Polisi "wame-underestimate impact" ya kumtuhumu Mbowe kwa makosa ya ugaidi?

Ukiacha kelele zinazopigwa kwa nguvu Sana hapa nchini Tanzania za kutakiwa, Freeman Mbowe aachiwe huru, kutokana na makosa yanayoonekana wazi kuwa Jeshi la Polisi nchini limeamua "kubambika" ya ugaidi, lakini vyombo mbalimbali vya dunia navyo vimeungana na wapigania haki wa hapa nchini, kama vile mashirika ya habari ya CNN na Aljazeera, yamejitokeza na kuipa "headline" hiyo taarifa ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kupata tuhuma hiyo nzito ya ugaidi.

Madhara ya serikali hii kumbambikia Freeman Mbowe Makosa hayo ya ugaidi ni makubwa Sana kuliko tunavyofikiria.

Lazima ifahamike wazi kuwa wawekezaji ambao walikuwa wanafikiria kuleta mitaji yao hapa nchini, baada ya kuona mabadiliko ya uongozi wa juu, baada ya kufariki Rais Magufuli, watasita kufanya hivyo, kutokana na kuogopa kuleta mitaji yao kwenye nchi ambayo uongozi wa nchi umeutangazia dunia kuwa kiongozi mkuu wa chama cha upinzani cha Chadema, anatuhuma za ugaidi!

Lakini ukiangalia mwenendo wa viongozi wakuu wa nchi hii, wanatumia mwanya wa wanaodai Katiba yetu ya nchi, kuwabambikia viongozi wa upinzani kwa Makosa yasiyokuwa na dhamana ya ugaidi, kwa lengo tu la kuwakomoa, kutokana na kupigania haki za watanzania, ambapo wao viongozi wa serikali hawapendi watanzania waipate haki hiyo!

Kwa hiyo tutarajie wawekezaji kutoka nchi za nje kupungua Sana kuja hapa nchini kutokana na hofu hii, waliyoianzisha wao viongozi wa serikali, kuwa nchi yetu ina magaidi!
Tatizo kubwa la viongozi wa Afrika ni kutotambua unyeti wa nafasi wanazo kabidhiwa kikatiba. Badala ya kutembea ndani ya malengo ya kimkakati kwa mustakabali mwema na maslahi mapana ya nchi zao, wao hugeukia "trivial things" ambayo vinawashushia hadhi katika jumuiya ya kimataifa!
 
Inafikirisha sana picha hii.
Screenshot_20210724-071303.jpg
 
Are you serious, na ulinzi wote wa Rais kweli Mdude anaweza hata kugusa kamba za viatu vya Madam?
Nimeshangaa hayo madai ya hao Polisi wetu, kuwa eti Mbowe alipanga njama za kuwaua viongozi wakuu wa serikali!

Baada ya kuona huyo Mbowe yuko "frontline" katika kuidai Katiba mpya, ambapo hao wenye mamlaka hawaitaki kwa maslahi yao binafsi
 
who cares??

mmekosa influence makete na kasulu...itakuwa nje???

nani mtaani ana shida na Mbowe? ushaona kina mtu kaandamana???

Kama ndani leo kuna harusi kibao....hakuna anayemjali wala kumsikiliza Mbowe

Mataifa ya nje wanaopiga kelele ni wasioneemeka na TZ..wanaoneemeka wako kimya!!!!

Jifunzeni kutatua matatizo kwa kuwaza ku win mass ya watanzania na sio nje!!!!!??

pumbavu
Mirembe moja hiyo...
 
Nchi hii haijawah kushughulikia seriously baadhi ya matukio.

Kukamatwa Kwa Mbowe kunaweza kuweka kujibu baadhi ya sintofaham. Mbowe amekuwa akituhumiwa kutumia mbinu nying kubak kuwa madarakani.

Maadam anatuhumiwa tu basi badala ya kushinikizwa aachiwe (mashinikizo ya kipuuzi kabisa) tushinikize sheria isipindishwe katika mwenendo wa kesi yake.
Kutumia mbinu nyingi kubaki madarakani???????aisee POLE SANA MKUU,RUDI TU WODINI HUJAPATA RUKHSA YA DAKTARI
 
Yaani huyo mama yenu ata-regret kwa kwa hizo hasira alizonazo za kutaka kumkomoa Mbowe, kwa kutumia Jeshi "lake" la Polisi, kwa kumtuhumu kiongozi huyo wa upinzani nchini, Freeman Mbowe, kuwa ni gaidi!

