Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siyo kweli na wala hizo siyo vurugu, unajua kuwa leo kuna mechi ya simba na yanga? Hapo corona inakuwa likizo au hilo walizungumziaje? Ok waweza weka ushahidi/clip ya Mbowe akiwaita wajinga?Rais, ambaye ni amiri jeshi mkuu, kasema subirini kwanza mambo ya katiba mpya, yeye anaanzisha makongamano (ni uasi huo). RC na DC wanasema ili kudhibiti corona tupunguze mikusanyiko isiyo ya lazima, ya lazima iombewe kibali, yeye anawaita wajinga. Huoni kama hizo ni chokochoko?
Ulitaka awe Musiba?Yaani mmetafuta mtu wenu mmoja huko Birmigham eti ndio mchambuzi wa demokrasia yaAfrica??
Ulitaka awe Musiba?Yaani mmetafuta mtu wenu mmoja huko Birmigham eti ndio mchambuzi wa demokrasia yaAfrica??
Nashangaa hadi saivi Gwantanamu hawajaomba tu export mtu wao wakamuhifadhi gereza kuu la magaidi Duniani.Sehemu salama ya Gaidi ni jela, Mbowe yupo sehemu anayostahili, anapiga story na kunguni tu, hakuna mwekezaji serious anayeona Mbowe ni mtu muhimu, hizi story zenu za vijiweni zibaki huko huko kwa nyumbxxx wenzio.
Nani mama?Hajiheshim... Wacha ajifunze..
Sukuma Gang wamemset naye kajaa mzima mzima kwenye fremu yao,walio wanagongesheana glassToka nchi hii ipate uhuru kuna kesi kama mbili ama tatu za Uhaini. Lakini toka tumepata kuanza mfumo wa vyama vingi vya kisiasa kumekuwepo na kamatakamata hasa kule ambapo Samia katoka Zanzibar kutokana na mfumo wao wa Siasa za chuki.
Magufuli alikuwa mhuni tu na ukatili wake wa kumalizana kikatili kisiasa kwa Wapinzani wake uongozi wake uliweza kutumia mfumo wa kueliminate Wapinzani mfano hai ni tukio la Lissu. Pamoja na mambo yake kidogo alikuwa na haya ama aibu kwa kuogopa kuonekana mbele ya jamii ya wastaarabu ukatili wake kukaundwa msemo wa watu wasiojulikana.
Huyu mama sijui anatafuta nini ama haelewi kuwa kapachikwa pasi moja mbaya sana kutokana na kusifiwa kuwa anaupiga mwingi sasa kapewa pasi mkasi kwa kumpa Kiongozi wa Chama kikuu cha Upinzania kesi ya Ugaidi. Mama ajue kabisa kajitafutie ubaya na waliokuwa wanampenda.
Hofu yake ni nini kwani angeacha haya makongamano ya kudai katiba mpya angepungukiwa na nini? Kenya wanaupinzani Mkubwa na kufikia hatua ya Mpinzani kujiapisha kuwa Rais wa watu wa Kenya hatukusikia Ugaidi wala Uhaini.
Mama nakutabiria utaongoza hii nchi kwa hofu kubwa sana. Tegua huu mtego ambao wapinzani wako ndani ya CCM hasa akina Mwigulu wanakupigia ngoma unaicheza.
Zipa masikio acha kukanyaga Katiba ruhusu watu waongee. Wewe ni mama unajisikiaje mtoto wa mwanamke mwenzio anasokomezwa kesi ngumu kuwa na huruma.
Kwani unatununulia wewe bando?Lialia wa mbowe wiki hii si simu zenu zitaisha wino kuandika nyuzi kila dakika
Hata kama wamekung'oa ubongo unadhani Mbowe ni gaidi ?Yaani mmetafuta mtu wenu mmoja huko Birmigham eti ndio mchambuzi wa demokrasia yaAfrica??
Ukiacha kelele zinazopigwa kwa nguvu Sana hapa nchini Tanzania za kutakiwa, Freeman Mbowe aachiwe huru, kutokana na makosa yanayoonekana wazi kuwa Jeshi la Polisi nchini limeamua "kubambika" ya ugaidi, lakini vyombo mbalimbali vya dunia navyo vimeungana na wapigania haki wa hapa nchini, kama vile mashirika ya habari ya CNN na Aljazeera na BBC, yamejitokeza na kuipa "headline" hiyo taarifa ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kupata tuhuma hiyo nzito ya ugaidi.
Madhara ya serikali hii kumbambikia Freeman Mbowe Makosa hayo ya ugaidi ni makubwa Sana kuliko tunavyofikiria.
Lazima ifahamike wazi kuwa wawekezaji ambao walikuwa wanafikiria kuleta mitaji yao hapa nchini, baada ya kuona mabadiliko ya uongozi wa juu, baada ya kufariki Rais Magufuli, watasita kufanya hivyo, kutokana na kuogopa kuleta mitaji yao kwenye nchi ambayo uongozi wa nchi umeutangazia dunia kuwa kiongozi mkuu wa chama cha upinzani cha Chadema, anatuhuma za ugaidi!
Lakini ukiangalia mwenendo wa viongozi wakuu wa nchi hii, wanatumia mwanya wa wanaodai Katiba yetu ya nchi, kuwabambikia viongozi wa upinzani kwa Makosa yasiyokuwa na dhamana ya ugaidi, kwa lengo tu la kuwakomoa, kutokana na kupigania haki za watanzania, ambapo wao viongozi wa serikali hawapendi watanzania waipate haki hiyo!
Kwa hiyo tutarajie wawekezaji kutoka nchi za nje kupungua Sana kuja hapa nchini kutokana na hofu hii, waliyoianzisha wao viongozi wa serikali, kuwa nchi yetu ina magaidi!
Mtaa gani Mheshimiwa?Kila ukipita mitaani, hata wale wwnaCCM wenye akili timamu, wanasema wazi kuwa kwenye hili huyu Bibi ameharibu, na kukitia aibu chama.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Eti hata china anataka koloni. Yani tumeshatawaliwa mpaka tumechukulia ni kawaidaHuu ujinga upinzani utawa cost sana, Term iliyopita, madai yale yale ya mashirika ya nchi na vikwazo lkn wajue hao wanaowaita wawekezaji wako na interest ya faida sio mtu.
Halafu bora hata walalamike nchi za kiarabu au mashariki ya mbali sio hao watawala wetu wa zamani.
Mambo yamebadilika sana hata china anataka koloni kwahiyo wao wakilinga China anaona fursa
Sasa Mkuu hii ni akili yenu. Vipi na wao wakitumia akili kama ya kwenu? Mtafanyaje sasa?MUJINI tunasema IMEKULA KWAO sasa polisiccm wanahaha jinsi ya kumuachia mtuhumia wa ugaidi bila dhamana. Ngoja tusubiri tuone hii kasheshe inavyoendelea. Nimetokea kuipenda sana Twitter kwani kwenye sakata kama hili la Mbowe ni rahisi sana kuvitag vyombo vya habari vikubwa duniani ná pia Viongozi wakubwa duniani hasa wale wa nchi za Magharibi AKA BEBERUS,
Sasa Mkuu hii ni akili yenu. Vipi na wao wakitumia akili kama ya kwenu? Mtafanyaje sasa?
Ninachokiona hapa hamuwakomoi bali mnarahisisha kazi yao.
Suala jengine ni kuvitag vyombo vikubwa ili kuwapa taarifa kinachoendelea nchini kuhusu haswa kinachoitwa demokrasia. Najaribu kuvuta kumbukumbu kipindi cha Magu nguvu aliyoitumia ilikuwa ni kubwa sana na hao Jumuiya za Kimataifa hawakufanya wengi waliyokuwa wakiyataraji.
