Polisi wadaiwa kushambulia na kusababisha kifo Tarime

Kwa maelezo hayo ulivyoandika kama ni kweli, Itoshe tu kusema huyo jamaa yako alikua ni mwehu..
Huwezi kubeba tu mtoto wa mtu eti kisa umenyimwa mtoto wako, alafu ana uhakika gani kama huyo mtoto ni WA kwake, pili anaendaje ukweni kudai mahali?
Huyo jamaa yako ilitakiwa apambane na huyo mwanamke sio familia yake
😄

Ova
 
Ijumaa iliyopita Rafiki yangu wa karibu mkoani Mara, wilaya ya Tarime alikwenda nyumbani Kwa wazazi wa mke wake. Alienda huko kushawishi mke wake arudi nyumbani kutokana na mgogoro wao wa muda mrefu, lakini kukatokea na kutoelewana na wenyeji wake wakiwemo wazazi na mashemeji kuhusiana na hilo. Mke wake huyo alikuwa yupo hapo kwa muda mrefu tu kutokana na migogoro yao, so kutokana na hilo akataka arudishiwe mahari au aondoke na mkewe wakaendelee na maisha.

Basi yakatokea mabishano pale, kwa kuwa imeshindikana kupewa mke , jamaa akataka apewe mtoto wake lakini nalo likashindikana, ilikuwa Mzozo mkubwa pale, jamaa mwisho wa siku akachachamaa anataka mtoto, ndugu wa mke wakawa hawataki, tena mtoto yule akafungiwa chumbani

Jamaa akaamua kubeba mtoto yeyote aliyekuwa pale ambaye siyo Mwanae akaondoka naye akawaambia hatotoa mtoto hadi apewe mtoto wake.

Basi jamaa akampeleka yule mtoto kwa dada yake, halafu yeye akaenda kwake .

Huku Nyuma ndugu wa ile familia ya mwanamke wakaenda kuripoti polisi kwamba mtoto wao ametekwa na mwizi wa watoto.

Lakini pia mashemeji na ndugu wakavamia nyumbani kwa yule rafiki wakimfosi atoe mtoto, jamaa naye akagoma akidai mtoto wake kwanza ndo wapewe mtoto wao. Mara polisi nao wakatia timu wakijua kweli ni mwizi wa watoto wakaanza kumshambulia jamaa kwa mapanga, ndugu na mashemeji nao wakaanza kumshambulia jamaa pia, ila jamaa alikuwa amejipanga naye akapamba nao hadi kumjeruhi polisi mmoja, na mke wake ambaye naye alikuwa eneo la tukio naye alichezea mapanga kadhaa. Basi jamaa alibaki peke yake ndani ya kundi la mapolisi na ndugu wa mke, wakamshambulia hadi kufa.

Hadi Sasa polisi na mke bado wapo hospitali wamelazwa kwa matibabu
Marehemu alikua mchokozi! Alikufa ila alikufa kwa mbinde
 
Mi ninachoweza kushauri nyie vijana wa Tarime, acheni utemi usio kuwa na faida, dunia imebadilika, watu hivi sasa hawaogopi mapanga.

Mkoa wa Mara mna ka proud flani utasikia kijana anasema "mimi ndio mkurya".

Bro hizo zilipendwa, hivi sasa ukizingua watu wana deal na wewe perpendicular.
hao wakurya sio watu. tulimuozesha mmoja binti yetu akawa kutwa vipigo binti akaona ya nini akakimbia na mtoto akarudi arusha. mpaka leo wajomba tunalea mtoto.
 
Duamira n jambo jingine. Je angekiwa ni mtoto wake anatekwa na shemeji yako kwa ajili ya maugomvi yao ungechukua hatua gani?
Ndio maana nimesema dhamira na sio sheria, elewa maudhui, hiyo ni karma ndugu yangu, kwakuwa wanajua chanzo kilicho pelekea hali hiyo mioyo yao haitokuwa na amani kamwe, watajijibu wenyewe kama walikuwa na sababu za msingi kumzuia mtoto wake au ni hasira , na kama walikuwa na sababu za msingi kumkatalia mke au ni nguvu ya ndugu wa mke , na waweza kukuta mke alikuwa radhi kurudi lakini ndugu wakakataa na akabebwa na nguvu ya ndugu kukubali hilo

Katika hii dunia epuka kuwa chanzo cha kutoa uhai wa mwingine tena kwa sababu za kutunga, walikuwa wanajua sababu za huyo jamaa kubeba huyo mtoto na hajambeba kifichoni kwa mujibu wa maelezo,sasa walikuwa na sababu gani kuripoti polisi kwamba jamaa ni mtekaji wa watoto?walishindwa nini kueleza polisi ukweli halisi Wakati wanaujua ukweli wa tukio zima?
 
Angefuata taratibu...ila jamii za Mara hususani wazazi wa wanawake wanaopenda sana kung'ang'ania watoto bila sababu za msingi na kuwafanya watoto waishi maisha magumu.
japo simpendi nyerere bora alivyowapunguza nguvu hawa watu jeshini. wangekuja kutusumbua siku moja
 
Mtoa mada alijua akirembesha kwa kutaja polisi na mwanamke basi atapata uungwaji mkono naona ngoma ishamgeukia hii, hao polisi wa kutumia mapanga itakuwa mgambo tu,
 
Utakuwa huwafahamu vizuri polisi wa nchi hii. Hao jamaa mara kibao tu tumesikia wakihusika kuwateka, kuwaua na kuwapora fedha wafanyabiashara.

Kuna majambazi kibao tu humo wamejichanganya na kujificha kwenye gwanda, bora hata mgambo hutekeleza amri na maelekezo ya hao polisi.
 
Nawajua ila sio kwenye mapanga, halafu huoni marehemu alikuwa anahatarisha usalama wa raia au?
 
Ndio maana nimesema dhamira na sio sheria, elewa maudhui, hiyo ni karma ndugu yangu, kwakuwa wanajua chanzo kilicho pelekea hali hiyo mioyo yao haitokuwa na amani kamwe, watajijibu wenyewe kama walikuwa na sababu za msingi kumzuia mtoto wake au ni hasira , na kama walikuwa na sababu za msingi kumkatalia mke au ni nguvu ya ndugu wa mke , na waweza kukuta mke alikuwa radhi kurudi lakini ndugu wakakataa na akabebwa na nguvu ya ndugu kukubali hilo

Katika hii dunia epuka kuwa chanzo cha kutoa uhai wa mwingine tena kwa sababu za kutunga, walikuwa wanajua sababu za huyo jamaa kubeba huyo mtoto na hajambeba kifichoni kwa mujibu wa maelezo,sasa walikuwa na sababu gani kuripoti polisi kwamba jamaa ni mtekaji wa watoto?walishindwa nini kueleza polisi ukweli halisi Wakati wanaujua ukweli wa tukio zima?
Umefafanua vema kabisa.

Kuna jamaa mmoja huku naye alijinyonga ukweni sebuleni kwa mamamkwewe alipofuata mkewe na watoto watatu kwa sababu ya upinzani wa kipuuzi wa familia ya wakweze.

Japo siungi mkono maamuzi dhaifu kama hayo ya hao victims (niliyemtaja na huyu wa mleta mada) lakini familia za wakwe huchangia sana kuharibu ndoa, na pengine kuharibu kabisa maisha ya wajukuu.

Matatizo sugu ya ndoa huchangia sana kusababisha changamoto ya afya ya akili hasa yakiwakuta watu dhaifu wanaoendeshwa na hisia zaidi, matokeo yake ni maamuzi kama hayo. Sasa badala ya wakwe kusaidia kupunguza matatizo, wengi wao hushiriki kuyaanzisha na kuyatilia petroli.

Maandiko yanasema 'ndoa na iheshimiwe na watu wote', ukishiriki kuiharibu kijinga namna hiyo kuna namna mbeleni karma itakupa kipigo tu.
 
Kuna jamaa hapo juu amesema jamaa yako amekufa kijinga sana.

Eti unadai urudishiwe mahali, eti upewe mtoto.
Mtoto akikua atakutafuta baba yake, au akifikisha miaka 7 kisheria unamdai tu mahakamani.
Wanawake wakuoa wamejaa mitaani huku kibao tu, wewe mwenyewe tu.

Elimu ya msingi iliyobora ni muhimu sana kwa watanzania woote, maisha ya watu yaboreshe watu wasiwe na stress kiasi hichi..
Watu wakisoma vizuri na wakawa na maisha mazuri kuna ujinga unapungua pia.
 
Nawajua ila sio kwenye mapanga, halafu huoni marehemu alikuwa anahatarisha usalama wa raia au?
Kama hujui kuwa wanaweza kutumia silaha yoyote basi bado hujawafahamu.

Ni kweli alikuwa anahatarisha usalama, ila ni upungufu wa akili na weledi polisi kukosa kabisa mbinu za kumpunguza makali na kumtia pingu apelekwe kwenye vyombo vya sheria, badala yake kumcharanga mapanga hadi kummaliza kabisa!

Tatizo lao wamewekeza nguvu nyingi kupambana na wapinzani ambao huwa hawana hata wembe wala hawarushi hata kofi, matokeo yake kutokana kukosa mbinu wakikutana na mtu ana silaha hata wawe wengi kama utitiri solution yao itakuwa kuhakikisha wanamuua kwanza ndipo wamdhibiti akiwa ni no more. Lakini pia wanakosa busara katika utatuzi wa migogoro na kuishia kutumia miguvu tu. Ikitumika akili nyingi nguvu kidogo au zero kabisa) migogoro ya namna hiyo huwa ni rahisi tu kuuimaliza, hata mimi ningeumaliza mgogoro huo kwa amani kabisa, na watu wangecheka, wangepeana mikono, na maisha yangeendelea bila damu kumwagika wala kutoboana macho.
 
We unaongea ujinga usieleweka.
Huyo jamaa alitaka kuleta utemi, inawezekana alishidndwa kutii amri alikuwa ameshika panga, inawezekana aliambiwa aweke panga chini akakaidi, watu wa Tarime kwa ugomvi wa mapanga ndio zao.

