Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza
Kwenye video ile (according to uchunguzi) kuna watu 6, ambako watano walionekana, kama alikuwa eneo la tukio na alikuwa na simu inaweza kuthibitishwa pamoja na ushahidi wa binti, lakini kama janja janja zishaanza kufanyika binti mwenyewe anaweza kutishwa akasema kweli alikuwa anajiuza na wale ni walevi aliowaibia vitu katika kutoa huduma zake!
NIlipomsikia chalamila anadai iundwe tume kuchunguza lile tukio nikajua kuna mchezo unataka kuchezwa,baadae tukasikia bint kapelekwa kituo cha saikoloji sijui ile ilikua ni njia tu kumficha ili asiseme ukweli ili wapate kulindana,hawa watu karma itawakuta tu
 
Mimi nilisema na ninasema tena leo, ukinipa mamlaka ya urais leo, taasisi ya kwanza kuifumua na kuisuka upya ni Jeshi la polisi. Hii ni zama za jeshi letu kuwa na watu wasomi na wasiotiliwa shaka uadilifu wao.

Huyo Mallya alichosema ni kama anahalalisha yule dada kufanyiwa alichofanyiwa. Aibu!
Tuko bara la giza ambapo kuna watu wapo juu ya sheria,hii kitu sio afya kama taifa sababu matukio kama yale yanaweza kufanywa tena na tena na mhusika akijua atalindwa kama alivyolindwa mwingine,tunatengeneza taifa la kijinga kwa vizazi vyetu vijavyo
 
Huyu afande mngese anamlinda mtu wake hapa, mmmaamaae zao polisi wa bongo
Huyu alitakiwa kufukuzwa kazi on the spot
Kama tukio lilitokea mei maana yake bint hakutoa taarifa popote na hakuna uchunguzi wa kiforensia uliofanyika.

Kesi itakuwa ngumu sana upande wa dada
 
NIlipomsikia chalamila anadai iundwe tume kuchunguza lile tukio nikajua kuna mchezo unataka kuchezwa,baadae tukasikia bint kapelekwa kituo cha saikoloji sijui ile ilikua ni njia tu kumficha ili asiseme ukweli ili wapate kulindana,hawa watu karma itawakuta tu
Sio kulindana, sasa polisi watafanya nini mbele ya wanajeshi? Ukiona hivyo ujue wamepigwa stop. Waendelee tu kuwaonea CDM.
 
Wakuu,

Naona tunaenda kufanyiwa maigizo tena na kuna mtu anataka kulindwa. Eti uchunguzi umebaini vijana wale hawakutumwa na 'afande na kwamba vijana wale walikuwa kama wavuta bangi tu na yule binti alikuwa kahaba!

Mpaka utambulisho wa moja wao umebainika halafu leo maneno yanageuzwa hivi!

Nilikuwa saluni majuzi hapa, si mnajua stori za saluni zinavyonoga sasa wakawa wanajadili suala hili, sasa kwenye stori wakawa wanasema kwamba mmoja ya wale vijana waliohusika kwenye kumbaka binti ni mtoto wa askari mwenye cheo kikubwa, sasa katika malipo vijana wengine walipunjwa mgao, ili kumkomoa jamaa kwakua baba ake ni askari ndio wakaamua liwalo na liwe, wakaachia kideo. Ni kweli au ni story tu za vijiweni kama nyingine, sijui!

Anyways, kwa mara nyingine naona sheria inaenda kupindishwa wenye nguvu wanaenda kushinda hata kama ni wanyama na makatili wanaostahili kufungwa milele

=====

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), imesema bado haijafikishiwa jalada la kesi ya vijana watano wanaotuhumiwa kutekeleza tukio la ubakaji na ulawiti wa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, Mkoa wa Dar es Salaam.

Picha jongefu (video) kuhusu tukio hilo zilisambaa Jumapili ya Agosti 4, mwaka huu kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha vijana watano wakimbaka na kumwingilia msichana huyo kinyume cha maumbile.

Pia soma: Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama

Katika video nyingine watuhumiwa hao wanasikika wakimhoji binti huyo na kumshurutisha amwombe radhi mtu aliyetajwa kwa jina la afande, naye alifanya hivyo.

Hata hivyo, katika taarifa aliyoitoa kwa umma Agosti 9, 2024, Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime alisema uchunguzi umewezesha kubaini tukio hilo lilifanyika Mei 2024 katika eneo la Swaswa jijini Dodoma.

