Polisi wampe ulinzi mke wa Dr. Mwaka. Sakata la ndoa yao lina vita ya kiuchumi ambayo inaweza kupelekea mauaji

Polisi wampe ulinzi mke wa Dr. Mwaka. Sakata la ndoa yao lina vita ya kiuchumi ambayo inaweza kupelekea mauaji

Kwa mjibu wa ndoa ya kiisilamu mwanamke anaweza kutoa talaka shida ya huyu mwanamke anataka kupewa talaka ili adai Mali kama kweli sio kivuruge atoe talaka yeye mwanamke

Sent by Iphone 14 pro
 
Huyo Mwaka kazingua sana..yule mama kwa maelezo ya jana...anahitaji kusepa tu..lkn pia kwa ajili alivyokua anaongea..yuko tayari kutulia kama atabembelezwa...shida huyo Mwaka ni kama hajui anataka nini, anampiga pini kila idara bila direction yoyote
Kama anataka atoe talaka yy mwanamke

Sent by Iphone 14 pro
 
Mwaka naye ni mjinga ,amechuma mali kibao yaani anang'ang'ania nyumba na range tu? Ebu muachie mpe na talaka aende zake,hizo mali ni za watoto wako na si za mke.
 
Sitapenda kuchimba sana kwenye mgogoro wa ndoa

Lakini naomba kusema machache kwenye sura ya usalama wa kila mmoja kwenye mgogoro huo!

Ukitazama kwa juu juu unaweza kushangaa kwanini mambo yao ya ndoani yameifikia jamii.

Lakini ukitafakali sana unagundua sakata lao ni sawa na moto, ulianza kama moto mdogo ndani ya nyumba yao lakini ulishindikana kuzimwa kwa faya extuingusher, hivyo moto umekuwa mkubwa moshi umetanda kiasi cha kuhitaji msaada wa jamii na zimamoto!

Hivyo serikali ikichelewa kutoa msaada wa haraka itakuwa kama zimamoto iliyochelewa! Hakutakuwa na kuokoa kila kitu kitapukutika!

VITA YA KIUCHUMI NI MBAYA SANA
Queen (mke wa Dr Mwaka) anaonekana kuhitaji taratibu zote za haki zifuatwe katika sakata lao la ndoa! Lakini anayokutana nayo kwenye kesi yake huenda kama siyo Rushwa basi yanavurugwa na mfumo dume!

Kwa maelezo yake mwenyewe anakutana na majibu ya jeuri, vitisho katika mamlaka yake ya haki ya ndoa! (Swali kwanini wamtishe? Kwa nini wamjibu jeuri mteja katika shauri la haki?

utakubaliana na mimi kwamba Kama siyo rushwa basi ni mfumo dume!
Ambapo kama Tabia hii haijakomeshwa iko siku taifa litaingizwa kwenye migogoro ya kijinsia! (Tusifike huko)

KWANINI HAYO YOTE?
Kwa taswira ya mmoja mmoja hakuna anayemhitaji mwenzake kindoa! Lakini kwasababu za kiuchumi ndicho kinacholeta marumbano hayo!.

TUKIANZA NA DR. MWAKA!

Huyu MWAKA ni mfanyabiashara, kazi yake kubwa inayompa wateja wengi ni kusuluhisha migogoro ya ndoa na tiba kwenye masuala ya uzazi (ndoa)!.

faida ya kazi hii ndiyo inayomlisha, ndiyo iliyompatia wake zake wengine!

Kwa mfano!
Endapo Ahadi ya wateja wa Dr. MWAKA kumuona kwa ajili ya ushauri wa kindoa walilipia (laki tatu ~Hadi tano) inamaana kwa siku anaweza kuwa anaingiza zaidi ya (2mil hadi 5mil) bila shaka itakuwa ni pesa nyingi kwa mwezi na mwaka!

Ukiachilia mbali kazi ya ushauri, Imani ya mauzo ya dawa zake kutibu ndoa za wengine ni kubwa!

Hivyo ukijumlisha tiba na mauzo ya dawa utaona ni pesa nyingi kiasi gani
.
kwa lugha rahisi ni kwamba kumuua Dr. Mwaka kibiashara ni KUONDOA IMANI KWA WATEJA!

