Polisi wampe ulinzi mke wa Dr. Mwaka. Sakata la ndoa yao lina vita ya kiuchumi ambayo inaweza kupelekea mauaji

Polisi wampe ulinzi mke wa Dr. Mwaka. Sakata la ndoa yao lina vita ya kiuchumi ambayo inaweza kupelekea mauaji

Kwasababu ambazo zisizoweza kuvumilika! Na kwa hali ilivyo akibakia ndani ya ndoa ni rahisi sana kuumizwa! Hawataaminiana!
Mbona huwa nasikia mwanamke kama anaruka ruka mfano wa maharage ya mbeya, huwa anatulizwa kwa ukuni na hongo tu?

Dr Mwaka kashindwa vipi kushawishi kumlala mke wake na vijizawadi vya kuzugia ili yaishe?

Mtu una hela unawezaje kukimbiwa na mwanamke bhana?

Maana katika statements za mwanamke kuna sehemu anasema alipopigiwa simu kwenda kwa kadhi, alitegemea itakuwa ni kikao cha usuluhisho ambao Mwaka aliutaka!

Baadaye ndiyo akageuziwa kibao na kuswendekwa ndani.

Kama ningelikuwa ndiye mimi, ningelichuna ngozi na jiko nikarudisha ndani na issue ikaishia hapo simple like that!

Huyu dr huyu, anataka kutuangusha sasa sisi wanaume wapenda wanawakel!
 
Mzee Lowassa aliwahi kusema Elimu, Elimu, Elimu!! Mzee Mwaka shule ndogo, yule janja janja nyingi hadi watu wanaamini ana degree sijui ya India. Hapo kaachwa haachike tu, mali kitu gani wakati huyo Queen ana watoto nae wawili ambao ndio halali yao hio. Kama anapata hio pesa yote kwenye biashara zake nyumba kujenga ingine anaweza pia.haya ma ndoa ya wake wengi ya matangazo ndio mwisho wake uwa hivi, Haji Manara analijua hili amebaki kulia lia tu watu washamdaka mkewe.
 
Sitapenda kuchimba sana kwenye mgogoro wa ndoa

Lakini naomba kusema machache kwenye sura ya usalama wa kila mmoja kwenye mgogoro huo!

Ukitazama kwa juu juu unaweza kushangaa kwanini mambo yao ya ndoani yameifikia jamii.

Lakini ukitafakali sana unagundua sakata lao ni sawa na moto, ulianza kama moto mdogo ndani ya nyumba yao lakini ulishindikana kuzimwa kwa faya extuingusher, hivyo moto umekuwa mkubwa moshi umetanda kiasi cha kuhitaji msaada wa jamii na zimamoto!

Hivyo serikali ikichelewa kutoa msaada wa haraka itakuwa kama zimamoto iliyochelewa! Hakutakuwa na kuokoa kila kitu kitapukutika!

VITA YA KIUCHUMI NI MBAYA SANA
Queen (mke wa Dr Mwaka) anaonekana kuhitaji taratibu zote za haki zifuatwe katika sakata lao la ndoa! Lakini anayokutana nayo kwenye kesi yake huenda kama siyo Rushwa basi yanavurugwa na mfumo dume!

Kwa maelezo yake mwenyewe anakutana na majibu ya jeuri, vitisho katika mamlaka yake ya haki ya ndoa! (Swali kwanini wamtishe? Kwa nini wamjibu jeuri mteja katika shauri la haki?

utakubaliana na mimi kwamba Kama siyo rushwa basi ni mfumo dume!
Ambapo kama Tabia hii haijakomeshwa iko siku taifa litaingizwa kwenye migogoro ya kijinsia! (Tusifike huko)

KWANINI HAYO YOTE?
Kwa taswira ya mmoja mmoja hakuna anayemhitaji mwenzake kindoa! Lakini kwasababu za kiuchumi ndicho kinacholeta marumbano hayo!.

TUKIANZA NA DR. MWAKA!

Huyu MWAKA ni mfanyabiashara, kazi yake kubwa inayompa wateja wengi ni kusuluhisha migogoro ya ndoa na tiba kwenye masuala ya uzazi (ndoa)!.

faida ya kazi hii ndiyo inayomlisha, ndiyo iliyompatia wake zake wengine!

