BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na maofisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wamezuia ndoa ya utotoni aliyokuwa akifungishwa mtoto wa miaka 15 kwa mahari ya ng'ombe kumi na fedha Sh200, 000 kwa mtoto mwenzake mwenye miaka 17.
Tukio la kufungishwa ndoa hiyo lilikuwa lifanyike jana Jumanne Agost 16, 2022 katika kijiji cha Manyada, Kata ya Usanda, ambapo askari polisi pamoja na maofisa maendeleo ya jamii walifika eneo la tukio na kuzuia ndoa hiyo kufungwa.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Mhoja, alisema walipata taarifa ya kufungishwa ndoa ya mtoto huyo kutoka kwa wasamariawema ndipo wakapanga mikakati ya kwenda kuizuia kufungwa.
Mhoja amesema mtoto huyo (jina lake limehifadhiwa) inaelezwa amemaliza darasa la saba mwaka jana katika Shule ya Msingi Manyada na hakuendelea na masomo, ndipo wazazi wake wakachukua uamuzi wa kumuozesha.
“Sisi kama halmashauri, tutaona namna ya kumsaidia mtoto huyu ili aendelee na masomo na kuweza kutimiza ndoto zake, sababu bado ni mdogo sana na hatakiwi kuingia kwenye ndoa,” alisema Mhoja.
Kwa upande wake, mkuu wa dawati la jinsia na watoto wilaya ya Shinyanga kutoka Jeshi la Polisi Brihtone Rutajama ambaye alikuwa eneo la tukio alisema katika sherehe hiyo wamewakamata bibi harusi, mshenga, mama mzazi na mjomba wake huku wahusika wengine wakikimbia.
Aidha, alisema taarifa nyingine zaidi zitatolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo Janeth Magomi juu ya hatua zaidi ambazo zinafuata kwa wazazi hao.
Source: Mwananchi