Polisi wapandisha bei za stika kutoka Tsh. 3,000 hadi Tsh. 7,000, ongezeko la zaidi ya 133%

Polisi wapandisha bei za stika kutoka Tsh. 3,000 hadi Tsh. 7,000, ongezeko la zaidi ya 133%

Sasa si hazija expire tulizokua nazo, au tununue mpya?
Watu hawajali stika imeexpire wala nini. Wameniambia tunatekeleza kwa vitendo kauli ya mama: kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake mradi asile mpaka kuvimbiwa.

Lakini mimi mbona naona kama hawa matrafiki walishavimbiwa siku nyingi. Au hivi vitambi vyao vinatokana na nini?
 
TANGU MWANZO HIO 3000 SIJAWAHI KUPATA MAANA WANATEMBEA NAZO MIKONONI HUZIPATI OFISINI WANAZIFANYIA UDALALI, SAIVI 10K LAZIMA ITUTOKE.

ANYWAY ZIMEANZA KUTOKA LINI KWAN WIKI YA USALAMA BARABARANI IMEANZA?
 
Yuko sawa.. Nko kwenye semina hapa wamesema imepanda from 3k to 5k, tena ukihitaji hapa hapa unapata..
Nyie wa 7k mnapigwa
Baadae nitaweka nakala ya hiyo stika ya buku 7 hapa. Kama unayo hiyo ya buku 5 tafadhali tuwekee nakala hapa
 
Wakati watu tunalia vitu kupanda bei bila kujali uchumi wa wenye nchi, Polisi wamepandisha Bei ya stika ya Saloon car hadi Tsh. 7,000 kutoka Tsh. 3,000.

Ukiwauliza hizi stika zinapunguzaje ajali, wanakuwa wakali.
Hii nchi imejaa wizi kila kona.
 
Halafu na bei za mafuta hazikamatiki
 
majukumu yao ni nini kama tena tunawalipa kukagua gari na tayari tunawalipa mishahara kila mwezi kwa kodi zetu???
Kuna kamati ya usalama barabarani ya kitaifa, mkoa na wilaya. Hawa watu lazima wale, wajenge, wanunue magari na kuchapisha placards kwa hizo stika mnazonunua. Wale matrafiki wanaokagua magari hawafanyi kazi ya kanisa, nao wana commissions zao kwenye hiyo pesa ya stika.
 
Huu ni upuuzi unaowezekana kufanyika kwenye nchi ya wapuuzi tu.
 
Halafu na bei za mafuta hazikamatiki
Bei ya mafuta soko la dunia kwa sasa ni $80/barrel down from $160/barrel wakati vita ya urusi/ukraine inaanza. Licha ya bei kwenye soko la dunia kushuka, Sisi bado tunauziwa kwa bei ile ile kana kwamba mafuta bado yanauzwa ,$160/barrel
 
Wakati watu tunalia vitu kupanda bei bila kujali uchumi wa wenye nchi, Polisi wamepandisha Bei ya stika ya Saloon car hadi Tsh. 7,000 kutoka Tsh. 3,000.

Ukiwauliza hizi stika zinapunguzaje ajali, wanakuwa wakali.
Ukiwauliza hizi stika zinapunguzaje ajali, wanakuwa wakali.[emoji23]
 
Wanajuwa mtaishia kulalamika tu

Mwisho wa siku mtazikata tu hizo stika

Ushari wangu nyie wenye magari,pakini

Ova
Kupaki gari kwa kuwa bei ya stika imepanda is the least effective method of solving the problem. Mchele umepanda hadi buku nne kwa kilo, lakini watu hatujasusa kula wali au mapilau. Na kwa Tanzania hii ukipaki gari yako, usitegemee sisi wenye ist na rumion zetu tutakuunga mkono.

Labda nikupe msemo mmoja wa kichaga: nyani hawezi kuzira kukwea mitini.
 
Back
Top Bottom