Tetesi: Polisi wamempiga daktari mwenzetu mpaka kalazwa ICU

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
2,853
Reaction score
4,503
Yule jamaa aliyeonekana wakitoshana na traffic pale mwenye ni Daktari bingwa wa internal medicine,kwenye gari alikuwa ameweka koti jeupi nyuma ya kiti, wanajeshi wakamchukua, hatujui walimpeleka wapi, na jamaaa alikuwa anawahi kazini mloganzila.

Taarifa ni kwamba yupo hospital ICU, sasa ndugu zangu polisi mnatambulika vizuri sana,tutaoneshana huku hospitali,kwanini msimfungulie mashitaka?
 
Mimi nipo na nyinyi madaktari wetu.
 
Siku zote, jitahidi sana uepukane na mizozo na shari zisizo za lazima.

Yes, umemtandika Trafiki.

Nawe umeishia kupigwa mno na bado kuna kesi inakusubiri. Utapoteza muda, fedha na mambo mengi mno.

Sikufundishi kuwa muoga, ila tafakari popote uepukane na matumizi ya nguvu ya ovyo.

Uanaume si kushikana mashati. Uanaume ni uwezo wa kutumia akili kung'amua athari za maamuzi yako kabla hujatenda na kuamua.

Natoa pole kwa Daktari mwenzetu. Polisi fateni taratibu.
 
Utaratibumpolisi hawafati na walitaka kumuua daktari mwenzako na huenda akafia ICU

Wewe daktari unalipizaje?
Kumbuka Kisasi ni haq
 
Japo siungi mkono kujichukulia sheria mkononi, ila Wakatk miwngine madakitari au Raia tambua ni kosa kubwa sana kumpiga Askari/Mtumishi akiwa na Uniform au Eneo la kazi

Ngoja wampapase atarudi tu hapo Mloganzila
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…