Polisi wadaiwa kushambulia na kusababisha kifo Tarime

yahooo

Senior Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
126
Reaction score
276
Ijumaa iliyopita Rafiki yangu wa karibu mkoani Mara, wilaya ya Tarime alikwenda nyumbani Kwa wazazi wa mke wake. Alienda huko kushawishi mke wake arudi nyumbani kutokana na mgogoro wao wa muda mrefu, lakini kukatokea na kutoelewana na wenyeji wake wakiwemo wazazi na mashemeji kuhusiana na hilo. Mke wake huyo alikuwa yupo hapo kwa muda mrefu tu kutokana na migogoro yao, so kutokana na hilo akataka arudishiwe mahari au aondoke na mkewe wakaendelee na maisha.

Basi yakatokea mabishano pale, kwa kuwa imeshindikana kupewa mke , jamaa akataka apewe mtoto wake lakini nalo likashindikana, ilikuwa Mzozo mkubwa pale, jamaa mwisho wa siku akachachamaa anataka mtoto, ndugu wa mke wakawa hawataki, tena mtoto yule akafungiwa chumbani

Jamaa akaamua kubeba mtoto yeyote aliyekuwa pale ambaye siyo Mwanae akaondoka naye akawaambia hatotoa mtoto hadi apewe mtoto wake.

Basi jamaa akampeleka yule mtoto kwa dada yake, halafu yeye akaenda kwake .

Huku Nyuma ndugu wa ile familia ya mwanamke wakaenda kuripoti polisi kwamba mtoto wao ametekwa na mwizi wa watoto.

Lakini pia mashemeji na ndugu wakavamia nyumbani kwa yule rafiki wakimfosi atoe mtoto, jamaa naye akagoma akidai mtoto wake kwanza ndo wapewe mtoto wao. Mara polisi nao wakatia timu wakijua kweli ni mwizi wa watoto wakaanza kumshambulia jamaa kwa mapanga, ndugu na mashemeji nao wakaanza kumshambulia jamaa pia, ila jamaa alikuwa amejipanga naye akapamba nao hadi kumjeruhi polisi mmoja, na mke wake ambaye naye alikuwa eneo la tukio naye alichezea mapanga kadhaa. Basi jamaa alibaki peke yake ndani ya kundi la mapolisi na ndugu wa mke, wakamshambulia hadi kufa.

Hadi Sasa polisi na mke bado wapo hospitali wamelazwa kwa matibabu
 
Matatizo hayo chanzo umasikini na elimu duni, kuna makabila bado yako uncivilised kabisa unaishi bush duh!!!!
 
Huyo jamaa yako alikuwa ni mwehu. Huwezi ukaamia tu kubeba mtoto yoyote kisa wamekatalia mtoto wako ambaye hata hivyo yupo na mama yake. je, huyo mtoto yeyote aliyemchukua yeye ni mtoto wa mke wke? Huko alipompeleka ni kwao?
Basi jamaa akampeleka yule mtoto Kwa dada yake, alafu yeye akaenda kwake .Huku Nyumba ndugu wa Ile familia ya mwanamke wakaenda kuripoti polisi juu ya kwamba mtoto wao ametekwa na mwizi wa watoto.
Walikuwa sahihi, huyo jamaa ni kweli alimteka huyo mtoto na akatoa madai yake ili arudishe mtoto. Huo ni utekekaji kabisa.
Ulitaraji wamuache hai?
 
hakuwa mwizi, ni ishu ya mgogoro wa familia
 
Pole sana mkuu
 
Kwa maelezo hayo ulivyoandika kama ni kweli, Itoshe tu kusema huyo jamaa yako alikua ni mwehu..
Huwezi kubeba tu mtoto wa mtu eti kisa umenyimwa mtoto wako, alafu ana uhakika gani kama huyo mtoto ni WA kwake, pili anaendaje ukweni kudai mahali?
Huyo jamaa yako ilitakiwa apambane na huyo mwanamke sio familia yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…