Polisi wamkamata Joseph Sanura aka Ngosha, aliyekuwa mpenzi wa Penina wa Goba Centre

Polisi wamkamata Joseph Sanura aka Ngosha, aliyekuwa mpenzi wa Penina wa Goba Centre

Jurisprudence imekuwa usikariri kuna baadhi ya binadamu huweza kuishi ndani ya provocation attitude hata masaa mawili. Ni swala la ushahidi tu hapo
jurisprudence ya wapi hiyo? ya hapa kwetu au ya kuazima of which we are not bound with.
 
"Legend wa Mahaba" amemaliza mwendo KIFALA sana...

Kwenye 20's na 30's wengi wetu tunaendeshwa na mapenzi na hisia,, LIFE STARTS at 40.
 
imagine, unaanza kumkatakata mapanga mtoto wa watu, as if ni mali yako binafsi, ana wazazi, ana watoto, ana ndugu. hivi who are you kufikiri unammiliki mwanadamu?
....Simuungi mkono ngosha kwa kuua ila dada kama hutaki kumilikiwa kwa nini ulinikubalia?
 
Pia, girls, kama mwanaume humwelewi, usijifanye kumpenda na kupokea chochote anachokupatia, iwe hela au vitu.

Kupokea vitu toka kwake huku humwelewi ni kujiweka katika mazingira hatarishi.
Watakuja kukuambia nawanukuu 👇🏻

"Kwani si anatoa mwenyewe hajalazimishwa"

Hizi ndo akili za dada zetu wengi 👆🏻
 
Binadamu hawa ambao bado ni viwavi kuelekea utu ukiwaondolea adhabu ya kifo au/na diyar itafikia sehem kila kaya ina aliyeuawa!
Mjadala wa kufuta adhabu ya kifo urudishwe mezani!
Pia iundwe kamati ya nidham ngazi ya kitongoji yenye wazee wenye hekma na uadilifu ambayo itajishughulisha pia na mambo ambayo mahakama haiwezi ku capture moja kwa moja.
mf mashitaka ya kimapenzi na shambulio za kimaadili na saikolojia!
 
Inasikitisha,

images.jpg
 
Ngosha atakuwa ameshazoea maisha ya jela
Mkazi wa Goba Lastanza Kinondoni, Joseph Sanura maarufu kama Ngosha (31), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam. kwa tuhuma za mauaji ya Penina Rwegoshora (28) mkazi wa Goba center.

Taarifa ya Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, SACP. Muliro Jumanne imeeleza kuwa tukio hilo limetokea Mei 23, 2024 majira ya 07:00 huko maeneo ya Goba Center, Kinondoni katika Pub ya iitwayo Penina.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, uchunguzi wa awali wa Polisi unaonesha kulikuwa na mgogoro wa kimahusiano kati ya mtuhumiwa na marehemu kabla ya kushambuliwa kwa panga na mtuhumiwa.

Aidha, taarifa ambazo Dar24 Media imezipata kwa vyanzo mbalimbali zinabainisha kuwa Joseph alikua anamuhisi mpenzi wake anachepuka, na inasemekana siku hiyo Penina hakurejea nyumbani hali iliyomlazimu mtuhumiwa kumfuata ofisini kwake na kumshambulia hadi kupelekea umauti.

Inaarifiwa kuwa pia Penina ameacha watoto wawili na mwili wake unazikwa hii leo Mei 24, 2024 jioni huko Goba huku Polisi ikisema upelelezi unakamilishwa, ili mtuhumiwa afikishwe Mahakamani haraka iwezekanavyo.

Pia soma: Penina wa Goba Centre auawa na aliyekuwa mpenzi wake kwa kukatwa mapanga
View attachment 2998445
 
Back
Top Bottom