SlIASA: Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limetoa kibali kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya Maandamano yaliyotangazwa kufanyika Januari 24, 2024 katika baadhi ya Mitaa ya Jiji la Dar
Kuna viji threads threads huwa vinapanda humu JF, wengi wakividharau na kuviona ni vi thread tuu vya kawaida, kumbe sio vi thread vya kawaida, ni vi thread umba!.
Thread ya kawaida ni ile thread ambayo umeandika tuu kitu chochote
ambayo haileti matokeo yoyote, lakini thread umba ni ile thread ambayo umetoa ushauri fulani, hiyo thread inakuwa imeliumba hilo jambo uliloliandika, kisha linakuja kufanyika.
Hata kama aliyesababisha likafanyika sio lazima uwe wewe, au hiyo thread yako, ila kwa vile kauli huumba, na thread ni kauli, hilo uliloshauri likifanyika, wewe unakuwa alichangia kufanyika kwa hilo jambo, thread yako inakuwa imesaidia kupaaza sauti na ujumbe kuwafikia walengwa!.
Maandamano ni Haki ya Vyama vya Siasa, Serikali itoe kila ushirikiano kwa CHADEMA hata kama uelekeo ni Ikulu
Nawatakia maandamano mema na mimi mwenyewe, Pasco Mayalla, japo sio Chadema, lakini ninashiriki kikamilifu!.
P