Polisi waliohusika na M.150 Wafukuzwa kazi!

Polisi waliohusika na M.150 Wafukuzwa kazi!

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
1,832
Reaction score
566
Mkuu wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam,Kamanda SULEMAN KOVA,amesema kwamba Jeshi la Polisi limewafukuza Askari Polisi Watano waliohusika na Wizi wa pesa zaidi ya shilingi Ml,150 walizoiba ktk tukio la Ujambazi lililotokea mwishoni mwa mwaka jana maeneo ya KARIAKOO!
Akizungumza na Waandishi wa Habari alisema kwamba baada ya Polisi kufanya Upelelezi pamoja na Kuwahoji baadhi ya raia waliokuwepo ktk eneo la Tukio siku ile, walijiridhisha kwamba ni ukweli kwamba Askari polisi hao watano waliiba pesa hizo!

Ndipo waliamua kuwashtaki ktk Mahakama ya kijeshi pamoja na kuwafukuza Kazi!!

Source:ITV HABARI SAA 2 USIKU!

NB:
Je hatua kuwashtaki Polisi hao ktk Mahakama ya Kijeshi pekee badala ya Mahakama ya Kiraia ni sawa??
Tayari wamevuliwa vyeo na kwamba wao sio Askari polisi tena ila ni raia wa kawaida,kama hakuna Kiini Macho,hapo je Kuna nini?
 
Mbona yeye hajajifukuza? Majina yametajwa? Wasijesema wamewafukuza aafu wakawahamishia makete wakaue wateja wa nmb wakati wakichukua hela zao.
 
yeye bado nikamanda mkuu wangu? lahaula!mimi ningeshasepa kwa neno la kustaafu kwa hiyari ama kuwajibika,nchi hii!
 
Hivi hawa wanaofukuzwa wanapelekwa wapi? Isije kuwa ndio tunawaongeza waalifu, ni vyema hawa watu wakafatiliwa kwa makini, au wakawekwa ndani kwa makosa hayo ya kipuuzi.
 
Wamerudisha hizo milioni 150 au wamefukuzwa kazi tu. Wanatakiwa walipe na kazi wafukuzwe wasipo lipa washtakiwe.
Hayo unayoyataka kwa Bongo hii, utangoja sana tu! Ni vipi kuhusu akina Nzowa na wenzake waliotaka kumwekea madawa ya kulevya mtoto wa Mengi? Hizo milioni 150 tunajua hawawezi kuzirudisha kwa kuwa walishawapelekea wakubwa wao ambao nao walikatiwa kitu kidogo tu, kikubwa wamekula akina Kova. Kama wanabisha wawapeleke mahakamani kama wasipowaumbua, labda wawauwe kama yule Yasin wa Zombe.

hh
 
Hivi hawa wanaofukuzwa wanapelekwa wapi? Isije kuwa ndio tunawaongeza waalifu, ni vyema hawa watu wakafatiliwa kwa makini, au wakawekwa ndani kwa makosa hayo ya kipuuzi.

Kimsingi kinachotokea ni Mbwa kala Mbwa.
Wote wamepata mgao, anayefukuza na anayefukuzwa.

Ngoma sare yenye magoli kumi kumi.
 
Wamerudisha hizo milioni 150 au wamefukuzwa kazi tu. Wanatakiwa walipe na kazi wafukuzwe wasipo lipa washtakiwe.

Mkuu siamini!!!!
Ama kuna mtu ametumia ID yako...
 
Wamerudisha hizo milioni 150 au wamefukuzwa kazi tu. Wanatakiwa walipe na kazi wafukuzwe wasipo lipa washtakiwe.

kumbe sometimes huwa una akili!
Uwe unatembea nazo bana muda wote!
 
Mshahara wa polisi kwani shilling ngapi coz mtu kachukua 150 million unamfukuza kazi inasaidia nini
After 3 month anafukuzana na mengi mwaka ukiisha tajiri kuliko bakresa
Poor thinking capacity ya viongozi wetu ndo inaigarimu nchi
Kova kesho kutwa atawaomba rushwa hawa matajiri aliowafukuza kazi
Pumbavu
 
Tafadhari kama mwenye majina kamili ya wale askari wezi ayaweke hapa plz.
 
Wamerudisha hizo milioni 150 au wamefukuzwa kazi tu. Wanatakiwa walipe na kazi wafukuzwe wasipo lipa washtakiwe.

serekali hii ingekuwa hivyo nisingehama sisiem,mwambie fast jet aanze na mapacha watatu,kinana,jairo na waliouza wale twiga pia walioua reli na viwanda.mkiwashitaki hawa 2015 hamna haja ya kampeni
 
Wamerudisha hizo milioni 150 au wamefukuzwa kazi tu. Wanatakiwa walipe na kazi wafukuzwe wasipo lipa washtakiwe.

kwa Tz haiwezekani, walioiba benki kuu waliambiwa na rais wa wajinga Kikwete warudishe! Umesahau?
 
Wamerudisha hizo milioni 150 au wamefukuzwa kazi tu. Wanatakiwa walipe na kazi wafukuzwe wasipo lipa washtakiwe.

Kumbe mara zingine unafikiri kwa kutumia Kichwa na sio "MASABURI"kama ambavyo tumezoea kukuona ktk Hoja za Msingi!!
Ni ukweli usiopingika kwamba kuwafukuza kazi na Kuwashtaki bila kuwaamuru walipe fedha walizoiba,ni sawa na kuwahalalishia fedha hizo kuwa ni Kiinua Mgongo chao!!

Lazima Kamanda Kova na Wahusika wote wahakikishe kwamba Wanalisafisha Jeshi la Polisi kutokana na Sifa mbaya ambayo imekua nayo sasa kwa muda mrefu kwa ajili ya Polisi wachache wenye Tamaa ya Kutaka Kutajirika haraka haraka kwa njia za Mkato huku wakisahau Wajibu na KANUNI ya Kazi yao!!

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!
MUNGU IBARIKI CHADEMA!!!!
 
Ina maana serikali ya JK imeacha kusiliza maelekezo ya CHADEMA sasa inaongozwa kwa maelekezo ya JAMII FORUMS, selikali ya kipuuzi hii, jamani nakumbuka jana wakati tukijadili yale matapeli ya kipolisi ya TUNDUMA yaliyopeleka sampuli ya chumvi badala ya dawa za kulevya, kuna mchangiaji aliuliza hivi!!! Mbona wezi wa milion 150 hatujawasikia hadi leo ??? lilikuwa swali kwa Nchimbi waziri wa ndani ya nyumba.Cha ajabu leo KOVA kakurupuka bila kupiga mswaki anakuja kutueleza kufukuza hao askari.Je hii ni serikali kweli???? au mazingaombwe.
 
Back
Top Bottom