Polisi wamenitrack niliokota simu, kesho natakiwa kituoni

Polisi wamenitrack niliokota simu, kesho natakiwa kituoni

Siku yakikukuta Usisahau hili
Matatizo Huja tu kwanjia Nyingi
Mwaka 2000 nilienda Mahakamani Kisutu kumkatia mtu dhamana. Wakati tunasubiri kuingia nikaona niingie ktk session moja ya open court. Kesi niliyokuta pale ilikuwa siku ya hukumu. Jamaa alikuwa ameshtakiwa kukutwa na mali ya wizi, na kwenye hukumu Hakimu alise.a kununua mali ya wizi pia ni ushiriki wa tendo la wizi. Mvua ikashushwa kwake miaka 3 jela baada ya kupunguzwa kutoka miaka 5.

Tokea siku hiyo, huniuzii mali mkononi nikanunua.....
 
Duh 2000.

Heshima yako mkuu
 
Imeandikwa
" Ukiona choo ndotoni usikitumie, ni mtego"

Sasa ndugu yangu upo ugenini na uliamua kukitumia kwa haja kubwa na ndo kumekucha sasa.
 
Msaada wa kisheria simu ya kuokota nakamatwa na polisi. Mama yangu aliokota simu smat phone akanipa sababu yeye Hawezi tumia nikaweka laini hapa nimepagawa,

Hii imekaaje mbaya zaidi aliepoteza simu anadai kwao ilibiwa simu, TV nch 32, jiko la ges plate mbili.

Je, machomokaje katika hili tatizo?
Mkiona kimya mjue nawasiliana na polisi maana wanasumbua balaa
Tupa hiyo simu aokote boyaaa

Anyway we uliokotaje smartphone mkuu 👨‍🏫👨‍🏫
 
Hapo kwa kutumia DOCTRINE OF RECENT POSSESSION wewe ni mwizi na ndiye uliyeiba simu hiyo

Mara tuu, uokotapa kitu chochote ambacho sii Mali yako Moja kwa Moja nenda Kituo chochote Cha polisi kilichopo karibu yako na utaandika maelezo jinsi ulivyokiokota. Kitafunguliwa Taarifa kwenye kitabu kiitwacho LOSS AND FOUND PROPERTY REGISTER na utapewa kumbukumbu ya Taarifa hiyo kama unapopewa RB ya kesi

Pale ambapo mwenye Mali atapatikana na kutoa vielelezo vyote vya umiliki atakabidhiwa Mali yake na wewe utajulishwa

Pale ambapo kwa kipindi kirefu mwenye Mali hajaonekana ,itaandikiwa inventory na baada ya kutoka kwenye gazeti la serikali itauzwa kwa mnada.

Epuka msemo wa uongo wa kiswahili usemao CHAKUOKOTA SII CHA KUIBA.Hapa wahenga waliodanganywa umma na msemo huu upo kinyume na sheria na unahamasishi wizi utaishia jela, mbaya zaidi ukute simu hiyo kabla ya kuibiwa lilifanyika kosa la jinsi kubwa
Hata hao polisi kuwaachia mali ya kuota ni kosa,maana nao wataikota tuu.
 
Msaada wa kisheria simu ya kuokota nakamatwa na polisi. Mama yangu aliokota simu smat phone akanipa sababu yeye Hawezi tumia nikaweka laini hapa nimepagawa,

Hii imekaaje mbaya zaidi aliepoteza simu anadai kwao ilibiwa simu, TV nch 32, jiko la ges plate mbili.

Je, machomokaje katika hili tatizo?
Mkiona kimya mjue nawasiliana na polisi maana wanasumbua balaa
Rudisha na TV ya watu.
 
Pole sana mkuu kwa changamoto unayokabiliana nayo. Binafsi mimi nina ushauri tofauti kidogo na wanao kushauri uitupe hiyo simu ama uvunje line zako ili polisi wasikipate. Mimi nadhani kwakufanya hivyo utakuwa umewapa polisi nguvu ya kuamini wewe ndiye mwizi na umehisika moja kwa kwaja na upotevu wa hivyo vitu vingine, na wakitaka kukupata wanakupata tu.

Kwa kuzingatia hali ya polisi wetu hapa nchini, mara nyingi wanapokuwa na tuhuma kama hizi za mali inayodaiwa kuibiwa, inaweza kuleta usumbufu hata kama hukuhusika moja kwa moja.

Kisheria, unapokutwa na mali inayodaiwa kuwa ya wizi, unatakiwa kueleza namna ulivyoipata na kuthibitisha kuwa hukujua au hukupaswa kuwa na sababu ya kuamini kuwa iliibwa. Nadhani katika kesi yako, unahitaji kueleza kwa polisi kuwa mama yako aliokota simu hiyo na hakuwa na nia mbaya. Ni vyena pia mama yako awe tayari kueleza mazingira ya kuipata simu hiyo, hasa kama kweli aliikota.

Hata hivyo, kwa kuwa tunawafahamu maafisa wa vyombo vyetu vya usalama namna walivyo, kuna uwezekano wa kukumbana na shinikizo la kukiri kosa au kudaiwa rushwa ili suala likwame. Ni muhimu sana ujue haki zako na uwe na tahadhari katika mawasiliano na polisi. Usikubali kushinikizwa kukiri kosa au kutoa maelezo yanayoweza kukutia hatiani bila ya kushauriana na wakili.

Pia, kama una uwezo wa kumpata wakili mapema, itakuwa bora zaidi kwa sababu anaweza kukusaidia kujadiliana na polisi kwa niaba yako na kuhakikisha kuwa haki zako zinaheshimiwa. Kwa sasa, weka ushirikiano lakini pia zingatia haki zako kisheria. Usisaini maelezo yoyote bila kuyaelewa vizuri.​
 
Mim mwenyewe nasubiria mkeka utiki Kuna madogo mwezi wa 5 nilipishana nao nikiwa na pikipiki kufika mbele aangalia simu siioni kugeuza kuja wauliza wakana Mimi nikaona isiwe kesi nikasepa kufungua kesi itafutwe na waliizima hawajaiwasha mpk Leo ila najua ipo day mtu atajichanganya
Siku hizi zinauzwa kama spea kwa mafundi simu
 
Msaada wa kisheria simu ya kuokota nakamatwa na polisi. Mama yangu aliokota simu smat phone akanipa sababu yeye Hawezi tumia nikaweka laini hapa nimepagawa,

Hii imekaaje mbaya zaidi aliepoteza simu anadai kwao ilibiwa simu, TV nch 32, jiko la ges plate mbili.

Je, nachomokaje katika hili tatizo?
Mkiona kimya mjue nawasiliana na polisi maana wanasumbua balaa.

Naona kama hadithi ya kutunga.....
Umeokota simu, wamekutrack na kukutaka ufike kituo cha polisi (inamaana hujafika bado)
Umejuaje kuwa mwenye simu anadai kuibiwa vitu, tena uwe na orodha kabisa?
 
Zima simu potea. Waachane na wewe.
Usajili wa laini yake,ushajulikana, popote aendapo atakamatwa heri ajisalimishe anaweza eleza ukweli wote kwenye hukumu akafikiriwa,akikimbia ataonekana ye ndo mwizi,atalipa vyote na kifungo juu
 
Msaada wa kisheria simu ya kuokota nakamatwa na polisi. Mama yangu aliokota simu smat phone akanipa sababu yeye Hawezi tumia nikaweka laini hapa nimepagawa,

Hii imekaaje mbaya zaidi aliepoteza simu anadai kwao ilibiwa simu, TV nch 32, jiko la ges plate mbili.

Je, nachomokaje katika hili tatizo?
Mkiona kimya mjue nawasiliana na polisi maana wanasumbua balaa.
Pole
 
Back
Top Bottom