Polisi wamenitrack niliokota simu, kesho natakiwa kituoni

Msaada wa kisheria simu ya kuokota nakamatwa na polisi. Mama yangu aliokota simu smat phone akanipa sababu yeye Hawezi tumia nikaweka laini hapa nimepagawa,

Hii imekaaje mbaya zaidi aliepoteza simu anadai kwao ilibiwa simu, TV nch 32, jiko la ges plate mbili. Je machomokaje katika hili tatizo?
Mkiona kimya mjue nawasiliana na polisi maana wanasumbua balaa
Kisheria presumption ni kwamba wewe ndio mwizi itabidi uende kupangua kama wewe sio mwizi , na tahadhari kwa wote simu used ni kiti hatari unaweza kusota muda mrefu rumande hadi wajiridhishe kama sio wewe huko mahakamani, imagine hiyo simu mwenyewe angekuwa kauliwa wakati inaibwa? Si murder case hiyo
 
Kuokota simu sawa sawa na kuokota maiti.
Hapo ulipo ujue una kesi ya mauaji, mbaya zaidi polisi wanajua jina lako na unapoishi.
Ukipangua kesi ya mauaji utabaki na ya kuvunja nyumba na kuiba kutumia silaha.
Kwanza, hebu waonyeshe polisi silaha yako unapoihifadhi. Ole wako Kama umesahau ulipoificha, Kuna vitu watakutanyia mpaka ukumbuke.
Bye bye.
 
Huyo mamako alikudanganya. Alienda kudanga akahongwa hiyo simu na mwizi au jambazi, muulize vizuri.

Babako unamjuwa? Mnaishi nae?
Mzee mzima mshika dini huna Ustaarabu? Yanini kumtusi mama usiyemjua kuwa anadanga? Ndio ninyi mnataka kutufundisha dini za peponi wakati matendo yenu ni sifuri
 
Msaada wa kisheria simu ya kuokota nakamatwa na polisi. Mama yangu aliokota simu smat phone akanipa sababu yeye Hawezi tumia nikaweka laini hapa nimepagawa,

Hii imekaaje mbaya zaidi aliepoteza simu anadai kwao ilibiwa simu, TV nch 32, jiko la ges plate mbili.

Je, machomokaje katika hili tatizo?
Mkiona kimya mjue nawasiliana na polisi maana wanasumbua balaa
Simu hawaokoti mkuu.
 
Bichwa lako la habari, uliokota wewe, utumbo wako wa habari, aliokota mamako.

Unaelewa unavyojikaanga hapo?

Ama wewe mwizi au mamako mwizi au kahongwa na mwizi.

Hakuna zaidi.
 
Msaada wa kisheria simu ya kuokota nakamatwa na polisi. Mama yangu aliokota simu smat phone akanipa sababu yeye Hawezi tumia nikaweka laini hapa nimepagawa,

Hii imekaaje mbaya zaidi aliepoteza simu anadai kwao ilibiwa simu, TV nch 32, jiko la ges plate mbili.

Je, machomokaje katika hili tatizo?
Mkiona kimya mjue nawasiliana na polisi maana wanasumbua balaa
mimi juzi bodaboda kanipita vuuuu vumbi kama lote mara nikasikia tii kumbe ameangusha bahasha chap kwa haraka cheki ndani samaki watatu wakubwa home maharage kama yote , namwona jamaa anapunguza mwendo, niliingia chochi moja mitaa siifahamu, hadi home, chakuokota si cha kuiba.
 
Back
Top Bottom