Polisi wakamata dhahabu ya Sh milioni 140 ikitoroshwa, mtuhumiwa atokomea, atelekeza gari

Polisi wakamata dhahabu ya Sh milioni 140 ikitoroshwa, mtuhumiwa atokomea, atelekeza gari

taratibu za sasa kwenye madini ngumu sana, bado hapo kuna mkanganyiko, uchunguzi ufanyike....ukiwa na master dealer licence uko huru kwenda kokote na mzigo ila tu uwe na documents za kodi toka hapo wilayani madini zinazoonyesha umelipa mrahaba na unatoka na madini nje ya wilaya au mkoa.... brokers licence inakuruhusu kufanya biashara ndani tu ya mkoa husika.... hii ni confusing story,..
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Maafisa Madini Wilaya ya Chunya limefanikiwa kukamata madini aina ya dhahabu yenye thamani zaidi ya Tsh milioni mia arobaini (140).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, ameeleza kuwa Februari 9, 2022 majira ya saa 19:30 usiku katika kizuizi cha Polisi Chalangwa kilichopo Kata ya Chalangwa, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Askari Polisi kwa kushirikiana na Maafisa Madini Wilaya ya Chunya walikamata Gari T.948 DTM aina ya Toyota Crown iliyokuwa ikiendeshwa na mtu aliyefahamika kwa jina BARAKA SINGU @ NYODA, ambaye baada ya kusimamishwa kwenye kizuizi hicho alikimbia na kutelekeza gari hiyo.

Katika upekuzi uliofanywa kwenye gari hiyo vilikutwa vipande 36 vya madini aina ya dhahabu vyenye uzito wa gramu 1367.07 vyenye thamani ya Tshs. 147,694,961.83/= na fedha taslimu Tshs. 504,600/=, lengo ni kukwepa kodi na tozo za serikali.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa kwa hatua zaidi za kisheria.

Aidha, linatoa rai kwa wafanyabiashara kutambua kuwa mkono wa serikali ni mrefu hivyo ni vyema kufanya biashara halali kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo ili kuepuka kukinzana na sheria.

View attachment 2114949
Mnajua senema nyie?
 
Yuko ndani ya territory bado anatorosha madini wapi na wapi, after all dhahabu unaweza ukaamua kuuza au usiamue kuuza, kama alikuwa anaenda kuhifadhi nyumbani kwake who knows. Hakuna sheria inayoladhimisha kuwa ukiwa na dhahabu lazima uiuze sometimes unaweza itunza for future .

Kuna namna hapa...

Uwe unauliza kabla hujaandika huu utopolo.

FYI kuna leseni za utunzaji na usafirishaji dhahabu, ni lazima uwe nayo ili uweke kufanya hivyo. Huyu hakuwa na vibali it's a no brainer ndo maana kakimbia, jidanganye dhahabu ni yako bila vibali upigwe kesi ya uhujumu uchumi.
 
Kwani sheria inasemaje juu ya mahala mtu anaweza kuuza madini yake? Kuna masoko mangapi ya kuuza na kununua dhahabu nchini? Ukichimba dhahabu Chunya ,Je huwezi kwenda kuiuza Kwenye solo la Kahama?

Unaweza kama una leseni ya kusafirisha tu. Asiye na leseni hawezi.
 
Hawa Polisi siku hizi wasivyoaminika hasa likija swala la madini hata kama ni mimi ningekimbia.

Na hapo swali la msingi ni je, kweli idadi iliyotajwa ndiyo iliyokamatwa?
Hapo hakuna upigaji,kwa sababu taasisi mbili zimehusika, polisi+wizara ya madini,upigaji ungekuwepo kama wangekuwa watu wa wizara ya madini peke yao au polisi peke yao.
 
Yuko ndani ya territory bado anatorosha madini wapi na wapi, after all dhahabu unaweza ukaamua kuuza au usiamue kuuza, kama alikuwa anaenda kuhifadhi nyumbani kwake who knows. Hakuna sheria inayoladhimisha kuwa ukiwa na dhahabu lazima uiuze sometimes unaweza itunza for future .

Kuna namna hapa...
Ukishayapata unayalipia kodi kwanza vinginevyo we mwizi
 
Polisi hawa hawa awakimbie tu bila sababu😅😂
Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kwamba hivyo vinavyotangazwa ndivyo vilivyotokea!
Jeshi hili hili au jeshi lipi??

Hapo kuna walakini, ama vipande vilikuwa vingi ama walikuwa na pesa ama yote mawili!

Mtuhumiwa wa kukwepa Kodi, njoo utueleze ukweli kama bado uko hai, popote ilipo!
 
Mh! Hivi alishindwa kutoa rushwa akaacha zigo la namna hiyo..?
Huyu ndo mtu alieukimbia utajiri alasivyo ipo namna imetendeka kwa maisha haya uache 140 million!!!! Ha ha ha!.
Aisee itakua haujawahi kuingia kwenye kumi 18 za watu wa serikali halafu hawana background yoyote ile ya biashara..unawesa kuta zigo lote hilo thamani ni 140m wao wanakwambia tupe milioni 300 tukuachie huu mzigo ni wa milioni 700 wakati mfukoni una 500,000 kama ya huyo jamaaa
 
Aisee itakua haujawahi kuingia kwenye kumi 18 za watu wa serikali halafu hawana background yoyote ile ya biashara..unawesa kuta zigo lote hilo thamani ni 140m wao wanakwambia tupe milioni 300 tukuachie huu mzigo ni wa milioni 700 wakati mfukoni una 500,000 kama ya huyo jamaaa
Ndo maana watu huroga!
 
Sasa he ukikamatwa ukiwa njiani kwenda kuprocesa kibali inakuwaje hivi hawaoni hii Sheria ipo unreasonable???

Kimsingi huwezi kutoka mgodini uache madini pale utakuta hayapo unless haujui mazingira ya migodini, jiwe likitoka huwa silaha nje nje ni hakuna mtu kutoka kwenye shimo Wala mtu kuingia.

Tajiri anashuka shimoni anahesabu mawe yake anayachimbia kibindoni then akitoka nje gari inawashwa Kama imeibiwa na hakuna kusimamia hata trafiki akikusimamisha Wala polisi yeyote.

Sasa Hawa polisi wa chunya taarifa yao Ina walakini, huyu jamaa lazima Kuna kitu maana kakimbia akiwa ndani ya wilaya na mara nyingi ukiona polisi wameamua kuripoti basi wameshindwana na jamaa na wanaona atawachomea.
Huo uchimbaji wa kizamani siku hizi haupo.
 
Kwan dhahabu na fedha ukiziwekakwenye siti alafu kwenye radio unaweka nyimbo za kikatoliki na bibliatatu nne ndan watakujua kweli
 
Back
Top Bottom