Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa

Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa

Wwe ndiyo wa hovyo hadi nakuonea huruma, mmesha aambiwa mara nyingi sana kutokujua sheria siyo kinga ya kutokuchukuliwa hatua za kisheria!!
Hili 👆 👆 ni kweli kabisa na halina ubishi.
Lakini ni NANI anayetakiwa kuwafanya au kuwawezesha wale wasioijua Sheria waijue Sheria? Kama tukiwa waungwana kiUkweli, huyo mwezeshaji ndio awe wa kwanza kuwajibishwa halafu ndo huyo asiyejua Sheria afuate.
Ni sawa na kumlaumu mtoto asiyejua kusoma na kuandika kumbe wazazi wake ndo hawakumpeleka shule.
 
Na wewe .....tumia logic basi.......yeye yupo Dodoma amekusanyaje pesa ya wahanga akiwa Dodoma....kama sio utapeli ni nini?😀
Unajua hata mie nilikua najiuliza sana,kwani tangu ijumaa niffer tupo nae Dodoma katika uzinduzi wa duka lake,sasa nawaza kua Dar alifika lini mpaka nakuanza changisha hiyo michango?
 
Uyu dada sio kwamba watu wanamwonea wivu hapana...

Shida ni kwamba ana kiherehere sana na kuishobokea ccm,,mara kumsifia sijui nani anaupiga mwingi..mda wote kujipendekeza kwa serikali tawala..sasa ccm wanamnyoosha ndio maana wengi wanamcheka.

Ajiandae kukaguliwa biashara zake na watoza Kodi 🙂‍↔️🙂‍↔️ na kama tunavojuana wafanyabiashara tunavyofanya bidii kukwepa Kodi za serikali 🤣🤣..

Akitoka uko mwambieni aache uchawa afanye biashara zake kimya..
Sio uchawa kihelehele
 
Huyu dada inaonekana kama ana maadui wengi sasa sijui ni fitna au wivu tu juu yake au ni nini?
Maana nimesikia leo kioind wasafi radio akina zembwela na kitenge wanamkalia kooni haswa mpaka nikajiuliza ,shida ni hii hii michango au labda kuna mengine?
Wale ni vilaza bendera fata upepo kichwani ni zero
 
Back
Top Bottom