Polisi "wame-underestimate impact" ya kumtuhumu Mbowe kwa makosa ya ugaidi?

Polisi "wame-underestimate impact" ya kumtuhumu Mbowe kwa makosa ya ugaidi?

MATAGA mnaungana na Mbowe kumuharibia Mama...

Hatukubali.
Hizi tuhuma anazotuhumiwa Mbowe za ugaidi, hata ukimueleza mtoto mdogo anayesoma chekechea atajua kuwa Jeshi la Polisi limembambikia.

Hivi hili Jeshi la Polisi halioni aibu hata aina ya kubambika kesi?

Eti wanadai kuwa Mbowe alipanga njama za kuwaua viongozi wakuu wa serikali!
 
Wewe ndio unamu-underestimate Rais Samia Suluhu Hassan

Hakuna atayedharau au kutishia mamlaka ya Rais halafu akaachwa bila kuulizwa

ACHA KAZI IENDELEE
 
Huu ujinga upinzani utawa cost sana, Term iliyopita, madai yale yale ya mashirika ya nchi na vikwazo lkn wajue hao wanaowaita wawekezaji wako na interest ya faida sio mtu.

Halafu bora hata walalamike nchi za kiarabu au mashariki ya mbali sio hao watawala wetu wa zamani.
Mambo yamebadilika sana hata china anataka koloni kwahiyo wao wakilinga China anaona fursa
 
Hizi tuhuma anazotuhumiwa Mbowe za ugaidi, hata ukimueleza mtoto mdogo anayesema chekechea atajua kuwa Jeshi la Polisi limembambikia
Hajiheshim... Wacha ajifunze..
 
Ukiacha kelele zinazopigwa kwa nguvu Sana hapa nchini Tanzania za kutakiwa, Freeman Mbowe aachiwe huru, kutokana na makosa yanayoonekana wazi kuwa ni ya "kubambika" ya ugaidi, lakini vyombo mbalimbali vya dunia navyo vimeungana na wapigania haki wa hapa nchini, kama vile mashirika ya habari ya CNN na Aljazeera, yamejitokeza na kuipa "headline" hiyo taarifa ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kupata tuhuma hiyo nzito ya ugaidi.

Madhara ya serikali hii kumbambikia Freeman Mbowe Makosa hayo ya ugaidi ni makubwa Sana kuliko tunavyofikiria.

Lazima ifahamike wazi kuwa wawekezaji ambao walikuwa wanafikiria kuleta mitaji yao hapa nchini, baada ya kuona mabadiliko ya uongozi wa juu, baada ya kufariki Rais Magufuli, watasita kufanya hivyo, kutokana na kuogopa kuleta mitaji yao kwenye nchi ambayo uongozi wa nchi umeutangazia dunia kuwa kiongozi mkuu wa chama cha upinzani cha Chadema, anatuhuma za ugaidi!

Lakini ukiangalia mwenendo wa viongozi wakuu wa nchi hii, wanatumia mwanya wa Katiba yetu ya nchi, kuwabambikia viongozi wa upinzani kwa Makosa yasiyokuwa na dhamana ya ugaidi, kwa lengo tu la kuwakomoa, kutokana na kupigania haki za watanzania, ambapo wao viongozi wa serikali hawapendi watanzania waipate haki hiyo!

Kwa hiyo tutarajie wawekezaji kutoka nchi za nje kupungua Sana kuja hapa nchini kutokana na hofu hii, waliyoianzisha wao viongozi wa serikali, kuwa nchi yetu ina magaidi!
Akili ya kipumbavu Sana, kwamba tumuache mtu afanye anavyotaka yy na kutishia hadi viongozi kwa kuogopa eti wawekezaji wataogopa kuja kuwekeza,Tanzania ni nchi huru na Ina Rais anaye iongoza na watu wote tunatakiwa kutii mamlaka ya nchi,
Sasa hutii chochote, unajiamulia tu kwa kudharau kuwa kiongozi ni mwanamke, Tena unamlazimisha kabisa eti ukae nae uongee nae,na unasema waziwazi kuwa utafanya chochote,unaenda mbali zaidi kumwambia uta mnyolea wembe ulio mnyolea mtangulizi wake, na mtangulizi wake Kesha kufa, unategemea mama akuache t?
Point yangu hapo nikwamba tutii mamlaka husika, hakuna aliye juu ya Rais, wala Wazungu hawawezi kutuingilia,
 
Nchi za MAGHARIBI na UGAIDI....

