Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Ukiacha kelele zinazopigwa kwa nguvu Sana hapa nchini Tanzania za kutakiwa, Freeman Mbowe aachiwe huru, kutokana na makosa yanayoonekana wazi kuwa Jeshi la Polisi nchini limeamua "kubambika" ya ugaidi, lakini vyombo mbalimbali vya dunia navyo vimeungana na wapigania haki wa hapa nchini, kama vile mashirika ya habari ya CNN na Aljazeera na BBC, yamejitokeza na kuipa "headline" hiyo taarifa ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kupata tuhuma hiyo nzito ya ugaidi.
Madhara ya serikali hii kumbambikia Freeman Mbowe Makosa hayo ya ugaidi ni makubwa Sana kuliko tunavyofikiria.
Lazima ifahamike wazi kuwa wawekezaji ambao walikuwa wanafikiria kuleta mitaji yao hapa nchini, baada ya kuona mabadiliko ya uongozi wa juu, baada ya kufariki Rais Magufuli, watasita kufanya hivyo, kutokana na kuogopa kuleta mitaji yao kwenye nchi ambayo uongozi wa nchi umeutangazia dunia kuwa kiongozi mkuu wa chama cha upinzani cha Chadema, anatuhuma za ugaidi!
Lakini ukiangalia mwenendo wa viongozi wakuu wa nchi hii, wanatumia mwanya wa wanaodai Katiba yetu ya nchi, kuwabambikia viongozi wa upinzani kwa Makosa yasiyokuwa na dhamana ya ugaidi, kwa lengo tu la kuwakomoa, kutokana na kupigania haki za watanzania, ambapo wao viongozi wa serikali hawapendi watanzania waipate haki hiyo!
Kwa hiyo tutarajie wawekezaji kutoka nchi za nje kupungua Sana kuja hapa nchini kutokana na hofu hii, waliyoianzisha wao viongozi wa serikali, kuwa nchi yetu ina magaidi!