Hivyo kwa gharama yoyote iwe mvua iwe jua TALAKA YA NDOA HII Haiwezi kuwa rahisi kama wengi walivyotarajia!.

Kumpoteza mke wake kwa talaka ni shambulio kubwa sana la kibiashara ya mwaka pamoja na mapato pia inahatalisha ndoa zake zingine!

Swali ni je hayo yote dr. Mwaka hakuyajua mapema?

majibu ni mepesi tu "Kiburi cha pesa, Dharau na mfumo dume"
hivyo ndivyo vinavyoweza kuwa vimechangia!

Sakata hili ni sawa na bundi kuhamia kwa mganga! Analia usiku kucha, na mganga badala ya kupiga manyanga kwa tiba badala yake anatoa silaha kumpiga bundi ili kumnyamazisha kufumba wateja wake wasimkimbie!

Katika vita hii Dr mwaka anaweza kufanya tukio baya sana ili kulinda biashara yake na wake zake!

Usalama wa Queen upo mashakani kama polisi hawatampa ulinzi kuanzia sasa!

Mambo yao ya kisheria na haki yatizamwe haraka kwa usalama wao!

Mgogoro wa nyumba ni sehemu ndogo sana wa maslahi ya Dr.mwaka!

Maslahi makubwa ya anayolinda Mwaka ni biashara yake na wake zake wanaobaki wasimkimbie!

Ikumbukwe pia mwaka anamikopo benki ambayo marejesho yanategemea biashara hiyo!

Updates
TUME YA HAKI ZA BINADAM ikiongozwa na kamishina wamefika kwa mke wa mwaka ili kuona namna ya usalama wa mwanamke umeguswa! Na wamebaini kuna HOJA ya msingi ambayo inahitaji msaada!

Hivyo uwezekano wa mwaka kufanya ukatili ili kuifumba jamii ni mkubwa mno endapo shauri lao kama halitasikilizwa mapema! Na itangazwe wazi!
Hizo ni hisia zako tu, Mwaka anataka taratibu zifuatwe kwenye utoaji talaka ya kidini. Sheria ya dini inamruhusu mke kurudisha mahali na kuomba talaka, kwanini huyo mwanamke hafanyi hivyo?
Kelele za yule mwanamke ni kutaka jamii imuonee huruma kuwa anaonewa, ikiwa huyo mwanamke ni jirani yako ama mnajuana mwambie aache magumashi afuate taratibu
Pia biashara ya mwaka haiwezi kufa kama wateja wake ni hawa watanzania ninaowajua mimi.
 
Huyo Mwaka kazingua sana..yule mama kwa maelezo ya jana...anahitaji kusepa tu..lkn pia kwa ajili alivyokua anaongea..yuko tayari kutulia kama atabembelezwa...shida huyo Mwaka ni kama hajui anataka nini, anampiga pini kila idara bila direction yoyote
Usimuamini mwanamke kwa maelezo tu.
 
Kwanini hili limekuwa swala la jamii nzima?

Huyo mwanamke ana umuhimu gani kwenye hili taifa?

Akwende huko!
Ni muhimu sana huyo anawakilisha wanawake wengi ambao hawajapata watu wa kuwasemea kuhusu haki zao pale ndoa inapofika kikomo, na kupitia kwake wengi wetu tumejua udhaifu wa hizi taasisi za kidini zilizopewa mamlaka ya kutatua changamoto hizi.
 
Hizo ni hisia zako tu, Mwaka anataka taratibu zifuatwe kwenye utoaji talaka ya kidini. Sheria ya dini inamruhusu mke kurudisha mahali na kuomba talaka, kwanini huyo mwanamke hafanyi hivyo?
Kelele za yule mwanamke ni kutaka jamii imuonee huruma kuwa anaonewa, ikiwa huyo mwanamke ni jirani yako ama mnajuana mwambie aache magumashi afuate taratibu
Pia biashara ya mwaka haiwezi kufa kama wateja wake ni hawa watanzania ninaowajua mimi.
Tashwishwi kwelikweli hivi Mwaka ni kabila gani?
 
Back
Top Bottom