Aliwataja vijana waliokamatwa kwa kosa la kumlawiti na kumbaka binti huyo ni Clinton Damas jina maarufu Nyundo, Praygod Mushi, Amini Lema na Nikson Jakson.

Misime alisema watuhumiwa hao walikamatwa mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani na Jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wawili ambao walikuwa hawajapatikana mpaka wakati huo.

Mwananchi leo Jumapili Agosti 18, 2024 limezungumza na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu kuhusiana na hatua iliyofikiwa katika uchunguzi wa sakata hilo na kipi kinaendelea.

Mwakitalu amesema jalada la tukio hilo bado halijamfikia mezani kwake kwa kuwa bado linaendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi.

“Bado upelelezi unaendelea na likifika kwangu ni kukamilisha upelelezi tu, isipokuwa kwa sasa bado jeshi linaendelea na upelelezi,”amesema DPP Mwakitalu.

Alipoulizwa kuhusu mwenendo wa uchunguzi wa tukio hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Ramadhan Kingai amesema aulizwe Kamanda wa Mkoa wa Dodoma na Msemaji wa Jeshi la Polisi watakuwa na majibu sahihi.

“Suala hilo mtafute Kamanda wa Polisi Dodoma au Msemaji wa Jeshi la Polisi watakueleza hatua za tukio hilo lilipofikia,”amesema Kingai

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Theopista Mallya amesema jalada la tuhuma hizo limekamilika na kwamba kesho Jumatatu Agosti 19, 2024 atafuatilia kama litapelekwa mahakamani.

Amesema katika uchunguzi, Jeshi la Polisi limebaini vijana hao waliotuhumiwa kwa madai ya kutumwa, walikiri kutoagizwa na askari kama ilivyoelezwa.

"Kilichobainika vijana hao hawakutumwa na askari, walikuwa kama walevi na wavuta bangi tu, lakini yule dada alikuwa kama anajiuza 'kahaba’.

"Neno askari ni General (jumla) kwa kuwa hata mgambo ni askari, hivyo hatuwezi kulifafanua zaidi kwa kuwa haikubainishwa wazi na tunaliacha hivyo" amesema kamanda huyo.

Hata hivyo, Mwananchi ilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi, Misime kutaka kujua kama watuhumiwa wengine wawili waliobakia kati ya sita wanaotuhumiwa hakupokea simu na alipotumiwa ujumbe kwa whatsapp aliousoma lakini hakujibu chochote.
Hii nchi wasiojielewa ni raia,
Hili siyo la kwanza na Wala halitakuwa la mwisho..
Si tumekubaliana ni nchi ya amani na mama anaupiga mwingi?
Sawa tuendelee na msimamo wetu muhimu Kila mmoja ale ashibe akojoe akalale...
Mnyonge akiiba kuku tumsulubu mpaka afe lakini wenye kushika mpini waendelee kulindana,ndiyo amani yetu hiyo.
 
Nilishasema humu kuwa hao vijana hawatofanywa chechote kile kwasababu dalili zilionekana mwanzo hakika magufuli atakumbukwa kwa mengi
Huyo ndo kabisa aive na moto kumbuka tukio la mtt wa mwisho alilofanya clouds akaja kusema ahavifanyii kazi taarifa za mtandao huyo ndo si lolote alikua na cycle yake tu unless uwe sio cycle yake
 
Huyu kwanza haheshima sheria. Ameshatoa kauli ya hukumu kwamba muathirika ni kahaba, waliimuathiri ni wavuta bangi sasa uchunguzi mwingine ni wa nini. Swali langu. How did our country come to this point kuwa na jeshi la polisi kama hili? Na wanaliangalia tu. Kuna agenda gani nyuma ya pazia? Aibu!

Ni muhimu ikiwa kuna raia mwema ana taarifa sahihi zenye uthibitisho vijana wale kutumwa na mtu kufanya walicho kifanya, ni vizuri na muhimu sana akashirikiana na vyombo vya uchunguzi au akawasilisha ushahidi huo usio na shaka kwa vyombo vya uchunguzi ili haki itendeke...

Vinginevyo, huruma pekee haitampatia haki muathirika na wahusika kupata adhabu stahiki 🐒
Huyo raia mwema hutaki aendelee kuishi,hili jambo Kwa hapo lilipofikia tafsiri yake ni Kuna mtu au watu wanalindwa na siyo wadogo.
Hawagusiki hata na Sheria
 
Wakuu,

Naona tunaenda kufanyiwa maigizo tena na kuna mtu anataka kulindwa. Eti uchunguzi umebaini vijana wale hawakutumwa na 'afande na kwamba vijana wale walikuwa kama wavuta bangi tu na yule binti alikuwa kahaba!

Mpaka utambulisho wa moja wao umebainika halafu leo maneno yanageuzwa hivi!

Nilikuwa saluni majuzi hapa, si mnajua stori za saluni zinavyonoga sasa wakawa wanajadili suala hili, sasa kwenye stori wakawa wanasema kwamba mmoja ya wale vijana waliohusika kwenye kumbaka binti ni mtoto wa askari mwenye cheo kikubwa, sasa katika malipo vijana wengine walipunjwa mgao, ili kumkomoa jamaa kwakua baba ake ni askari ndio wakaamua liwalo na liwe, wakaachia kideo. Ni kweli au ni story tu za vijiweni kama nyingine, sijui!

Anyways, kwa mara nyingine naona sheria inaenda kupindishwa wenye nguvu wanaenda kushinda hata kama ni wanyama na makatili wanaostahili kufungwa milele

=====

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), imesema bado haijafikishiwa jalada la kesi ya vijana watano wanaotuhumiwa kutekeleza tukio la ubakaji na ulawiti wa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, Mkoa wa Dar es Salaam.

Picha jongefu (video) kuhusu tukio hilo zilisambaa Jumapili ya Agosti 4, mwaka huu kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha vijana watano wakimbaka na kumwingilia msichana huyo kinyume cha maumbile.

Pia soma: Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama

Katika video nyingine watuhumiwa hao wanasikika wakimhoji binti huyo na kumshurutisha amwombe radhi mtu aliyetajwa kwa jina la afande, naye alifanya hivyo.

Hata hivyo, katika taarifa aliyoitoa kwa umma Agosti 9, 2024, Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime alisema uchunguzi umewezesha kubaini tukio hilo lilifanyika Mei 2024 katika eneo la Swaswa jijini Dodoma.

Aliwataja vijana waliokamatwa kwa kosa la kumlawiti na kumbaka binti huyo ni Clinton Damas jina maarufu Nyundo, Praygod Mushi, Amini Lema na Nikson Jakson.

Misime alisema watuhumiwa hao walikamatwa mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani na Jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wawili ambao walikuwa hawajapatikana mpaka wakati huo.

Mwananchi leo Jumapili Agosti 18, 2024 limezungumza na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu kuhusiana na hatua iliyofikiwa katika uchunguzi wa sakata hilo na kipi kinaendelea.

Mwakitalu amesema jalada la tukio hilo bado halijamfikia mezani kwake kwa kuwa bado linaendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi.

“Bado upelelezi unaendelea na likifika kwangu ni kukamilisha upelelezi tu, isipokuwa kwa sasa bado jeshi linaendelea na upelelezi,”amesema DPP Mwakitalu.

Alipoulizwa kuhusu mwenendo wa uchunguzi wa tukio hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Ramadhan Kingai amesema aulizwe Kamanda wa Mkoa wa Dodoma na Msemaji wa Jeshi la Polisi watakuwa na majibu sahihi.

“Suala hilo mtafute Kamanda wa Polisi Dodoma au Msemaji wa Jeshi la Polisi watakueleza hatua za tukio hilo lilipofikia,”amesema Kingai

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Theopista Mallya amesema jalada la tuhuma hizo limekamilika na kwamba kesho Jumatatu Agosti 19, 2024 atafuatilia kama litapelekwa mahakamani.

Amesema katika uchunguzi, Jeshi la Polisi limebaini vijana hao waliotuhumiwa kwa madai ya kutumwa, walikiri kutoagizwa na askari kama ilivyoelezwa.

"Kilichobainika vijana hao hawakutumwa na askari, walikuwa kama walevi na wavuta bangi tu, lakini yule dada alikuwa kama anajiuza 'kahaba’.

"Neno askari ni General (jumla) kwa kuwa hata mgambo ni askari, hivyo hatuwezi kulifafanua zaidi kwa kuwa haikubainishwa wazi na tunaliacha hivyo" amesema kamanda huyo.

Hata hivyo, Mwananchi ilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi, Misime kutaka kujua kama watuhumiwa wengine wawili waliobakia kati ya sita wanaotuhumiwa hakupokea simu na alipotumiwa ujumbe kwa whatsapp aliousoma lakini hakujibu chochote.
CCM oyeeeee,kazi iendelee kizimkazi mitano tena!
 
Back
Top Bottom