Tumeona Uganda kilichotokewa kwa Bobby Wine si kizuri lakini hamna walichokifanya na sehemu nyengine tofauti tofauti. Hii inatupa nini?
Cha ziada na cha umuhimu Chadema iwekeze zaidi kwa umma wa Wtz wenyewe ili Wtz wenyewe wawaamini kama ilivyokuwa 2010. Mbali na hapo kwa hizi njia mnazozitumia mtaonekana vibaraka wa nchi za nje.
Kwa jinsi unavyochangia humu inaonekana umepata cheo hivi karibuni ambacho hukustahili kukipata na bahati mbaya sana cheo hicho ni kila kitu kwako na unaamini utaishi nacho Milele.Nchi za MAGHARIBI na UGAIDI....
Unapotaja tu ugaidi ,Magaidi ,gaidi ujue nchi za MAGHARIBI hushtuka mno......nimeshangaa eti unasema kuwa NCHI HIZO ZITAKUWA NA HURUMA na wahusika wa vitendo hivyo......
Hivi ni lini nchi hizo zimeanza kuwa na HURUMA NA KUGUSWA NA WANAOHUSIKA NA HAYO MAMBO?!!!
Kwao ukituhumiwa ugaidi basi ujue utatambulika sio gaidi mpaka pale MAHAKAMA ikithibitisha hayo......
Kutuhumiwa si KUHUKUMIWA....
Tusubiri mahakama ifanye kazi yake.....
Nasubiri mahakama ifanye kazi yake zaidi ya humu mitandaoni KUHUKUMU kuwa ANA/HANA HATIA......
#MahakamaNiMuhimiliWaNchi
#KaziIendelee
Kama hili linatambulika yeye rais akaomba apatiwe muda ili aliweke vizuri hili. Kuna miradi mikubwa ipo nje ya uwezo wa serikali imeachwa na awamu iliyopita.Hataki kujifunza na kubadirika. Mwendazake alivuruga Uchumi na maisha ya kila mtu kwa kuendekeza visasi na siasa za hovyo zilizoitumbukiza Nchi shimoni
Niweke wazi msimamo wangu sina chama!Maccm mtaji wao mkubwa ni ujinga uliokithiri nchini. Kwa Watanzania wanaojitambua wanasimama bega kwa bega na Chadema. Unadhani ni kwanini maccm YANAHOFIA Katiba mpya ná Tume huru ya uchaguzi Mkuu!?
Niweke wazi msimamo wangu sina chama!
Hao watanzania wanaosimama bega kwa bega kwa hili siwaoni zaidi ya mitandao miwili ya Jf na Twitter. Amini ninachokuambia kuna wengine hawajui kama Mbowe kakamatwa! Hawajui kama Chadema inadai katiba mpya! Na ni watu wa hapa mjini kabisa!
Ila nilichokiona kwa wale ambao wanaolifahamu hili wanaona ni Makosa ya Mbowe kwa hili kwa sababu siyo hisani rais kutenda haki bali ni kwa mujibu wa sheria ila Mbowe na Chadema wakumbuke ni wapi walipotoka wakikusudia awamu iliyopita kwa maana uhuru unaopatikana sasa hivi tofauti na awamu iliyopita na kesi za wafungwa wa kisiasa zilikuwa zinaachiliwa ama kufutwa na Mbowe mahakama imetaka arudishiwe fedha zake.
Tutarudi tena kwa kufanywa haya si hisani bali ni sheria. Sasa ingeliwafaa wakumbuke ni wapi walipotoka. Mbali na hilo hii nchi ameipokea ikiwa na uchumi hoi. Miradi mikubwa imeachwa kuliko uwezo wa serikali, wahitimu hawana ajira, sekta binafsi zipo hoi n.k kwa hili akaomba apatiwe muda ili atengeneze mazingira yawe angalau kwa kiasi chake. Na ndicho raia wanachokilalamikia kwa sasa.
Sasa ni kipi kilichomfanya Mbowe na Chadema wakose uvumilivu?