Wewe ungekuwa ná uvumilivu kama babaako angetandikwa risasi 16 bila kuwa ná hatia yoyote ile? Wewe ungekuwa na uvumilivu kama Ben Saanane na Azory wangekuwa ni ndugu zako Baba mmoja mama mmoja halafu wanapotea kinyemela na Serikali kugoma kufanya uchunguzi?
FYI Chadema wamekuwa wavumilivu kwa miaka 30 sasa. Nchi ina mfumo wa vyama vingi tangu 1991 lakini katiba ya nchi ni ile ta chama kimoja!? Unataka wawe wavumilivu kwa muda gani ili wewe uridhike ná uvumilivu wa Chadema? Miaka 30 mingine!? 😳😳😳😳
Natambua unachokihisi Mkuu.
Mie pia sijaridhishwa na matendo yaliyofanywa na CCM uliyoyabainisha hapo juu na nayakumbuka vizuri.
Uchaguzi uliyofanyika 2020 yalitokea mambo ya ajabu mengi haswa ya kutumia sehemu ya jeshi na kusababisha mauaji yaliyotekea Znz na huku bara. Wengi wa raia hawakujua nini kilichotokea kwa sababu ya kuminywa kwa vyombo vya habari. Magari jeshi na vikosi vilivyopelekwa Znz vilipitishwa njia ya Bagamoyo kwa sababu vingepita mjini raia wengi wangehoji na ingelijenga sintofahamu kubwa sana.
Halikadhalika nguvu iliyotumika bara na wizi wa kura uliyofanyika wa wazi laiti kungelikuwa na uhuru wa vyombo vya habari Mungu pekee ndiye anayejua ni kipi kingelitokea. Ina maana gani hii?
Miongoni mwa Uzi zilizoletwa uchaguzi wa 2020 mmoja miongoni mwa mwana Jf aliandika "Hii nchi inaonekana vyombo vya dola anayelindwa wa kwanza ni M/kti wa chama tawala ambaye ni rais wa pili na wa mwisho raia". Licha ya kuwa na hivyo vyote lakini bado dola ilijihami kwa kuficha mambo mengi ya raia kupata habari yaliyofanyika uchaguzi wa 2020.
Watu wanaweza kulishinda jeshi ndicho ninachomaanisha. Na hii hofu dola wanaonekana wanayo! Na ari ya namna hii raia walikuwa nayo pia uchaguzi wa mwaka 2015 mpaka Kikwete akasema alidhani CCM ingelimfia mikononi mwake.
Ninachomaanisha ni kuwa: Unapotaka kupambana na CCM wekeza kwa raia. Hata wazee wetu walipokuwa wanadai uhuru waliwekeza kwa raia. Walitembea na baiskeli siku kwa siku. Ni watu pekee tu ndiye wanaouwezo wa kuondoa udhalimu madarakani. Hata Lissu alipoulizwa kuhusu mustakabali wa Tz alijibu ni waTz wenyewe ndiyo waliyoshindwa kuikomboa nchi yao.
Jeshi la nchi linafahamu amani inapokesekana ndani ya nchi inakuwaje kwa sababu wana mission tofauti tofauti na wameyaona katika nchi nyengine. Hivyo hawataruhusu ujinga wa namna hiyo wa kutwanga watu mitaani utokee. Mfano halisi baada ya kifo cha Pogba inafahamika ni kipi Jeshi walichokifanya.
Hitimisho: Kwenye hii mission ilipofelia Chadema ilienda chama kama chama kwa sababu ilikuwa imebeba machungu ya waliyofanyiwa na Chama hikihiki CCM awamu iliyopita na hiyo ni hisia. Ninachokiamini mimi CCM kupambana nae haitaji hisia! Inahitajika akili na mipango madhubuti unaokumbuka kuwa raia ndiyo mtaji wao.