Pre GE2025 Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

Pre GE2025 Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Maisha yenyewe ya Dar ni Maandamano tosha. rejea mwendokasi
 
Yakijirudia ya UKUTA itanilazimu kubaki mtazamaji

Hatupaswi kurudi nyuma kwa sababu yoyote Ile isipokuwa watekeleze matakwa yaliyoamuliwa na chama

Wakuwajibika wawajibike na wanaowashikilia kinyume cha Sheria na wenyewe wawaachie

Tofauti na hapo tukutane tarehe 23

Bila kusahau wanazo wapi mahabusu za kuhifadhi hata 2,000 tu wetu?
 
Tusubirie kauli ya kamati baada yakuketi
@tanpol eti baada ya RAIS kutoa amri upelelezi kufanyika bila madam president kutoa kauli uchunguzi usingefanyika
 
Lipi jema kwa jeshi la polisi kuwaleta waliotekwa na kuwakamata watekaji au kuzuia maandamano?
Hakika hawa ni wanafiki

Maandamano yako pale pale asubiri Mwenyekiti Mbowe awajibu.

Ila nahisi Mbowe watamtaka ajisalimishe kwenye kituo cha Polisi kilicho karibu nae kabla ya sept23

Ila namtaka mbowe asijethubutu Kujisalimisha pressure ya maandamano hayo iko juu yanasubiriwa kwa hamu na watanzania wapenda haki na amani.
 
Ningependa kutoa pongezi za dhati kwa Jeshi la Polisi la Tanzania kwa kazi kubwa, ya kujitolea na ya weledi wanayoendelea kufanya katika kulinda usalama wa raia na mali zao. Kwa muda mrefu sasa, jeshi letu limekuwa mstari wa mbele kuhakikisha amani inatawala, huku likidhibiti magenge ya kihalifu na kuleta utulivu katika maeneo mengi nchini. Hii ni kazi ya kijasiri inayohitaji maarifa, nidhamu, na moyo wa kujitoa kwa ajili ya taifa.

Kupitia juhudi hizi, raia wanapata fursa ya kuishi kwa amani, kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii bila hofu. Tunatambua kwamba bila usalama hakuna maendeleo, na kwa hili, tunawashukuru sana maafisa wa Jeshi la Polisi kwa kujitoa kwao usiku na mchana kuhakikisha tunabaki salama. Tunaamini kuwa kwa ushirikiano wa jeshi na wananchi, Tanzania itaendelea kuwa ngome ya amani na utulivu. Hongereni sana kwa kazi nzuri mnayoendelea kufanya kwa ajili ya taifa letu! #JeshiLaPolisi #AmaniNaUsalama #Tunawaamini
 
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime, ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano yaliyoandaliwa na CHADEMA, ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika Septemba 23 katika jiji kuu la kibiashara, Dar es Salaam. Marufuku hiyo imetolewa kwa lengo la kudumisha amani na usalama wa wananchi.


Misime aliongeza kwamba hatua hii imechukuliwa kwa sababu baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA wamekuwa wakipanga mikakati ya kuchochea vurugu nchini, hali ambayo inaleta hatari kwa amani ya nchi. Alisema kuwa mara kadhaa serikali imeagiza kufanyika kwa uchunguzi ili kubaini walipo wanachama waliodaiwa kupotea, lakini baadhi ya watu wanaendelea kutoa mipango inayolenga kuharibu amani.

Soma: Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea

"Kwanini wanataka kututoa kwenye reli hatua za kiupelelezi zinazoendelea baada ya Rais Samia Suluhu kuagiza kufanyika kwa uchunguzi, mara kadhaa viongozi na wafuasi wamekuwa wakipanga na kuratibu mikakati mbalimbali na kutoa mipango yenye lengo la leta vurugu nchini ili kuharibu amani ya nchi yetu kwasababu zao wenyewe, kutokana na taarifa hiyo jeshi la polisi nchini limepiga marufuku kuacha kuendelea kuhamasisha kujihusisha katika uhalifu huo"
Nchi hii haina demokrasia kabisa.
 
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime, ameeleza kuwa Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano yaliyoan
Jeshi la polisi ni zaidi ya kwuma. Kwani maandamano ni uhalifu? Sijawahi kusikia kauli ya kipumbavu kama hii iliyotolewa na jeshi la poliCCM. Mbona CCM wakitaka kuandamana hawaulizwi? Wapuuzi wakubwa mbwa koko!
 
Andamaneni sasa keyboard warriors. Kelele za nini?
 
Ningependa kutoa pongezi za dhati kwa Jeshi la Polisi la Tanzania kwa kazi kubwa, ya kujitolea na ya weledi wanayoendelea kufanya katika kulinda usalama wa raia na mali zao. Kwa muda mrefu sasa, jeshi letu limekuwa mstari wa mbele kuhakikisha amani inatawala, huku likidhibiti magenge ya kihalifu na kuleta utulivu katika maeneo mengi nchini. Hii ni kazi ya kijasiri inayohitaji maarifa, nidhamu, na moyo wa kujitoa kwa ajili ya taifa. Kupitia juhudi hizi, raia wanapata fursa ya kuishi kwa amani, kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii bila hofu. Tunatambua kwamba bila usalama hakuna maendeleo, na kwa hili, tunawashukuru sana maafisa wa Jeshi la Polisi kwa kujitoa kwao usiku na mchana kuhakikisha tunabaki salama. Tunaamini kuwa kwa ushirikiano wa jeshi na wananchi, Tanzania itaendelea kuwa ngome ya amani na utulivu. Hongereni sana kwa kazi nzuri mnayoendelea kufanya kwa ajili ya taifa letu! #JeshiLaPolisi #AmaniNaUsalama #Tunawaamini
Subiri trh 23

Waambieni wanaopaswa kuwajibika wawajibike na wawarudishe waliowakamata kinyume cha Sheria tofauti na hapo maandamano yapo palepale
 
Kwa hiyo sasa unapendekeza tubakie kulia lia labda watatuonea huruma?
Watanzania walio wengi wako Bize na Yanga na Simba mtu wa namna hiyo ni kazi sana kumkomboa.

Yale Maandamano ya juzi juzi wengi walikuwa wanashangaa tuu wamekaa kwenye Vijiwe vyao vya Kahawa.
 
Chadema,hekima ni kusubiri upelelezi ukamilike, muone nini kimeletwa mezani, tukijadili tuone!
Hakuna uchunguzi wowote unafanywa na hao wahalifu. Imekuwa ni kawaida ccm kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuumiza, kuacha wapinzani na vilema vya maisha, hata vifo kisha polisi kujifanya wanafanya uchunguzi bila kutoa majibu. Kwa sasa uvumilivu umefikia mwisho. Cdm wafanye kama walivyofanya wamasai ili wawapate wanachama wao. Kuendelea kutegemea hao watuhumiwa kutoa taarifa ni kujidanganya.
 
Chadema watulize vishundu kwanza mamlaka zifanye kazi yake. Hata wangeandamana miezi mwisho wa siku ni haohao Polisi watakaotakiwa kutafuta na kukamata watuhumiwa na ni hizohizo Mahakama za Tanzania ambazo wanadai hawaziamini zitakazoshughulikia.

Waache siasa kwenye sheria
Kwahiyo hawafanyi kazi mpaka raisi atoe kauli ya kuwatuma. Ndio maana policcm hawapo kwaajili ya kuwalinda wananchi kiujumla bali kwa kukilinda chama cha majambazi(ccm)
 
Back
Top Bottom