Unapotaja tu ugaidi ,Magaidi ,gaidi ujue nchi za MAGHARIBI hushtuka mno......nimeshangaa eti unasema kuwa NCHI HIZO ZITAKUWA NA HURUMA na wahusika wa vitendo hivyo......

Hivi ni lini nchi hizo zimeanza kuwa na HURUMA NA KUGUSWA NA WANAOHUSIKA NA HAYO MAMBO?!!!

Kwao ukituhumiwa ugaidi basi ujue utatambulika sio gaidi mpaka pale MAHAKAMA ikithibitisha hayo......

Kutuhumiwa si KUHUKUMIWA....

Tusubiri mahakama ifanye kazi yake.....

Nasubiri mahakama ifanye kazi yake zaidi ya humu mitandaoni KUHUKUMU kuwa ANA/HANA HATIA......

#MahakamaNiMuhimiliWaNchi
#KaziIendelee
Nchi za magharibi zina details zote za Magaidi huwa hazisubiri kutajiwa majina na polisi wa Tz. Hivyo wanajua everything
 
Yaani huyo mama yenu ata-regret kwa kwa hizo hasira alizonazo za kutaka kumkomoa Mbowe, kwa kutumia Jeshi "lake" la Polisi, kwa kumtuhumu kiongozi huyo wa upinzani nchini, Freeman Mbowe, kuwa ni gaidi!

Ambapo madhara yake ni makubwa Sana kwa wawekezaji wakubwa wa nchi, kusita kuleta mitaji yao nchini, kwa hofu ya ugaidi
Amkomoe Kwa kipi aisee?

Si tunataka utawala wa sheria?

Hana mamlaka ya kuingilia mahakama
 
Ukiacha kelele zinazopigwa kwa nguvu Sana hapa nchini Tanzania za kutakiwa, Freeman Mbowe aachiwe huru, kutokana na makosa yanayoonekana wazi kuwa Jeshi la Polisi nchini limeamua "kubambika" ya ugaidi, lakini vyombo mbalimbali vya dunia navyo vimeungana na wapigania haki wa hapa nchini, kama vile mashirika ya habari ya CNN na Aljazeera, yamejitokeza na kuipa "headline" hiyo taarifa ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kupata tuhuma hiyo nzito ya ugaidi.

Madhara ya serikali hii kumbambikia Freeman Mbowe Makosa hayo ya ugaidi ni makubwa Sana kuliko tunavyofikiria.

Lazima ifahamike wazi kuwa wawekezaji ambao walikuwa wanafikiria kuleta mitaji yao hapa nchini, baada ya kuona mabadiliko ya uongozi wa juu, baada ya kufariki Rais Magufuli, watasita kufanya hivyo, kutokana na kuogopa kuleta mitaji yao kwenye nchi ambayo uongozi wa nchi umeutangazia dunia kuwa kiongozi mkuu wa chama cha upinzani cha Chadema, anatuhuma za ugaidi!

Lakini ukiangalia mwenendo wa viongozi wakuu wa nchi hii, wanatumia mwanya wa wanaodai Katiba yetu ya nchi, kuwabambikia viongozi wa upinzani kwa Makosa yasiyokuwa na dhamana ya ugaidi, kwa lengo tu la kuwakomoa, kutokana na kupigania haki za watanzania, ambapo wao viongozi wa serikali hawapendi watanzania waipate haki hiyo!