Ambapo madhara yake ni makubwa Sana kwa wawekezaji wakubwa wa nchi, kusita kuleta mitaji yao nchini, kwa hofu ya ugaidi
Rais wa nchi 'aregret' kwa sababu ya huyo mbowe? Acheni mzaha! Mbowe ni nani ndani ya nchi hii? Wacha kesi iende mahakamani, mbona kwa Sabaya mlishangilia sana. Malipo ni hapa hapa duniani.
 
Ukiacha kelele zinazopigwa kwa nguvu Sana hapa nchini Tanzania za kutakiwa, Freeman Mbowe aachiwe huru, kutokana na makosa yanayoonekana wazi kuwa Jeshi la Polisi nchini limeamua "kubambika" ya ugaidi, lakini vyombo mbalimbali vya dunia navyo vimeungana na wapigania haki wa hapa nchini, kama vile mashirika ya habari ya CNN na Aljazeera, yamejitokeza na kuipa "headline" hiyo taarifa ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kupata tuhuma hiyo nzito ya ugaidi.

Madhara ya serikali hii kumbambikia Freeman Mbowe Makosa hayo ya ugaidi ni makubwa Sana kuliko tunavyofikiria.

Lazima ifahamike wazi kuwa wawekezaji ambao walikuwa wanafikiria kuleta mitaji yao hapa nchini, baada ya kuona mabadiliko ya uongozi wa juu, baada ya kufariki Rais Magufuli, watasita kufanya hivyo, kutokana na kuogopa kuleta mitaji yao kwenye nchi ambayo uongozi wa nchi umeutangazia dunia kuwa kiongozi mkuu wa chama cha upinzani cha Chadema, anatuhuma za ugaidi!

Lakini ukiangalia mwenendo wa viongozi wakuu wa nchi hii, wanatumia mwanya wa wanaodai Katiba yetu ya nchi, kuwabambikia viongozi wa upinzani kwa Makosa yasiyokuwa na dhamana ya ugaidi, kwa lengo tu la kuwakomoa, kutokana na kupigania haki za watanzania, ambapo wao viongozi wa serikali hawapendi watanzania waipate haki hiyo!

Kwa hiyo tutarajie wawekezaji kutoka nchi za nje kupungua Sana kuja hapa nchini kutokana na hofu hii, waliyoianzisha wao viongozi wa serikali, kuwa nchi yetu ina magaidi!
Wawekezaji hawawezi kushindwa kuja Tanzania kwasababu ya wahuni kama Mbowe. Walijaribu kumdharau Mama sasa wacha waone cha moto.
 
Mtu afanye vurugu aachiwe sababu tu ya kuogopa wawekezaji? Huo ni upuuzi
Imenenwa kwenye Biblia, kitabu cha Mithali 14:34

Haki huinua Taifa, bali dhambi ni aibu kwa watu wote

Hivi hudhani hilo suala la Jeshi letu la Polisi, kumbambikia Mbowe kesi ya ugaidi, kuwa ni aibu kwa serikali nzima ya CCM?
 
Imenenwa kwenye Biblia, kitabu cha Mithali 14:34

Haki huinua Taifa, bali dhambi ni aibu kuwa watu wote

Hivi hudhani hilo suala la Jeshi letu la Polisi, kumbambikia Mbowe kesi ya ugaidi, kuwa ni aibu kwa serikali nzima ya CCM?
Una hakika gani kama kabambikiwa? So wewe unaamini Mwamba hawezi kukosea?
 
Ukiacha kelele zinazopigwa kwa nguvu Sana hapa nchini Tanzania za kutakiwa, Freeman Mbowe aachiwe huru, kutokana na makosa yanayoonekana wazi kuwa Jeshi la Polisi nchini limeamua "kubambika" ya ugaidi, lakini vyombo mbalimbali vya dunia navyo vimeungana na wapigania haki wa hapa nchini, kama vile mashirika ya habari ya CNN na Aljazeera, yamejitokeza na kuipa "headline" hiyo taarifa ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kupata tuhuma hiyo nzito ya ugaidi.

Madhara ya serikali hii kumbambikia Freeman Mbowe Makosa hayo ya ugaidi ni makubwa Sana kuliko tunavyofikiria.

