Polisi wamkamata Joseph Sanura aka Ngosha, aliyekuwa mpenzi wa Penina wa Goba Centre

Polisi wamkamata Joseph Sanura aka Ngosha, aliyekuwa mpenzi wa Penina wa Goba Centre

Mkazi wa Goba Lastanza Kinondoni, Joseph Sanura maarufu kama Ngosha (31), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam. kwa tuhuma za mauaji ya Penina Rwegoshora (28) mkazi wa Goba center.

Taarifa ya Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, SACP. Muliro Jumanne imeeleza kuwa tukio hilo limetokea Mei 23, 2024 majira ya 07:00 huko maeneo ya Goba Center, Kinondoni katika Pub ya iitwayo Penina.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, uchunguzi wa awali wa Polisi unaonesha kulikuwa na mgogoro wa kimahusiano kati ya mtuhumiwa na marehemu kabla ya kushambuliwa kwa panga na mtuhumiwa.

Aidha, taarifa ambazo Dar24 Media imezipata kwa vyanzo mbalimbali zinabainisha kuwa Joseph alikua anamuhisi mpenzi wake anachepuka, na inasemekana siku hiyo Penina hakurejea nyumbani hali iliyomlazimu mtuhumiwa kumfuata ofisini kwake na kumshambulia hadi kupelekea umauti.

Inaarifiwa kuwa pia Penina ameacha watoto wawili na mwili wake unazikwa hii leo Mei 24, 2024 jioni huko Goba huku Polisi ikisema upelelezi unakamilishwa, ili mtuhumiwa afikishwe Mahakamani haraka iwezekanavyo.

Pia soma: Penina wa Goba Centre auawa na aliyekuwa mpenzi wake kwa kukatwa mapanga
Huwa najiuliza hivi inakuwaje unajimilikisha mwanamke wakati hujamuoa na unakuwa na wivu kabisa
 
imagine, unaanza kumkatakata mapanga mtoto wa watu, as if ni mali yako binafsi, ana wazazi, ana watoto, ana ndugu. hivi who are you kufikiri unammiliki mwanadamu?
unachosahau ni kwamba ingawa sote ni watanzania lakin tunatofautiana hatua ya evolution tuliyofikia!
Penina alitakiwa kulielewa hili kabla haja date Ngosha OG!
Tangu nijionee wasukuma hawajavuka hata mstari wa kutofautisha chupi za kike na kiume nikajua bado sana! (mwanaume utavaaje chupi ya lesi lesi!!!)
Sishabikii ukabila lakin si vibaya kujua uliyempata wako hatua ipi kuhusu mapenzi, mwanamke, mtoto, dini, mila na desturi.
 
ukute huyo ngosha ndo alikua mchepukaji mkuu tena wa hivyo huwa wana wivu balaa kumbe wao huko nje ndo wamezidi.

Mimi nawahakikishia mara nyingi ukiskia mwanamke ame cheat ni either mwanaume wake amemcheat sana na analipiza kisasi au mwanaume hana muda nae. Bishaneni na ukweli
 
Nashauri watanzania turudi kwenye scoreboard tuache uzinzi/uasherati na tuwe waaminifu kwa wengine. Haya mambo ya mauaji ni matokeo tu. Asante
 
kuna mambo mengi kwenye hilo, sio provocation pekee, hata death resulting from a fight, na mengine kibao. nilichosema, kesi nyingi sana za ugomvi huishia manslaughter though kila kesi inatofautiana kulingana na facts zake. zipo pia zinazodondokea kwenye pure murder but majority of this kind huishia manslaughter. mauaji yeyote yenye pre-meditated malice aforethought, ni kunyongwa hadi kufa. na kweli kama hapa alijiandaa na panga akaenda nalo pale, hawezi kuplead provocation wala death resulting from a fight, wala self-defence, kwasababu hatujui facts za kesi, tulichosikia ni kwamba jamaa kamuulia palepale, kama kwenye grocery kulikuwa na panga au la, au alitoka nalo home hatujui. tusubiri tupate facts.
Hakuna mtu anapenda kwenda jela. Kwenye utetezi mtu husema chochote ili ajinusuru na ngome. Unaweza kuta Ngosha akasema alibeba panga akiwa anaenda kwenye shughuli zake za ujenzi, panga likiwa ni kifaa cha ujenzi huko site aendako, akapitia kumsalimia Penina na wakiwa hapo wakagombana na akajikuta amemkata na panga mara kadhaa akiwa katika temporary insane mind.

Kwamba wakati akienda lengo lilikuwa ni kusabahi tu.

Ila ngoja tusubiri facts wakati wa kesi. Unaweza kuta baada ya demu kutopatikana na kutopokea simu, jamaa alituma text kibao za vitisho, hivyo kumfanya awe alijiandaa kabisa kutekeleza kilichotokea.
 
Girls before muingie kwenye relationship hakikisha mpenzi wako akili yake Ina afya
Usidharau red flag yoyote
Kauli kama nitakuua,nitakupasua,nitakumaliza ni mojawapo ya red flags usipuuze

R.I.P Penina
siku hizi tumeacha kusingizia shetani twasingizia afya ya akili,
jambo ambalo ungetakiwa kuwashauri ndugu zako ni kuwa waaminifu na wakweli kwenye mahusiano basi,
hata mwenye afya ya akili ukimkatili anakukatili vizuri tu hata kama hajawahi kukupa kauli za vitisho
 
aisee hawa watani zangu waporipori kwelikweli,mwanamke alishakuwa na mahusiano kabao, muuza pombe, ana watoto na wanaume wengine, anakatakata hivyo, angekuwa alimkuta bikra si angewehuka kabisa? au angefyeka mtaa mzima kama nyegere?
Na hapo usikute jamaa ana mkono wa sweta na akavumiliwa
 
Kumtoa roho mtu kwa mtu kwa ajili ya mapenzi kwangu mimi ni ujuha tu, maana sasa hapo Ngosha anaanza sumbuka na polisi, mahakama, kote huko atahongoa, bado ataweka advocate hela napo itamtoka, haya marehemu kaacha watoto so Ngosha anaonekana muuaji kwenye macho ya hao watoto.

Kama mtu kaamua kuutumia mwili wake kwa mtu mwingine ni bora kuachana tu mbona Ke/Me wapo wengi mpaka wamepitiliza!!
Hizo ni busara zako mkuu ukiwa Bado hujapanic Wala hujakutana na changamoto yeyote inayohusu penzi unakuta mtu kawekeza gharama kubwa halaf muda unakuta huelewi unaona mapichapicha tu Hadi busara zije kichwani mwako Kwa sisi watu wa kanda ya ziwa ulishauwa jitu vita ni vita mura
 
siku hizi tumeacha kusingizia shetani twasingizia afya ya akili,
jambo ambalo ungetakiwa kuwashauri ndugu zako ni kuwa waaminifu na wakweli kwenye mahusiano basi,
hata mwenye afya ya akili ukimkatili anakukatili vizuri tu hata kama hajawahi kukupa kauli za vitisho
This applies to both....hata wanaume wanatakiwa kuwa waaminifu
Kwa sababu wapo wanawake wenye shida ya afya ya akili
 
Hakuna mtu anapenda kwenda jela. Kwenye utetezi mtu husema chochote ili ajinusuru na ngome. Unaweza kuta Ngosha akasema alibeba panga akiwa anaenda kwenye shughuli zake za ujenzi, panga likiwa ni kifaa cha ujenzi huko site aendako, akapitia kumsalimia Penina na wakiwa hapo wakagombana na akajikuta amemkata na panga mara kadhaa akiwa katika temporary insane mind.

Kwamba wakati akienda lengo lilikuwa ni kusabahi tu.

Ila ngoja tusubiri facts wakati wa kesi. Unaweza kuta baada ya demu kutopatikana na kutopokea simu, jamaa alituma text kibao za vitisho, hivyo kumfanya awe alijiandaa kabisa kutekeleza kilichotokea.
Mkuu inabidi uwe mwanasheria wangu, haha
 
Girls before muingie kwenye relationship hakikisha mpenzi wako akili yake Ina afya
Usidharau red flag yoyote
Kauli kama nitakuua,nitakupasua,nitakumaliza ni mojawapo ya red flags usipuuze

R.I.P Penina
Red flag kubwa zaidi.
Ni wewe kutozingatia hisia za mwenzako licha ya uwekezaji anaoweka kwako.
 
Hizo ni busara zako mkuu ukiwa Bado hujapanic Wala hujakutana na changamoto yeyote inayohusu penzi unakuta mtu kawekeza gharama kubwa halaf muda unakuta huelewi unaona mapichapicha tu Hadi busara zije kichwani mwako Kwa sisi watu wa kanda ya ziwa ulishauwa jitu vita ni vita mura
Na wengi humu utakuta walishawapiga wapenzi wao huko kwa visa vya kitoto kabisa.
 
imagine, unaanza kumkatakata mapanga mtoto wa watu, as if ni mali yako binafsi, ana wazazi, ana watoto, ana ndugu. hivi who are you kufikiri unammiliki mwanadamu?
Anzia Hapo Hapo bro!; Huku utafakari MSUKUMO ULIOMSUKUMA KUFIKIA MAAMUZI HAYO!
Kuna Mtu Alitamka kwamba ANASIKITIKA KUKAMATWA LAKINI HASIKITIKI KUUA.
RIP Penina!
 
kuna mambo mengi kwenye hilo, sio provocation pekee, hata death resulting from a fight, na mengine kibao. nilichosema, kesi nyingi sana za ugomvi huishia manslaughter though kila kesi inatofautiana kulingana na facts zake. zipo pia zinazodondokea kwenye pure murder but majority of this kind huishia manslaughter. mauaji yeyote yenye pre-meditated malice aforethought, ni kunyongwa hadi kufa. na kweli kama hapa alijiandaa na panga akaenda nalo pale, hawezi kuplead provocation wala death resulting from a fight, wala self-defence, kwasababu hatujui facts za kesi, tulichosikia ni kwamba jamaa kamuulia palepale, kama kwenye grocery kulikuwa na panga au la, au alitoka nalo home hatujui. tusubiri tupate facts.
Jurisprudence imekuwa usikariri kuna baadhi ya binadamu huweza kuishi ndani ya provocation attitude hata masaa mawili. Ni swala la ushahidi tu hapo
 
watani zangu kina ngosha wanakuwaga waporipori kweli, sijuiw ataacha lini ushamba.
Ngosha na mwanamke mweupe utamwambia nini akuelewe?

Wakija JF wanawaponda single mother kumbe wanakufa juu yao, demu Penina ana watoto wawili.
 
Back
Top Bottom