Hata askari wa US , ukiambiwa , weka mikono dirishani na utoke nje halafu ukaleta ukaidi wa kipuuzi eti sitaki unapeleka mikono mifukoni, risasi zinakuhusu.
 
Yeye mwanamke Ndo alitakiwa akavunje ndoa mahakamani ili akakae home kihalali, Mahakama ikiona mwanamke hana sababu za msingi kisheria, inakataa ndoa kuvunjwa, ikiona ni sawa inavunja..Huwezi kukaa home kienyeji. KwanzA wewe unaonekana mwanamke wa kizaramu Ndo mana mnaachana kifala na ndio mana wengi wenu ni masingo Maza
We ni mjinga.
Huyo jamaa yake ndiye angeenda mahakamani kumshtaki mkewe, yeye anakwenda kwao usiku kuanzisha vurugu.

We unaonekana ni wale mademu wa kujiuza bar na kuchukuliwa na walevi hapo Tarime ndio mnapenda vurugu za kijinga za kugombania wanaume.
 
We unaongea ujinga usieleweka.
Huyo jamaa alitaka kuleta utemi, inawezekana alishidndwa kutii amri alikuwa ameshika panga, inawezekana aliambiwa aweke panga chini akakaidi, watu wa Tarime kwa ugomvi wa mapanga ndio zao.

Hata askari wa US , ukiambiwa , weka mikono dirishani na utoke nje halafu ukaleta ukaidi wa kipuuzi eti sitaki unapeleka mikono mifukoni, risasi zinakuhusu.
Kwahiyo wewe bwana mwerevu akili yako kubwa ikiwaza na kuwazua inaishia kupata kuwa solution ni kumcharanga mapanga hadi kumuua? Kama walipata upenyo wa kumcharanga mapanga walishindwa vipi kumkamata akiwa hai akatibiwe then awajibishwe kisheria?

Kwanza lini polisi wameanza kutumia panga kudili na wahalifu? Wangemuua kwa risasi wakasema alikaidi amri at least tungeelewa japo kwa kufosi.

Huu utaratibu wa kutumia mapanga ukihalalishwa kwa wapinzani si tutawazika wengi
 
Wangetumia mbinu ipi kumkamata hebu elezea we unaye elewa njia za kumkamata muhalifu aliye na silaha.
 
Ijumaa iliyopita Rafiki yangu wa karibu mkoani Mara, wilaya ya Tarime alikwenda nyumbani Kwa wazazi wa mke wake. Alienda huko kushawishi mke wake arudi nyumbani kutokana na mgogoro wao wa muda mrefu, lakini kukatokea na kutoelewana na wenyeji wake wakiwemo wazazi na mashemeji kuhusiana na hilo. Mke wake huyo alikuwa yupo hapo kwa muda mrefu tu kutokana na migogoro yao, so kutokana na hilo akataka arudishiwe mahari au aondoke na mkewe wakaendelee na maisha.

Basi yakatokea mabishano pale, kwa kuwa imeshindikana kupewa mke , jamaa akataka apewe mtoto wake lakini nalo likashindikana, ilikuwa Mzozo mkubwa pale, jamaa mwisho wa siku akachachamaa anataka mtoto, ndugu wa mke wakawa hawataki, tena mtoto yule akafungiwa chumbani

Jamaa akaamua kubeba mtoto yeyote aliyekuwa pale ambaye siyo Mwanae akaondoka naye akawaambia hatotoa mtoto hadi apewe mtoto wake.

Basi jamaa akampeleka yule mtoto kwa dada yake, halafu yeye akaenda kwake .

Huku Nyuma ndugu wa ile familia ya mwanamke wakaenda kuripoti polisi kwamba mtoto wao ametekwa na mwizi wa watoto.

Lakini pia mashemeji na ndugu wakavamia nyumbani kwa yule rafiki wakimfosi atoe mtoto, jamaa naye akagoma akidai mtoto wake kwanza ndo wapewe mtoto wao. Mara polisi nao wakatia timu wakijua kweli ni mwizi wa watoto wakaanza kumshambulia jamaa kwa mapanga, ndugu na mashemeji nao wakaanza kumshambulia jamaa pia, ila jamaa alikuwa amejipanga naye akapamba nao hadi kumjeruhi polisi mmoja, na mke wake ambaye naye alikuwa eneo la tukio naye alichezea mapanga kadhaa. Basi jamaa alibaki peke yake ndani ya kundi la mapolisi na ndugu wa mke, wakamshambulia hadi kufa.

Hadi Sasa polisi na mke bado wapo hospitali wamelazwa kwa matibabu
Huyo jamaa yako alikuwa na kaujinga flani
 
Wangetumia mbinu ipi kumkamata hebu elezea we unaye elewa njia za kumkamata muhalifu aliye na silaha.
Ungesoma vizuri ungeelewa walichotakiwa kufanya, ila kwakuwa una hasira kali ndo maana unaishia kuita watu kuwa ni wajinga kwakuwa tu umetofautiana nao kimitazamo.

Ukiweza elezea uhalali wa polisi kutumia mapanga kudili na wahalifu.
 
Back
Top Bottom