Polisi yasikitishwa na kifo cha kada wa CHADEMA, Ali Kibao. Latoa wito kwa mwenye taarifa za kweli na uhakika awasilishe kwa mujibu wa taratibu

Yaani ni mlimbukeni na wachawa wenzake humu wamo yaani wanafurahia kusikia viongozi wa chadema wanatekwa na kuuawa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio taarifa ya jeshi la polisi View attachment 3090505
.
Ebu Polisi wasituone sisi ni wajinga...
Yaaani basi linavamiwa Tegeta barabara kuu... Na mtu mmoja tu anatekwa... Anapelekwa anakopelekwa... Anapigwa then mwili unaokotwa ALAFU bado mnasema tuna jeshi la polisi!
Walifanya jitihada zipi kuokoa uhai wake?
 
CCM hatuungi mkono Vitendo vya mauaji.ndio maana Chama kimelaani tukio hilo na hata serikali.ndio maana Mheshimiwa Rais ametoa maagizo ya kufanyika kwa uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo la mauaji.
Yaani mnataka kusema na tuwaamini kuwa kwa sasa kutekana ni jambo la kawaida??
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio taarifa ya jeshi la polisi View attachment 3090505
.
 
Hiyo pole kampe shangazi yako gagula huko Mbeya.
 
Pole sana ndugu yangu.Mungu akusaidie tu.najuwa unamaumivu makali na uchungu moyoni mwako.
Sana! Alafu mtu kama hajui ni kama hayupo tanzania, alisema ni drama na wengine wamesema wanajiteka, yaani mpaka iweje ndio tuonewe huruma au haya mambo yafike mwisho!? Yaani inafikia tukio linapigwa katikati ya jiji kubwa tanzania mchana kweupe na vyombo....... A! Basi bwana!
 
Acha dharau zako watu wana hasira wewe unaleta mzaha wa uchawa kwenye msiba.
 
Anaepigwa ni ng'ombe wa mwisho japo anaechelewesha ni wa mbele.
 
CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendelea kutawala kidhalimu
 
Kosa langu ni lipi katika kuwasilisha taarifa ya jeshi la polisi? Vipi kama taarifa hiyo ingetolewa na kuletwa na mtu mwingine? Acha chuki zako binafsi
Lucas, usiwaone wanaokufa ni wapumbavu sana. Huu mfumo wa kuwaua watu kwa sababu wanamkosoa Rais au Serikali kuna siku unaweza kukufikia wewe au ndugu yako. Maana hujui kesho kutatokea nini ndani ya CCM. Kikiwa cha kukukera, ukakosoa tu, ujue na wewe yatakufika.

Hawa watekaji na wauaji wapo chini ya Ikulu, na wanaripoti Ikulu, sasa polisi wanaposema watu wawapelekee taarifa, si dhihaka kubwa hii!!

Halafu na wewe unamalizia kwa kusema eti Mama ametufikia, ilihali ni dhahiri haya mambo yana baraka za ikuli; ametufikia kwa kuua watu? Unasema kazi iendelee, kazi gani, hii ya kuua watu?

Tuache unafiki, tupingane kwa hoja lakini haya mambo ya kutekana na kuuana ni ya kishetani. Kwa bahati mbaya Rais Samia na watu wake huu mfumo wa utekaji na uuaji, wameukumbatia na wanaulinda, ndiyo maana wameweka mpaka sheria ya kuwalinda hao wauaji. Samia moja kwa moja, katika hili ni sehemu ya wauaji:

1) Sheria ya kuruhusu state agents kutoshtakiwa hata wakifanya jinai kama hizi za kuteka na kuua, mswada wake uliandaliwa na Serikali ya CCM, ukaridhiwa na Baraza lake la mawaziri, ukapitishwa na Bunge la CCM, na kusainiwa na Rais wa CCM.

2) Watu wanatekwa na kuawa, uliwahi kumsikia Rais akikemea, zaidi ya ile kauli kuwa hakuna utekaji, ni drama tu? Kwa hiyo Ali amefanya drama ya kujiua. Sativa amefanya drama ya kujipiga risasi!!

3) Kwangu mimi, uhai wa mwanadamu mwenzangu, uwe ni wa Lucas, Ali, Mbowe, Mpango, Zito, Tlaatlaah, au mwingine yeyote, una thamani kuliko Urais wa Samia au ubunge wa mtu yeyote. Maana kama uhai wangu ulivyo na thamani, ndivyo ulivyo wa mwingine yeyote. Tubishane, tukosoane, tutukanane, tudharauliane, lakini KUUANA HAPANA. Haya mengine ni makosa, lakini kuua watu ni ushetani. Hii sasa ipo chini ya mashetani, yanaonfoa roho za watu wengine kama yanavyochinja kuku. Sina ushirika na muuaji yeyote yule, hata angekuwa ni ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…