View attachment 1382873
Pamoja na Ulinzi wa namna hii wa viongozi wa ccm lakini kumbe viongozi hawa wanaweza kudhurika ! wanaweza hata kupigwa vibao , kupigwa fimbo ama hata kupewa sumu kama Ilivyothibitishwa na RPC wa Dar es Salaam Lazaro Mambosasa.
Natoa wito kwa wanadamu kuacha kujivuna na kujimwambafai kwa sababu ya madaraka , mlinzi pekee na wa uhakika ni Mungu pekee , huyu hawezi kukubwaga wala kukutilia sumu .
Maandiko matakatifu yanaeleza kwamba AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU ( YEREMIA 17 : 5 )