Kwa hiyo tutarajie wawekezaji kutoka nchi za nje kupungua Sana kuja hapa nchini kutokana na hofu hii, waliyoianzisha wao viongozi wa serikali, kuwa nchi yetu ina magaidi!

who cares??


mmekosa influence makete na kasulu...itakuwa nje???


nani mtaani ana shida na Mbowe? ushaona kina mtu kaandamana???

Kama ndani leo kuna harusi kibao....hakuna anayemjali wala kumsikiliza Mbowe

Mataifa ya nje wanaopiga kelele ni wasioneemeka na TZ..wanaoneemeka wako kimya!!!!


Jifunzeni kutatua matatizo kwa kuwaza ku win mass ya watanzania na sio nje!!!!!??


pumbavu
 
Nchi hii haijawah kushughulikia seriously baadhi ya matukio.

Kukamatwa Kwa Mbowe kunaweza kuweka kujibu baadhi ya sintofaham. Mbowe amekuwa akituhumiwa kutumia mbinu nying kubak kuwa madarakani.

Maadam anatuhumiwa tu basi badala ya kushinikizwa aachiwe (mashinikizo ya kipuuzi kabisa) tushinikize sheria isipindishwe katika mwenendo wa kesi yake.
 
Sijasema wana unabiii wa matukio yanayoenda kutokea.Nimesema wana taarifa za watu gani au vikundi vipi ni vya magaidi.Kama Mbowe vile hawahitaji kuambiwa na Polisi Tanzania kuwa Mbowe Ni gaidi.Wao wenyewe kupitia vyombo vyao wanajua kuwa Mbowe Ni gaidi au sio gaidi.
Kujua fulani kuwa Ni mwizi sio kwamba ndio kujua kuwa lini atakuja kukuibia
Kwani UGAIDI hauwezi kufanywa na MTU MMOJA ?!!!

Hivi MAJAMBAZI hawawezi kujiongeza na kutenda UGAIDI ?!!

Unapoongelea ugaidi halafu mathalani UKAMFIKIRIA gaidi Osama na mitandao yake basi ujue hutofikiria kuwa MTU BAKI /WATU BAKI wanaweza kutaka kufanya UHUJUMU dhidi ya WATU WASIO NA HATIA NA JAMII kwa MALENGO WANAYOWAJUA WAO......

Sasa hao usemao "wanafahamu" matendo hayo wana taarifa ya VIBAKA/MAJAMBAZI NA WAHALIFU kote duniani ?!!

#KaziIendelee
 
Dai la katiba mpya linatishiaje mamlaka ya Rais?

Tatizo ni kuunganisha dai la katiba na ule wembe mliotumia kwa mtangulizi na mnaotaka kuendelea kuutumia sasa kwa mama Rais
 
Sehemu salama ya Gaidi ni jela, Mbowe yupo sehemu anayostahili, anapiga story na kunguni tu, hakuna mwekezaji serious anayeona Mbowe ni mtu muhimu, hizi story zenu za vijiweni zibaki huko huko kwa nyumbxxx wenzio.
We binti umeolewa?
 
Nchi hii haijawah kushughulikia seriously baadhi ya matukio.

Kukamatwa Kwa Mbowe kunaweza kuweka kujibu baadhi ya sintofaham. Mbowe amekuwa akituhumiwa kutumia mbinu nying kubak kuwa madarakani.

Maadam anatuhumiwa tu basi badala ya kushinikizwa aachiwe (mashinikizo ya kipuuzi kabisa) tushinikize sheria isipindishwe katika mwenendo wa kesi yake.
Kwa mahakama zipi?

Ndiyo maana tunashinikiza tupate Katiba mpya ya nchi, ili kila mhimili uwe huru, pamoja na mihimili hiyo miwili ya Judiciary na Legislature.

Hiyo ndiyo hofu kuu inayowapata hivi sasa watawala wetu, Hadi walazimike "kutunga" uongo kuwa Mbowe ni gaidi
 
Back
Top Bottom