Polisi wadaiwa kushambulia na kusababisha kifo Tarime

Polisi wadaiwa kushambulia na kusababisha kifo Tarime

Huko mahala hiyo migororo ya familia ipo mingi sana kiasi cha kufika mahala pa kuuana kabisa na imekuwa kama aina ya maisha yao hasa kwenye swala la kupigana na silaha za jadi. Nafikiri kuna haja ya kuongezwa juhudi ktk kuelimisha jamii za huko sana.
 
Kwa maelezo hayo ulivyoandika kama ni kweli, Itoshe tu kusema huyo jamaa yako alikua ni mwehu..
Huwezi kubeba tu mtoto wa mtu eti kisa umenyimwa mtoto wako, alafu ana uhakika gani kama huyo mtoto ni WA kwake, pili anaendaje ukweni kudai mahali?
Huyo jamaa yako ilitakiwa apambane na huyo mwanamke sio familia yake
Afya ya akili mkuu ??? Mimi mwanamke amelud kwao poa nenda na watoto Kama unaacha utajua mwenyew kwanza Nina uhakika Gani kuwa hao watoto ni wangu??

Halaf mke nimeishi nae hata Kama ni miaka miwili naendaje kudai mahari??

Kwanza Mimi akiondoka kulud kwao sipigi simu Wala kumfuata Hadi wazazi wake wanipigie simu kuwa familia Yako IPO huku na hatuelewi yaan waniite niende tuongeee

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Jamaa yako alikuwa hana busara. Mimi kuna familia nimeacha watoto watatu na nimetoa mahari, walileta huo upumbavu wa kukatalia baadaya marumbano nikwaacha, na huduma nikawa simpi mwanamke, ila nikukutana na mtoto nawapa hela maana wapo karibu na kila siku nawaona. Sasa hivi wamejifunza mpaka wanawaruhusu mpaka kuja nyumbani maana zamani ilikuwa noma wanawakatalia mpaka watoroke, mtoto mkubwa Ana miaka 11, wapili 8 na wa mwisho 4. So jamaa yako angeachana naye tu.
 
Siwezi kugombea mtoto,kama wamechukua poa,ntafta mwingine...mbegu si zipo.
 
Ijumaa iliyopita Rafiki yangu wa karibu mkoani Mara, wilaya ya Tarime alikwenda nyumbani Kwa wazazi wa mke wake. Alienda huko kushawishi mke wake arudi nyumbani kutokana na mgogoro wao wa muda mrefu, lakini kukatokea na kutoelewana na wenyeji wake wakiwemo wazazi na mashemeji kuhusiana na hilo. Mke wake huyo alikuwa yupo hapo kwa muda mrefu tu kutokana na migogoro yao, so kutokana na hilo akataka arudishiwe mahari au aondoke na mkewe wakaendelee na maisha.

Basi yakatokea mabishano pale, kwa kuwa imeshindikana kupewa mke , jamaa akataka apewe mtoto wake lakini nalo likashindikana, ilikuwa Mzozo mkubwa pale, jamaa mwisho wa siku akachachamaa anataka mtoto, ndugu wa mke wakawa hawataki, tena mtoto yule akafungiwa chumbani

Jamaa akaamua kubeba mtoto yeyote aliyekuwa pale ambaye siyo Mwanae akaondoka naye akawaambia hatotoa mtoto hadi apewe mtoto wake.

Basi jamaa akampeleka yule mtoto kwa dada yake, halafu yeye akaenda kwake .

Huku Nyuma ndugu wa ile familia ya mwanamke wakaenda kuripoti polisi kwamba mtoto wao ametekwa na mwizi wa watoto.

Lakini pia mashemeji na ndugu wakavamia nyumbani kwa yule rafiki wakimfosi atoe mtoto, jamaa naye akagoma akidai mtoto wake kwanza ndo wapewe mtoto wao. Mara polisi nao wakatia timu wakijua kweli ni mwizi wa watoto wakaanza kumshambulia jamaa kwa mapanga, ndugu na mashemeji nao wakaanza kumshambulia jamaa pia, ila jamaa alikuwa amejipanga naye akapamba nao hadi kumjeruhi polisi mmoja, na mke wake ambaye naye alikuwa eneo la tukio naye alichezea mapanga kadhaa. Basi jamaa alibaki peke yake ndani ya kundi la mapolisi na ndugu wa mke, wakamshambulia hadi kufa.

Hadi Sasa polisi na mke bado wapo hospitali wamelazwa kwa matibabu
Tz kuna Ujinga uliopitiliza!
 
We unaongea ujinga usieleweka.
Huyo jamaa alitaka kuleta utemi, inawezekana alishidndwa kutii amri alikuwa ameshika panga, inawezekana aliambiwa aweke panga chini akakaidi, watu wa Tarime kwa ugomvi wa mapanga ndio zao.

Hata askari wa US , ukiambiwa , weka mikono dirishani na utoke nje halafu ukaleta ukaidi wa kipuuzi eti sitaki unapeleka mikono mifukoni, risasi zinakuhusu.
Kuna channel YouTube ya police activity ya marekani asee huwa naogopa maana polisi wa us kauli ni moja tu,,,show me your hand do not reach,,,akisema hivo na ukajifanya kujikuna umeisha unapigwa ya kichwa na habari unaishia hapo.
 
We unaongea ujinga usieleweka.
Huyo jamaa alitaka kuleta utemi, inawezekana alishidndwa kutii amri alikuwa ameshika panga, inawezekana aliambiwa aweke panga chini akakaidi, watu wa Tarime kwa ugomvi wa mapanga ndio zao.

Hata askari wa US , ukiambiwa , weka mikono dirishani na utoke nje halafu ukaleta ukaidi wa kipuuzi eti sitaki unapeleka mikono mifukoni, risasi zinakuhusu.
Kuna channel YouTube ya police activity ya marekani asee huwa naogopa maana polisi wa us kauli ni moja tu,,,show me your hand do not reach,,,akisema hivo na ukajifanya kujikuna umeisha unapigwa ya kichwa na habari inaishia hapo.
 
US raia wengi hadi watoto wadogo wana silaha, kuna cases nyingi za askari kushambuliwa na kujeruhiwa ama kuuawa, hivyo huwa wanakuwa makini sana, ukijikuna tu na assume upo na silaha na ni hatari hivyo hachelewi kukushambulia.
 
Kwa maelezo hayo ulivyoandika kama ni kweli, Itoshe tu kusema huyo jamaa yako alikua ni mwehu..
Huwezi kubeba tu mtoto wa mtu eti kisa umenyimwa mtoto wako, alafu ana uhakika gani kama huyo mtoto ni WA kwake, pili anaendaje ukweni kudai mahali?
Huyo jamaa yako ilitakiwa apambane na huyo mwanamke sio familia yake
Itoshe kusema mwendazake alikuwa mjeuri na asiyeambilika, kwanza unaendaje kwenye mada ya kifamilia kama hiyo ukweni ukiwa peke yako?
 
Back
Top Bottom