Polisi watatu wafungwa miaka 20 jela kwa Rushwa

Polisi watatu wafungwa miaka 20 jela kwa Rushwa

Magufuli amefariki tarehe 17/3/2021 hao wamefanya tukio tar 19/3/2021 sasa marehemu anahusikaje au lazima uzi ulikuwa upate like na coment nyingi lazima umtaje marehemu,kazi yake ya kitume alikwisha imaliza hayupo tena muache apumzike kwa amani huko aliko!
Legacy...
Mazoea...
 
Wewe unaonyesha kiwango cha uhaya*ani kwa familia yako kuanzia kwa aliekuzaa mpaka mtoto yako
Tusameheane bosi mkubwa kwenye ujumbe wangu wa mwanzo nilikosea kusema wewe mjinga, ila pointi yangu ilikuwa siasa za kuzushiana ni mbaya sana maana zinatuondoa kwenye kijadili mambo ya maana yenye maendeleo kwa nchi yetu
 
Wewe ndiye unayestahili kutafakari kwa kina.

Kama ungekuwa unatafakari kwa kina ungejiuliza:

1) Kwa nini matukio kama hayo ya kumkamata mtu ambaye ana hela yake benki, anatishwa na polisi na viongozi wateule wa Rais kubambikiwa kesi wasipowapa pesa, kisha analazimishwa na hao polisi na kusindikizwa mpaka benki, pesa inachukuliwa kwa uimamizi wa polisi, mteule wa Rais au Polisi wanaondoka na hiyo pesa, yalifanyika wakati wa utaeala wa Magufuli tu? Hayakuwahi kuwepo kabla wala baada yake. Imethibitika, alifanya hivyo Sabaya, na sasa hawa maafisa wa polisi.

2) Kwa nini, ni wakati wa utawala wa Magufuli pekee, watu wote waliodhihirika kumkosoa Rais au Serikali yake, ama waliuawa, ama walitekwa ama walishambuliwa kwa risasi, na kunusurika kwa kudra za mwenyezi Mungu?

3) Ni wakati gani, zaidi ya wakati wa uongozi wa Magufuli, kuliwahi kutokea miili ya watu inatupwa kwenye viroba kwenye fukwe za bahari na mito, siyo mtu mmoja na siyo mara moja, na Serikali inagoma kufanya uchunguzi?

Ni dhahiri kuwa hayati MAGUFULI, hata kama hakuwaamrisha wafanye hivyo, lakini binafsi hakuumizwa wala kusikitishwa na chochote pale ambapo wateule wake au watu ambao yeye anawatumia katika uongozi wake wa kikatili, wakiendeleza ukatili kwa watu wengine. Ni sawa na Mobutu Seseseko wa Zaire aliyewaambia askari kuwawanawezaje kumwomba yeye awaoongezee mshahara wakati amewapa bunduki, akimaanisha bunduki alizowapa zinaweza kutumika katika kuwapa pesa.

Tukubaliane jambo moja, Magufuli alikuwa mchapa kazi sana lakini alikuwa mtu KATILI SANA.

Magufuli kwenye assessment ya haraka:

1) Haki za binadamu 20%
2) Demokrasia 0%
3) Utawala wa sheria 10%
4) Uchapa kazi 80%
5) Ujasiri na kujiamini 80%

Marehemu alikuwa na tatizo kubwa sana kwenye kuheshimu haki za watu na demokrasia.

Ni dhahiri marehemu aliyapenda majitu katili kwenye utawala wake, ndiyo aliyapatia madaraka.
- Umeshindwa kutofautisha wizi wa tabia na wizi wa kutumwa, naona unaandika vitu jumla jumla tu, nimeshakwambia; kama hao polisi walifanya hivyo bila ya uwepo wa Magufuli, huo ni uthibitisho hiyo ilikuwa tabia yao, na hizo pesa walizichukua wao.

- Kuhusu matukio ya watu kutekwa, sijui kama umewahi kumsikia Dr. Ulimboka na alichofanywa msitu wa Mabwepande.

Nimekusoma mwishowe nakuona unakiri kama hata kama Magufuli hakuwatuma kufanya hivyo... hapo kumbe tunakubaliana huo wizi ni tabia binafsi ya wahusika ndio maana wakaifanya hata baada ya kuondoka kwake, wangekuwa hawana hiyo tabia wasingefanya hivyo.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hawa ni majambazi tu hakuna kingine
Naomba tusikie wamefia kwenye mikono ya polisi pia huko jela kama majambazi wengine
Ila majina daa kweli upepo unavuma pande zote
Ila mnajua kuuchuna jamani
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu Askari Polisi watatu wa zamani wa Jeshi hilo Mkoa wa Arusha ( Inspekta Hillary Ferdinand Komba, Bartholomeo Augustine Maya na PC Apornary Proches Burretta ) kifungo cha miaka 20 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka.


Kosa lao hilo la matumizi mabaya ya madaraka walilifanya tarehe 19 March 2021 walipokwenda nyumbani kwa Profesa Justin Maeda Wilayani Arumeru, Arusha na kufanya upekuzi pasipo kufuata utaratibu kisha kutumia nguvu na kumchukua Profesa huyo hadi kwenye Benki mbili pamoja duka lake moja la vifaa vya ujenzi walikomlazimisha atoe pesa ( anazodai ni milioni 100) na kuwapatia ili wasimfikishe kwenye vyombo vya sheria wakimtuhumu kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na ngozi ya chui.
Hapa Faizafoxy sijui atasemaje sambamba na sakata la wiki iliyopita huko Arusha Bejamini Netanyahu
 
Kamanda Wankyo Ramadhan Nyegesa Aliiomba Nafasi Ya IGP Ili Alinyooshe Kwa Muda Mfupi
Likikaa Sawa Sawa Awaachie Wengine Sasa Wamemficha Sijui Wapi Maana Alipigwa Msukosuko Mpaka Akatupwa HQ
 
Magufuli alifariki March 17, 2021, wakati hilo tukio limetokea March 21, 2021. Kumbe marehemu anaweza kuwatuma watu?!

Msiwe mnakurupuka kuanzisha thread bila kwanza kufanya uchunguzi wa kina, na wengine nao kushangilia kama kasuku bila kufanya uchunguzi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Asipotaja mwamba kasred kake hakatavutia, pia yamkin vyeti feki group hawa watu wa vyeti feki hawajawah kupoa maumivu yao dhidi ya Chuma JPM.

Mlinunua sana vyeti vya elimu na kujipachika ufaulu msiokuwa nao.

Hata tuiopo siku tukifika madarakani tunawanyosha vile vile.
 
Moderator badilisheni heading. Mungu ndiye anafahamu jinsi Dkt Magufuli alivyokuwa mzalendo kwa wananchi wake. Hao walikuwa wahalifu kama alivyo wahalifu wa mitaani na Dkt Magufuli alishafariki hayupo na kumhusisha ni kumkosea heshima
Acha ujinga wewe chawa. Magufuli alikuwa dikteta na chawa kuliko unavyoweza kudhani 👇 👇 👇 👇 👇 👇 👇
 
Subiri za awamu hii na zenyewe akisha toka madarakani mtakuja kufunuliwa na kuona vishindo vya upigaji mshangilie hivi hivi
Kwa awamu hii, yumkini haupo uporaji wa pesa za watu mitaani, wanakomba tokea jikoni, na madeal ya kuuza rasilimali za nchi. Hawampori mtu mmoja mmoja kwa sababu hela itakuwa ndogo, wanawapora Watanzania wote kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom