PreGE2025 Polisi watatofautisha vipi waandamanaji na wapiga kura siku ya uchaguzi octoba 2025?

PreGE2025 Polisi watatofautisha vipi waandamanaji na wapiga kura siku ya uchaguzi octoba 2025?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,937
Reaction score
41,161
Hellow!

Neno tu "MAANDAMANO SIKU YA UCHAGUZI" ni taharuki tosha.

Pale kariakoo, polisi walijaribu kushawishi wafanyabiashara wafungue maduka, haikuwezekana sababu ya hofu ya fujo na hofu ya usalama na hofu ya mwitikio mdogo wa wateja.

Saaa nimekaa hapa nauliza hawa polisi wetu ambao huwa wanapiga mabomu hovyo, polisi wanapiga virungu Kila wataekutana naye,

1. Wataweza vipi kutofautisha mpiga kura na muandamanaji Ili kumtia mbaroni muandamanaji na kumlinda mpiga kura wakati huo huo wakiondoa hofu kwa watu wajitokeze vituoni kupiga kura?

2. Je wapiga kura watapigwa chapa usoni yenye kuwatofautisha na waandamanaji Ili risasi zikifyatuliwa zisiwafikie wala mabomu ya machozi?

3. Kuweka polisi barabarani kuzuia waandamanaji siku ya uchaguzi,kutanyima haki ya polisi kupiga kura, na kutalleta hofu ya watu kujitokeza kupiga kura hasa wazee na wanawake, hii ni sawa?

4. Kwa uzoefu, Kila kituo huwa na askari mmoja tu kusimamia usalama kituoni na vituo vingine hukosa askari, sasa hao askari wa kuzuia maandamano watoke wapi, watakodishwa toka nchi jirani?

Busara ni kuchutama,
Serikali isikize hoja na kuzifanyia kazi japo kwa shingo upande!

Nawasilisha 🙏
 
Maandamano hayatozuia shughuli zingine kuendelea sasa wewe nenda katumie maandamano kuharibu haki ya watu wengine kupiga kura uone kama haujafutika kwenye uso wa ardhi.
Kituo kimoja atakuwepo askari mmoja,

Niambie hawa polisi 400,000 waweze vp kuzuia maandamano nchi nzima kwa wakati mmoja siku ya uchaguzi?

Tumia kichwa chako vizuri kufikiri.
 
Unayejiandikisha sasa, rudia kusoma kilichoandikwa hapo juu🙄
 
Naona matumizi ya nguvu siku chache kabla ya siku ya uchaguzi, kukamatwa kwa baadhi ya watu potential wa upande mmoja na kuwa retained.
 
Kabla hatujafika mwezi wa 6 maandamano yatakuwa yamezimwa! Hakuna mshenzi atakayethubutu kuharibu Uchaguzi!
 
Back
Top Bottom