Polisi wadaiwa kushambulia na kusababisha kifo Tarime

Ijumaa iliyopita Rafiki yangu wa karibu mkoani Mara ,wilaya ya Tarime alikwenda nyumbani Kwa wazazi wa mke wake.Alienda huko kushawishi mke wake arudi nyumbani kutokana na mgogoro wao wa muda mrefu, lakini kukatokea ma kutoelewana na wenyeji wake wakiwemo wazazi na mashemeji kuhusuana na hilo.Mke wake huyo alikuwa yupo hapo Kwa muda mrefu tu kutokana na migogoro yao, so kutokana na Hilo akataka arudishiwe mahari au aondoke na mkewe wakaendelee na maisha.

Basi yakatokea mabishano pale, Kwa kuwa imeshindikana kupewa mke , jamaa akataka apewe mtoto wake lakini nalo likashindikana..ilikuwa. Mzozo mkubwa pale, jamaa mwisho wa siku akachachamaa anataka mtoto, ndugu za mke wakawa hawataki, tena mtoto yule akafungiwa chumbani
Jamaa akaamua kubeba mtoto yeyote aliyekuwa pale ambaye siyo Mwanae akaondoka naye akawaambia hatotoa mtoto Hadi apewe mtoto wake.

Basi jamaa akampeleka yule mtoto Kwa dada yake, alafu yeye akaenda kwake .

Huku Nyumba ndugu wa Ile familia ya mwanamke wakaenda kuripoti polisi kwamba mtoto wao ametekwa na mwizi wa watoto.
Lakini pia mashemeji na ndugu wakavamia nyumbani Kwa yule rafiki wakimfosi atoe mtoto, , jamaa naye akagoma akidai mtoto wake kwanza Ndo wapewe mtoto wao..mara polisi nao wakatia timu wakijua kweli ni mwizi wa watoto wakaanza kumshambuli jamaa Kwa mapanga, ndugu na mashemeji nao wakaanza kumshambulia jamaa pia, ila jamaa alikuwa amejipanga naye akapamba nao Hadi kumjerui polisi mmoja, na mke wake ambaye naye alikuwa eneo la tukio naye alichezea mapanga kadhaa. Basi jamaa alibaki peke yake ndani ya kundi la mapolisi na ndugu wa mke, wakamshambulia Hadi kufa..

Hadi Sasa polisi na mke bado wapo hospitali wamelazwa Kwa matibabu
Nguvu uhitajika kwenye kufanya kosa la kihalifu tu, lakini kwenye jambo la kheri, upendo tu unatosha. Kulikuwa na ulazima gani kwenda kufanya fujo kwa watu? Na hadi kuteka mtoto dah!

Apumzike kwa amani.

.Ova
 
Ijumaa iliyopita Rafiki yangu wa karibu mkoani Mara ,wilaya ya Tarime alikwenda nyumbani Kwa wazazi wa mke wake.Alienda huko kushawishi mke wake arudi nyumbani kutokana na mgogoro wao wa muda mrefu, lakini kukatokea ma kutoelewana na wenyeji wake wakiwemo wazazi na mashemeji kuhusuana na hilo.Mke wake huyo alikuwa yupo hapo Kwa muda mrefu tu kutokana na migogoro yao, so kutokana na Hilo akataka arudishiwe mahari au aondoke na mkewe wakaendelee na maisha.

Basi yakatokea mabishano pale, Kwa kuwa imeshindikana kupewa mke , jamaa akataka apewe mtoto wake lakini nalo likashindikana..ilikuwa. Mzozo mkubwa pale, jamaa mwisho wa siku akachachamaa anataka mtoto, ndugu za mke wakawa hawataki, tena mtoto yule akafungiwa chumbani
Jamaa akaamua kubeba mtoto yeyote aliyekuwa pale ambaye siyo Mwanae akaondoka naye akawaambia hatotoa mtoto Hadi apewe mtoto wake.

Basi jamaa akampeleka yule mtoto Kwa dada yake, alafu yeye akaenda kwake .

Huku Nyumba ndugu wa Ile familia ya mwanamke wakaenda kuripoti polisi kwamba mtoto wao ametekwa na mwizi wa watoto.
Lakini pia mashemeji na ndugu wakavamia nyumbani Kwa yule rafiki wakimfosi atoe mtoto, , jamaa naye akagoma akidai mtoto wake kwanza Ndo wapewe mtoto wao..mara polisi nao wakatia timu wakijua kweli ni mwizi wa watoto wakaanza kumshambuli jamaa Kwa mapanga, ndugu na mashemeji nao wakaanza kumshambulia jamaa pia, ila jamaa alikuwa amejipanga naye akapamba nao Hadi kumjerui polisi mmoja, na mke wake ambaye naye alikuwa eneo la tukio naye alichezea mapanga kadhaa. Basi jamaa alibaki peke yake ndani ya kundi la mapolisi na ndugu wa mke, wakamshambulia Hadi kufa..

Hadi Sasa polisi na mke bado wapo hospitali wamelazwa Kwa matibabu
Yaani Polisi nao wakashiriki kumshambulia huyo jamaa mpaka kumuua?....hata hao hawaitii Sheria?
 
Huyo mtoto ni WA mashemeji zake ambazo nao walikuwa wanampinga
Igeuze hivi:
Dada yako agombane na mume wake, baada ya ugomvi wao, dada yako anaondoka na mtoto kwenda kwa wazazi wenu.
Halafu huko ulipo unaletewa taarifa kwamba baada ya dada yako kugoma kumpatia mume wake mtoto wao, mume huyo kaamua kubeba mtoto wako na kuondoka naye.
Wewe ungeipokeaji hiyo taarifa ? Na unadhani ungemfanyaje huyo shemeji yako?
 
Polisi gani hao wanashambulia watuhumiwa kwa mapanga badala ya kumkamata na kumpiga pingu ukilinganisha wapo wengi?

Huyo jamaa hana akili vilevile. Unachukuaje mtoto usiyemjua ili urudishiwe mwanao?

Sehemu nyingine za hii nchi bado zipo nyuma kwa viwango vya kutisha. Hii story nzima unaweza dhani ni brainless comedy.
 
Kuna matukio yakitokea yanafikirisha na kudhihirisha uwezo mdogo sana walionao baadhi ya watu/jamii fulani wa kuchanganua mambo (Mema na Mabaya) ya kufanya na ya kutokufanya.

Azikwe, halafu waliobaki hai waowaji na waolewaji walogane au wauane.
Ili mpate matukio ya kutusimulia tena.
 
Kwa maelezo hayo ulivyoandika kama ni kweli, Itoshe tu kusema huyo jamaa yako alikua ni mwehu..
Huwezi kubeba tu mtoto wa mtu eti kisa umenyimwa mtoto wako, alafu ana uhakika gani kama huyo mtoto ni WA kwake, pili anaendaje ukweni kudai mahali?
Huyo jamaa yako ilitakiwa apambane na huyo mwanamke sio familia yake
Mkuu, mahari inadaiwa wapi
 
Back
Top Bottom