wakaanza kumshambulia jamaa pia, ila jamaa alikuwa amejipanga naye akapamba nao hadi kumjeruhi polisi mmoja, na mke wake ambaye naye alikuwa eneo la tukio naye alichezea mapanga kadhaa. Basi jamaa alibaki peke yake ndani ya kundi la mapolisi na ndugu wa mke, wakamshambulia hadi kufa.
Hadi Sasa polisi na mke bado wapo hospitali wamelazwa kwa matibabu