Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
View attachment 547452
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema baada ya Tundu Lissu kutolewa ha Polisi cha Kati leo mchana, amefikishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo.
Mapema asubuhi, mawakili akiwamo Fatma Karume walizuiliwa kuonana naye huku Jeshi la Polisi likisema litaendelea kumshikilia hadi uchunguzi utakapokamilika.
Mbunge huyo wa Singida Mashariki amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kilichoanza jana.
"Kabla ya kuelekea nyumbani kwake Tegeta, wamempeleka kwa mkemia mkuu na ameshapimwa mkojo, sasa sijui ni kitu gani wanachunguza, kwa sasa wameshaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kumpekua,"amesema Mrema.
Licha ya kulala rumande hakuna aliyeruhusiwa kuingia na kumuona Tundu Lissu wakiwamo wanasheria wake. Mbali na Fatma, wengine waliokuwapo ni Peter Kibatala na Frederick Kihwelo.
====
UPDATE 1
Mapema kabla, Lissu alipitishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali,alikataa kupimwa mkojo kwa sababu kipimo hicho hakihusiani na tuhuma za uchochezi.
More to follow
Ala ndo majibu yameonyesha hivyo?Huwezi kuwa na wenge kiasi hiko bila kutumia kitu cha Arusha
Ze kiki, bia unayolewesha sana.naona wamekosa jinai ila polisi nao wanatafuta kiki.
Kama sio ulofa na upumbavu wange anzia wapi? Wange anzia kupekua kwanza ndio wampeleke kwa mkemia mkuu eti?Hakuna lolote. Wanapoteza muda ili tu alale ndani leo. Jumatatu wanaanza tena abradakadabra zao. Sijui tumerogwa? Unakamatwa kwa uchochezi ila uchunguzi wa askari wetu sasa...unaanzia kwa mkemia mkuu kupimwa mkojo then kwako kupekuliwa. Huu ni "ulofa na upumbavu".
Linazidi kunoga.
Mbona kitu kirahisi hivi,ina maana uwezo wako ndio umefika,kikomo?,INAWEZEKANA ANAPOKUA ANATOA HAYO MANENO YA KICHOCHEZI ANAKUA AMESHAWEKA VITU,jalada la uchunguzi lazima kila angle wachungulie,mbona hujahoji iweje mchochezi akapekuliwe?Mkojo unahusiana vipi na uchochezi? Hii nchi ngumu sana kwakweli
Kama anatumia dona basi kwisha kazi yake
Hakuna lolote. Wanapoteza muda ili tu alale ndani leo. Jumatatu wanaanza tena abradakadabra zao. Sijui tumerogwa? Unakamatwa kwa uchochezi ila uchunguzi wa askari wetu sasa...unaanzia kwa mkemia mkuu kupimwa mkojo then kwako kupekuliwa. Huu ni "ulofa na upumbavu".
wenye akili ndo wanamali
zia kumuona sizonje ????
Link Mawakili waliopo Mjini Kigali Rwanda Wamelaani Vikali Kitendo cha Tundu Lissu KukamatwaDah tuhuma za uchochezi na kupima mkojo kunahusiana vipi
Maamuzi kutoka Juu
Kwahiyo?