Lazima ifahamike wazi kuwa wawekezaji ambao walikuwa wanafikiria kuleta mitaji yao hapa nchini, baada ya kuona mabadiliko ya uongozi wa juu, baada ya kufariki Rais Magufuli, watasita kufanya hivyo, kutokana na kuogopa kuleta mitaji yao kwenye nchi ambayo uongozi wa nchi umeutangazia dunia kuwa kiongozi mkuu wa chama cha upinzani cha Chadema, anatuhuma za ugaidi!

Lakini ukiangalia mwenendo wa viongozi wakuu wa nchi hii, wanatumia mwanya wa wanaodai Katiba yetu ya nchi, kuwabambikia viongozi wa upinzani kwa Makosa yasiyokuwa na dhamana ya ugaidi, kwa lengo tu la kuwakomoa, kutokana na kupigania haki za watanzania, ambapo wao viongozi wa serikali hawapendi watanzania waipate haki hiyo!

Kwa hiyo tutarajie wawekezaji kutoka nchi za nje kupungua Sana kuja hapa nchini kutokana na hofu hii, waliyoianzisha wao viongozi wa serikali, kuwa nchi yetu ina magaidi!
Ivi hii dhana ya kwamba wanasiasa wa upinzan hawakosei au hawana makosa?
Kwamfano ushahidi ukaonesha amehusika kwenye ugaidi mtakubali? Acheni sheria ifuatwe kama kweli hana makosa akaithibitishie mahakama hivyo vyombo vya habari vya kimataifa havitasaidia chochote zaid ya propaganda tu mana ndo wanachokipenda
 
Are you serious, na ulinzi wote wa Rais kweli Mdude anaweza hata kugusa kamba za viatu vya Madam?
Dada yangu kipi kinashindikana?!!

Rais wa Ufaransa mh.Macron alipigwa makofi na raia wake.....

Mh.Mzee Mwinyi alipigwa makofi na yule kijana chizi.....

George Bush alipigwa KIATU kule Iraq.....

Usicheze na BINADAMU ....

Mdude Nyagali amemtisha Rais....ametutisha wananchi kuwa "ATAUTUMIA WEMBE ALIOMNYOLEA HAYATI MAGUFULI KUMYOA MH.RAIS SSH ,na akahanikiza sisi UVCCM tumwambie mama yetu kuwa yeye hamuogopi"

Unataka hayo maneno tuyachukulie kirahisi?!! 🤣🤣

Unataka tusihoji kwanini 2+2=5?

#NchiKwanza
#KaziInaendelea
 
Sehemu salama ya Gaidi ni jela, Mbowe yupo sehemu anayostahili, anapiga story na kunguni tu, hakuna mwekezaji serious anayeona Mbowe ni mtu muhimu, hizi story zenu za vijiweni zibaki huko huko kwa nyumbxxx wenzio.

Mbowe hamtamuweza kumuweka mahabusu hamjaanza leo sana sana mnampaisha homa kali ya katiba mpya ndio inawafanya mshikwe na matumbo ya kuharisha katiba mpya mpya ndio suluhisho la haya yote.
 
Yaani huyo mama yenu ata-regret kwa kwa hizo hasira alizonazo za kutaka kumkomoa Mbowe, kwa kutumia Jeshi "lake" la Polisi, kwa kumtuhumu kiongozi huyo wa upinzani nchini, Freeman Mbowe, kuwa ni gaidi!

Ambapo madhara yake ni makubwa Sana kwa wawekezaji wakubwa wa nchi, kusita kuleta mitaji yao nchini, kwa hofu ya ugaidi
Kila ukipita mitaani, hata wale wwnaCCM wenye akili timamu, wanasema wazi kuwa kwenye hili huyu Bibi ameharibu, na kukitia aibu chama.
 
Nchi za MAGHARIBI na UGAIDI....

Unapotaja tu ugaidi ,Magaidi ,gaidi ujue nchi za MAGHARIBI hushtuka mno......nimeshangaa eti unasema kuwa NCHI HIZO ZITAKUWA NA HURUMA na wahusika wa vitendo hivyo......

Hivi ni lini nchi hizo zimeanza kuwa na HURUMA NA KUGUSWA NA WANAOHUSIKA NA HAYO MAMBO?!!!

Kwao ukituhumiwa ugaidi basi ujue utatambulika sio gaidi mpaka pale MAHAKAMA ikithibitisha hayo......

Kutuhumiwa si KUHUKUMIWA....

Tusubiri mahakama ifanye kazi yake.....

Nasubiri mahakama ifanye kazi yake zaidi ya humu mitandaoni KUHUKUMU kuwa ANA/HANA HATIA......

#MahakamaNiMuhimiliWaNchi
#KaziIendelee
Kwa ujinga huu alioufanya huyu bibi, hakuna mwenye busara Duniani atakayemsikiliza kwa lolote.

Nchi za Magharibi zinafuatilia sana maana alichokifanya huyu bibi hakina tofauti na kilichofanywa na utawala dikteta wa Syria. Wapinzani waliwaita magaidi wakitegemea nchi za Magharibi zitawaunga mkono, kinyume chake, walitajwa magaidi ndio waliosaidiwa na mataifa yote makubwa isipokuwa Urusi iliyoamua kusimama na Serikali ya kidikteta.
 
Hivi Tanzania hakujawahi kutokea Magaidi ?!!!

Misaada ya USAID ,GTZ JICA,DANIDA ilisitishwa/kupunguza walipotokea Magaidi kule KIBITI ,AMBONI TANGA na MTWARA?!!!

Je nao wawekezaji hawakujitokeza kipindi hicho ?!!!

Je UAMSHO walipotuhumiwa kwa ugaidi na kukaa ndani miaka 8 WAWEKEZAJI HAWAKUJITOKEZA ?!!!

KWA NINI Hofu ya kukosa WAWEKEZAJI IJE kipindi hiki cha KUTUHUMIWA mh.Mbowe ?!!!

TUHUMA huthibitishwa mahakamani tu .....

#KaziIendelee
Wawekezaji hawatakuja Tanzania siyo kwa sababu Mbowe amebambikiwa kesi ya ugaidi na Samia, bali ujumbe utakaotumwa Duniani, ni kuwa Tanzania siyo mahali salama maana unaweza kubambikiwa kesi yoyote na watawala wakati wowote, alimradi wakiamua kufanya hivyo.
 
Hizi tuhuma anazotuhumiwa Mbowe za ugaidi, hata ukimueleza mtoto mdogo anayesoma chekechea atajua kuwa Jeshi la Polisi limembambikia.

Hivi hili Jeshi la Polisi halioni aibu hata aina ya kubambika kesi?

Eti wanadai kuwa Mbowe alipanga njama za kuwaua viongozi wakuu wa serikali!
Mkuu ninachokijua hawajawahi kumshinda mbowe mahakamani ni issue ya muda tu watamwachia.Hiyo kesi ni ya kubumba na inaenda kuwaumbua na kuwaaibisha ila mama ataathiriwa vibaya na hawa washauri wake ambao wanamtoa nje ya reli wanataka aone kiti kigumu hivyo asema hagombei tena 2025.
 
Sehemu salama ya Gaidi ni jela, Mbowe yupo sehemu anayostahili, anapiga story na kunguni tu, hakuna mwekezaji serious anayeona Mbowe ni mtu muhimu, hizi story zenu za vijiweni zibaki huko huko kwa nyumbxxx wenzio.
Tozo za miamala ziko juu!!!... Makampuni ya simu yameanza kupiga mayowe!!!...wateja hakuna!!...Alafu tunasikia kuna Gaidi tena!!!.. Unadhani tukajenge Uchumi wa Namna gani?!!..
 
Si kweli ulisemalo.....

Unaongea KIHISIA zaidi ya mifano hai mingi ya KIUHALISIA....

Kule nchini Rwanda ,mpinzani wa serikali ,bi VICTOIRE INGABIRE alituhumiwa UGAIDI.....wawekezaji hawakuacha kuwekeza RWANDA....

#KaziIendelee
Ni wawekezaji gani wa maana waliopo Rwanda? Ni wawekezaji gani wa maana wapya waliokuja Tanzania wakati wa utawala wa Magufuli?

Wawekezaji wa maana, ni wale wawekezaji makini na wanaowekeza angalao kuanzia dola milioni 500. Wa mwisho natambua kuwa alikuwa Dangote, wakati wa utawala wa Kikwete.
 
Back
Top Bottom