Polisi wamkamata Joseph Sanura aka Ngosha, aliyekuwa mpenzi wa Penina wa Goba Centre

Polisi wamkamata Joseph Sanura aka Ngosha, aliyekuwa mpenzi wa Penina wa Goba Centre

vyanzo mbalimbali zinabainisha kuwa Joseph alikua anamuhisi mpenzi wake anachepuka, na inasemekana siku hiyo Penina hakurejea nyumbani hali iliyomlazimu mtuhumiwa kumfuata ofisini kwake na kumshambulia hadi kupelekea umauti.
Huyo ng'ombe mwitu kamuua mdada wa watu ofisini kwake. Yaani unahisi mke sijui mpenzi anakusaliti unatoka uko unaenda eneo lake la kazi na panga unamuua? Idiot
 
shida ni rasilimali muda na pesa alizotumia jamaa kwa huyo manzi plus ahadi kuwa yuko peke yake sasa ikatokea otherwise ndo butchering ilipotokea!
Rasilimali inatakiwa itumike kwenye familia sio Kwa Manzi. Tofautisheni familia na mchumba/Manzi. Alafu wanaume tujiandae kisaikolojia kuchapiwa kupo tu calm down
 
Nawaonea huruma sana hawa mabinti, watakufa sana. Wamedanganywa mapenzi ni pesa, ila wakipewa hizo pesa bado hawatulii.
Utawaua wewe? Matukio ya aina hii hutokea mara chache. By the way mimi ni mwanaume ila sisi wanaume nadhani ni viumbe wajinga sana. Kwa nini nasema hivi: Asilimia kubwa na wanaume wa Bongo tuna tabia ya kutongoza hovyo, yaani kila kinachopita mbele yako kikikuvutia ni lazima ujaribu. Sasa kwenye mazingira ya aina hii unategemeaje kama una mke au mpenzi na yeye asipate majaribu mengi? Yaani kadiri mwanaume unavyotumia mbinu kupata wanawake, ndiyo hivyo hivyo mwanamke wako anavyofanyiwa na watu wengine.
 
Rasilimali inatakiwa itumike kwenye familia sio Kwa Manzi. Tofautisheni familia na mchumba/Manzi. Alafu wanaume tujiandae kisaikolojia kuchapiwa kupo tu calm down
Mbona na mke wangu alizingua ivo ivo... ishu sio kuwekeza kwa nani, wanawake wakijijua hawampendi mtu wasitake pesa na jasho la mwanaume husika
 
Mwanamke umemkuta anauza bar umemtongoza amekubali ukamla halafu unajifanya umemzimikia sana yaani hata ujiulizi kabla yako wamemla watu wangapi kwa staili kama hiyo na ataendelea kuliwa kwa mtindo huo na watu wangapi! Matatizo mengine ni ya kujitakia tu.
 
nimesema hicho ni kichaka cha kweney gomvi nyingi zinazohusiana na mapenzi. nadra sana kupatikana na murder.
Inategemea na namna mauaji yalivyotokea na ushahidi. Kwa mfano, kama ngosha katoka nyumbani na panga kwenda ofisini kwa demu na kutekeleza mauaji, hiyo ni ushahidi kwamba mauaji yalikuwa "premeditated"........hayo ni mauaji ya kukusudia...........laa kama ingekua ni kughafilika kwa ghafla na akaokota panga lililokuepo eneo la tukio na kufanya mauaji, hapo kunaweza kuwa na utetezi wa kughafilika....hivyo kesi kuwa ni mauaji bila kukusudia.....
 
Ukiona mwanamke anauza bar au anawaza kufungua grocery ya pombe achana nae huyo ni malaya muuza ngunya na akili yake ndio imeishia hapo kwamba afungue kijiwe cha kuhalalisha kutumia nyapu apate kipato zaidi. Huyo mkimbie fasta hata kama ni mrembo kiasi gani.
 
Inategemea na namna mauaji yalivyotokea na ushahidi. Kwa mfano, kama ngosha katoka nyumbani na panga kwenda ofisini kwa demu na kutekeleza mauaji, hiyo ni ushahidi kwamba mauaji yalikuwa "premeditated"........hayo ni mauaji ya kukusudia...........laa kama ingekua ni kughafilika kwa ghafla na akaokota panga lililokuepo eneo la tukio na kufanya mauaji, hapo kunaweza kuwa na utetezi wa kughafilika....hivyo kesi kuwa ni mauaji bila kukusudia.....
kuna mambo mengi kwenye hilo, sio provocation pekee, hata death resulting from a fight, na mengine kibao. nilichosema, kesi nyingi sana za ugomvi huishia manslaughter though kila kesi inatofautiana kulingana na facts zake. zipo pia zinazodondokea kwenye pure murder but majority of this kind huishia manslaughter. mauaji yeyote yenye pre-meditated malice aforethought, ni kunyongwa hadi kufa. na kweli kama hapa alijiandaa na panga akaenda nalo pale, hawezi kuplead provocation wala death resulting from a fight, wala self-defence, kwasababu hatujui facts za kesi, tulichosikia ni kwamba jamaa kamuulia palepale, kama kwenye grocery kulikuwa na panga au la, au alitoka nalo home hatujui. tusubiri tupate facts.
 
Utawaua wewe? Matukio ya aina hii hutokea mara chache. By the way mimi ni mwanaume ila sisi wanaume nadhani ni viumbe wajinga sana. Kwa nini nasema hivi: Asilimia kubwa na wanaume wa Bongo tuna tabia ya kutongoza hovyo, yaani kila kinachopita mbele yako kikikuvutia ni lazima ujaribu. Sasa kwenye mazingira ya aina hii unategemeaje kama una mke au mpenzi na yeye asipate majaribu mengi? Yaani kadiri mwanaume unavyotumia mbinu kupata wanawake, ndiyo hivyo hivyo mwanamke wako anavyofanyiwa na watu wengine.
Yanatokea mara chache? We unaishi wapi kwanza, nisijekuwa naongea na mtu yuko Jupiter haelewi yanayoendelea hapa duniani.
 
Girls before muingie kwenye relationship hakikisha mpenzi wako akili yake Ina afya
Usidharau red flag yoyote
Kauli kama nitakuua,nitakupasua,nitakumaliza ni mojawapo ya red flags usipuuze

R.I.P Penina
Pia, girls, kama mwanaume humwelewi, usijifanye kumpenda na kupokea chochote anachokupatia, iwe hela au vitu.

Kupokea vitu toka kwake huku humwelewi ni kujiweka katika mazingira hatarishi.
 
Mbona na mke wangu alizingua ivo ivo... ishu sio kuwekeza kwa nani, wanawake wakijijua hawampendi mtu wasitake pesa na jasho la mwanaume husika
Ni sahihi unachosema na najua kunazile hasira za ghafla lamda umemzaba Kofi au ngumi kadondoka kafa. Hapo ningejua ni hasira za ghafla, lakini unachukua panga mpaka unafunga safari bado tu huwaji kupoteza uhuru maishani mwako mwote inaishia jela na warembo zaidi ya huyo penina wapo wengi tu
 
Back
Top Bottom