Bro! Tatizo ni sheria! Sheria inamkataza. Soma hapo namba 2. Ndiyo maana anaulizwa ikitaka kufanyiwa ukaguzi na mkaguzi mkuu wa CAG watakuwa na uhakika gani kama pesa alizozitoa ndiyo pesa halisi aliyokusanya?
kingine hiyo pesa hakuipeleka kwenye mfuko wa maafa bali yeye kama yeye alichangisha na kutaka kupeleka huduma.
Anaweza akapewa kesi hata ya utakatishaji hela na haina dhamana hiyo!
Na kilochomponza kingine ni kauli yake ya kumjibu hivyo waziri Mkuu. Wanajisahau hawa wanawake baadhi wakianza kupata majina na kukutana na baadhi ya viongozi au kutoka nao kimapenzi hivyo wanakuwa wanajiamini sana pasipo kutumia akili!
View attachment 3156476
Mkuu umesoma na kuelewa hiyo namba 2 inaeleza nini?
Hicho kifungu kinaeleza kwamba mtu akikusanya fedha za maafa ni lazima.aziwasilishe zote kwenye kamati ya maafa.
Wangetakiwa wasubiri huyo binti achangishe fedha na akishamaliza waone atazifanyeje. Kama zisingewasilishwa kwenye kamati ndio angekamatwa kwa kuvunja sheria.
Kuhusu kujua kiasi cha fedha alichokusanya na kilichowasilishwa kwenye kamati ya maafa kama ni sawa hiyo ni kazi ndogo sana kwa Financial Intelligency Unit ambao wapo wizara ya fedha .
Hii ishu Majliwa amekurupuka ingewezekana wangemtumia huyu binti positively angeweza kuwakusanyia hela nyingi sana kusaidia wahanga wa hilo janga la ghorofa
Ingewezekana Majaliwa badala ya kumtangaza vile negatively kama mtuhumiwa .
Angeagiza watu wake wa kitengo cha maafa wamuaproach positively wamuambie tumekuona mitandaoni umejitolea kukusanya fedha kwa ajili ya maafa ya kuanguka ghorofa kariakoo wangemshukuru kwa kuwasaidia kazi na wangempa maelekezo yafuatayo:-
1. Fedha za maafa zikikusanywa na mtu binafsi zinatakiwa ziwasilishww kwenye kamati ya maafa kwa mujibu wa sheria.
2. Wangemweleza pia michango anayokusanya inafatiliwa na serikali kupitia financial intelligence unit asijaribu . kuchakachua .
3. Wangempa support na promotion wangeweza kutangazia umma kwamba wanafahamu huyo binti anaendesha harambee ya kukusanya fedha za wahanga kwa niaba ya kamati.
(sheria inaruhusu kamati ya maafa kuomba msaada wa huduma mbalimbali)
4. Wangempa cheti cha pongezi na kutambua kazi aliyoifanya pamoja na kutangazia umma kiasi alichokusanya na kukiwasilisha kwenye kamati ya maafa
Hili suala lingechukuliwa hivi kwa mtazamo wangu huyo binti angeweza kuwakusanyia hao kamati ya maafa fedha nyingi sana.
Ila.lilivyochukuliwa limeleta picha ya hovyo ikiwemo kumuaibisha waziri mkuu mwenyewe pamoja na huyo binti .
Nampongeza huyo binti kwani anaonyesha anaujasiri pia anakubalika na watu wa kawaida.
Manake naamini Majaliwa michango aliohamasisha ya hili janga la kariakoo zitachangia taasisi tu za umma au binafsi tena zitafanya hivyo kwa kujipendekeza .
Huto binti waliomchangia ni kwa moyo wa dhati wa kujitolea kwa jinsi wanavyomwelewa na kumuamini na sio kujipendekeza.
Tutambue pia kushawishi watu wakuchangie fedha ni kazi ngumu sana na ukitaka kujua hayo angalia haya ma taasis ya charity yanapotaka kuajiri mtu anayeitwa fundriser hapa inahitajika zaidi soft skills ambazo serikalini hakuna serikali inajua hard skils tu kama za kukusanya kodi sijui kuuunda tasks force .kukamata mali, kufunga akaunti za watu, kutisha kufilisi,kupeleka mahakamani