Kwa mfano!
Endapo Ahadi ya wateja wa Dr. MWAKA kumuona kwa ajili ya ushauri wa kindoa walilipia (laki tatu ~Hadi tano) inamaana kwa siku anaweza kuwa anaingiza zaidi ya (2mil hadi 5mil) bila shaka itakuwa ni pesa nyingi kwa mwezi na mwaka!

Ukiachilia mbali ushauri, Imani ya mauzo ya dawa zake kutibu ndoa za wengine ni kubwa!

Hivyo ukijumlisha tiba na mauzo ya dawa utaona ni pesa nyingi kiasi gani
.
kwa lugha rahisi ni kwamba kumuua Dr. Mwaka kibiashara ni KUONDOA IMANI KWA WATEJA!

Hivyo kwa gharama yoyote iwe mvua iwe jua TALAKA YA NDOA HII Haiwezi kuwa rahisi kama wengi walivyotarajia!.

Kumpoteza mke wake kwa talaka ni shambulio kubwa sana la kibiashara linaliweka lehani mapato hata kuhatalisha ndoa zake zingine!

Swali ni je hayo yote hakuyajua mapema?

majibu ni mepesi tu "Kiburi cha pesa, Dharau na mfumo dume"
hivyo ndivyo vinavyoweza kuwa vimechangia!

Sakata hili ni sawa na bundi kuhamia kwa mganga! Analia usiku kucha, na mganga badala ya kupiga manyanga anatoa anatishia kumpiga bundi na bastola ili kumnyamazisha wateja wasimkimbie!

Katika vita hii Dr mwaka anaweza kufanya tukio baya sana ili kulinda biashara yake na wake zake!

Usalama wa Queen upo mashakani kama polisi hawatampa ulinzi kuanzia sasa!

Mambo yao ya kisheria na haki yatizamwe haraka kwa usalama wao!

Mgogoro wa nyumba ni sehemu ndogo sana wa maslahi ya Dr.mwaka!
Maslahi makubwa ya anayolinda ni biashara yake na wake zake wanaobaki!

Ikumbukwe pia mwaka anamikopo benki ambayo marejesho yanategemea biashara hiyo!

Hivyo uwezekano wa mwaka kufanya ukatili ili kuifumba jamii ni mkubwa mno endapo shauri lao kama halitasikilizwa mapema! Na itangazwe wazi!
Acha urongo hv unajua stahiki za mwanamke wa kiislam pindi ndoa inapovunjika!!??
 
Mzee Lowassa aliwahi kusema Elimu, Elimu, Elimu!! Mzee Mwaka shule ndogo, yule janja janja nyingi hadi watu wanaamini ana degree sijui ya India. Hapo kaachwa haachike tu, mali kitu gani wakati huyo Queen ana watoto nae wawili ambao ndio halali yao hio. Kama anapata hio pesa yote kwenye biashara zake nyumba kujenga ingine anaweza pia.haya ma ndoa ya wake wengi ya matangazo ndio mwisho wake uwa hivi, Haji Manara analijua hili amebaki kulia lia tu watu washamdaka mkewe.
Uchawi mwingi
 
Unafanishaje mfumo dume na mambo ya kipuuzi?! Ni wapi ulisoma au ulifundishwa kuwa mfumo dume ulimuelekeza dokta mwaka kugombana na mkewe na kuleteana nae hizo kash kash.
 
ningekuwa ni mimi mahakama wewe ungekuwa namba moja kuleta usaidizi wa maelezo maana inaonekana unaijua sana ndoa ya yule bwana kuliko hata yeye binafsi pengine. Upande mwingine mimi kama mwanaume siwaamini wanawake hata wawe wanaeleza huku wanalia...hao ni wahuni sana si lahisi kuwaamini....Mwaka afanye analoliamini tu...wala asifanye kwa kumhurumia mtu, atende haki tu...na talaka asitoe, itakuwa fundisho kwa wachache wenye tabia kama za yule mkewe
 
Hujielewi labda uwe hakimu kwenye mahakama ya ndizi
 
Back
Top Bottom