Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwanadamu ata umuwekee tozo elfu 2 atafanya jitihada akwepe tuHuenda hilo ndio tatizo hizo Tozo na Kodi sio rafiki..., hivi kuna mtu anaweza akanipa breakdown hapo Serikali inakula ngapi kwenye kila gram
Maskini kakimbia utajiri
Nope unakuta hawa wengi wanaokwepa kama asilimia lukuki ya kina TRA plus rushwa na red tapes za hapa na pale.....unakuta mtu anatoa hata robo tatu ambayo angetoa kama kodi anatoa Rushwa sasa kama unadhani Kodi na Tozo zingekuwa hata hio robo tatu au chini kidogo ya hapo wasingejipeleka wenyewe kutoa ?, unakuta pesa wanazotoa hongo za hapa na pale zile mtu angeweza kulipa kama zingekuwa na uhalisia...
Police Hawa Hawa Waliouwa Mtu Mwema Mtwara Kisa Madini
NakaziaAnatorosha kwenda wapi?Mtu bado yupo Mbeya ndani ya Tanzania useme anatorosha?.Kama alikuwa anaenda kutafuta soko zuri mkoa mwingine?
Polisi siwamini kabisa,ni majambazi yanayolipwa kwa kodi zetu.
Usikute alipewa achaguwe kutimka yaishe au sheria ichukuwe mkondo wakeJeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Maafisa Madini Wilaya ya Chunya limefanikiwa kukamata madini aina ya dhahabu yenye thamani zaidi ya Tsh milioni mia arobaini (140).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, ameeleza kuwa Februari 9, 2022 majira ya saa 19:30 usiku katika kizuizi cha Polisi Chalangwa kilichopo Kata ya Chalangwa, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Askari Polisi kwa kushirikiana na Maafisa Madini Wilaya ya Chunya walikamata Gari T.948 DTM aina ya Toyota Crown iliyokuwa ikiendeshwa na mtu aliyefahamika kwa jina BARAKA SINGU @ NYODA, ambaye baada ya kusimamishwa kwenye kizuizi hicho alikimbia na kutelekeza gari hiyo.
Katika upekuzi uliofanywa kwenye gari hiyo vilikutwa vipande 36 vya madini aina ya dhahabu vyenye uzito wa gramu 1367.07 vyenye thamani ya Tshs. 147,694,961.83/= na fedha taslimu Tshs. 504,600/=, lengo ni kukwepa kodi na tozo za serikali.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa kwa hatua zaidi za kisheria.
Aidha, linatoa rai kwa wafanyabiashara kutambua kuwa mkono wa serikali ni mrefu hivyo ni vyema kufanya biashara halali kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo ili kuepuka kukinzana na sheria.
View attachment 2114949
Una uhakika baada ya tozo zote na makato yote total ni 4% pekee ?, Na huyo mununuzi huwa akienda kuuza huko dunia ya mbali faida yake huwa ni asilimia ngapi ?Unaacha madini yote hayo,kisa mrahaba wa 4% duu,sasa serikali inayauza na hela inaingia huko
Hapo mwamba kakimbiza roho yake kwanza sio kwamba kakimbia huo mzigo.