Polisi watatu wafungwa miaka 20 jela kwa Rushwa

Askari hawa walikuwa wakifanya mambo aliyokuwa anayependa Magufuli kipindi chake . ================================================= View attachment 2864210
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu Askari Polisi watatu wa zamani wa Jeshi hilo Mkoa wa Arusha ( Inspekta Hillary Ferdinand Komba, Bartholomeo Augustine Maya na PC Apornary Proches Burretta ) kifungo cha miaka 20 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka.

Kosa lao hilo la matumizi mabaya ya madaraka walilifanya tarehe 19 March 2021 walipokwenda nyumbani kwa Profesa Justin Maeda Wilayani Arumeru, Arusha na kufanya upekuzi pasipo kufuata utaratibu kisha kutumia nguvu na kumchukua Profesa huyo hadi kwenye Benki mbili pamoja duka lake moja la vifaa vya ujenzi walikomlazimisha atoe pesa ( anazodai ni milioni 100) na kuwapatia ili wasimfikishe kwenye vyombo vya sheria wakimtuhumu kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na ngozi ya chui.

Profesa Maeda kwenye mahojiano ya @AyoTV_ April 2021 alisema Askari hao walimtaka awape kiasi hicho cha pesa lasivyo atashtakiwa kwa uhujumu uchumi na walimtisha kuwa jela inamuhusu, kitisho ambacho kilimfanya awape pesa hiyo harakaharaka ili kuepuka kupelekwa mahabusu au jela akihofia hali yake mbaya ya kiafya aliyokuwa nayo wakati huo.

Japokuwa Profesa Maeda alidai kuwapa Askari hao milioni 100 kwa tuhuma hizo alizodai ni za uongo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ikitoa hukumu kwa Askari hao leo imesema kiwango cha pesa walichokichukua kwa Profesa huyo ni shilingi milioni 73.

Sakata hili la Askari hao watatu liligundulika kwenye Vyombo vya dola baada ya Profesa Maeda ( pichani kulia) kujitokeza na kufikisha malalamiko yake kwa Vyombo hivyo ikiwemo TAKUKURU na Jeshi la Polisi ambalo baada ya uchunguzi wake liliamua kuwafukuza kazi Askari hao mwezi mmoja baadae. #MillardAyoMAHAKAMANI
Sabaya walimchomoa kumbe kwenye hii kesi
 
Nimeamini dhambi nilizo nazo ni ndogo sana ukilinganisha na wahalifu wengine ambao huenda wakawa kuni za kuchochea moto huko kuzimu.
 
Hata hukumu ya kifo ingetosha pia. 😭
 
Kilichomsaidia profesa itakua ana connection na kigogo serikalini la sivyo ndio alikua anaenda na maji kwa kesi ya kusingiziwa,wengi sana wamebambikiwa kesi kama hizo kwa maslahi ya polisi wachache wasio waaminifu
Alikuwa lecturer wa Sirro chuo kikuu
 
Ingependeza zaidi na mwendazake kabuli lake lipigwe pingu kwa miaka 20.

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Back
Top Bottom