Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

Naomba kufahamishwa unaweza kumchukua mtu vipimo bila hati ya mahakama?

Je polisi ana mamlaka ya kufanya vipimo bila ya mahakama? Je matokeo hayo yanaweza kuwa sehemu ya ushahidi?
 
View attachment 547452
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema baada ya Tundu Lissu kutolewa ha Polisi cha Kati leo mchana, amefikishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo.

Mapema asubuhi, mawakili akiwamo Fatma Karume walizuiliwa kuonana naye huku Jeshi la Polisi likisema litaendelea kumshikilia hadi uchunguzi utakapokamilika.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kilichoanza jana.

"Kabla ya kuelekea nyumbani kwake Tegeta, wamempeleka kwa mkemia mkuu na ameshapimwa mkojo, sasa sijui ni kitu gani wanachunguza, kwa sasa wameshaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kumpekua,"amesema Mrema.

Licha ya kulala rumande hakuna aliyeruhusiwa kuingia na kumuona Tundu Lissu wakiwamo wanasheria wake. Mbali na Fatma, wengine waliokuwapo ni Peter Kibatala na Frederick Kihwelo.

====

UPDATE 1

Mapema kabla, Lissu alipitishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali,alikataa kupimwa mkojo kwa sababu kipimo hicho hakihusiani na tuhuma za uchochezi.

More to follow

Mkojo???? Uchochezi na mkojo OK,uchochezi na kupekuliwa home, uchochezi mwingine inahisiwa aliuacha nyumbani !!!!!!!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo hii ndio intelijensia ya polisi? Aisee shukruni Sana.
 
Hakuna lolote. Wanapoteza muda ili tu alale ndani leo. Jumatatu wanaanza tena abradakadabra zao. Sijui tumerogwa? Unakamatwa kwa uchochezi ila uchunguzi wa askari wetu sasa...unaanzia kwa mkemia mkuu kupimwa mkojo then kwako kupekuliwa. Huu ni "ulofa na upumbavu".
Kama sio ulofa na upumbavu wange anzia wapi? Wange anzia kupekua kwanza ndio wampeleke kwa mkemia mkuu eti?
 
Mkojo unahusiana vipi na uchochezi? Hii nchi ngumu sana kwakweli
Mbona kitu kirahisi hivi,ina maana uwezo wako ndio umefika,kikomo?,INAWEZEKANA ANAPOKUA ANATOA HAYO MANENO YA KICHOCHEZI ANAKUA AMESHAWEKA VITU,jalada la uchunguzi lazima kila angle wachungulie,mbona hujahoji iweje mchochezi akapekuliwe?

ploudly ngosha [emoji243][emoji243][emoji243]
 
Mungu, mtetee Lisu.ccm hawana shida ya kuchunguza mkojo,kwani Lisu alipodaiwa kufanya uchochezi,alikojoa akiwa anaongea huo uchochezi ili wajue kama uliwaletea watu madhara ?

Hawa watu wanatafuta mbinu ya kumdhuru Lisu kwa makemikali/mariajent ya kupimia huo mkojo ! Uchochezi na mkojo vinahusiana nini ? Jamani magufuli,acha udhalilishaji wa kiwango hiki kwa binadamu wenzio !.Mungu safari hii niya miaka mingapi ?nakuomba Mungu wangu isifikie ile miaka ya wana wa Israeli.tenda Baba yangu,tuokoe hali hii imetuelemea mno.hatujui kesho nani atapimwa nini na kwasababu zipi ! Ongea na moyo wa huyu mtu,asizidi kudhuru wananchi, naomba na kuamini,Amen.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama anatumia dona basi kwisha kazi yake
Hakuna lolote. Wanapoteza muda ili tu alale ndani leo. Jumatatu wanaanza tena abradakadabra zao. Sijui tumerogwa? Unakamatwa kwa uchochezi ila uchunguzi wa askari wetu sasa...unaanzia kwa mkemia mkuu kupimwa mkojo then kwako kupekuliwa. Huu ni "ulofa na upumbavu".
wenye akili ndo wanamali

zia kumuona sizonje ????
Dah tuhuma za uchochezi na kupima mkojo kunahusiana vipi

Maamuzi kutoka Juu
Link Mawakili waliopo Mjini Kigali Rwanda Wamelaani Vikali Kitendo cha Tundu Lissu Kukamatwa

"Ni kitendo kibaya sana kimefanywa na Serikali ya Tanzania kupitia vyombo vyake vya Usalama, Tanzania inaweza kukosa mwakilishi kwenye Mkutano huu muhimu, na hili halina shaka tena kuwa, huu ulikuwa ni mpango wa siri wa Serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa Rais wa TLS hafiki hapa Rwanda ili kuficha uhalisia wa kile kinachoendelea Nchini Tanzania kwa sasa, hasa uvunjwaji wa Sheria za Tanzania na Haki za Binadamu kwa ujumla, ingawa mambo haya ya Tanzania naamini tutayazungumza kwa upana wake kupitia huu Mkutano wetu". Alifafanua Wakili kutoka Nchini Kenya aliyeko Kigali,..

Wakili Msemo Aljebra anasema Tundu Lissu alikuwa kesho Julai 21 awasilishe mada ambayo ni muhimu katika mkutano huo.
 
View attachment 547452
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema baada ya Tundu Lissu kutolewa ha Polisi cha Kati leo mchana, amefikishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo.

Mapema asubuhi, mawakili akiwamo Fatma Karume walizuiliwa kuonana naye huku Jeshi la Polisi likisema litaendelea kumshikilia hadi uchunguzi utakapokamilika.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kilichoanza jana.

"Kabla ya kuelekea nyumbani kwake Tegeta, wamempeleka kwa mkemia mkuu na ameshapimwa mkojo, sasa sijui ni kitu gani wanachunguza, kwa sasa wameshaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kumpekua,"amesema Mrema.

Licha ya kulala rumande hakuna aliyeruhusiwa kuingia na kumuona Tundu Lissu wakiwamo wanasheria wake. Mbali na Fatma, wengine waliokuwapo ni Peter Kibatala na Frederick Kihwelo.

====

UPDATE 1

Mapema kabla, Lissu alipitishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali,alikataa kupimwa mkojo kwa sababu kipimo hicho hakihusiani na tuhuma za uchochezi.

More to follow

1500678810784.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom