Kosa langu ni lipi katika kuwasilisha taarifa ya jeshi la polisi? Vipi kama taarifa hiyo ingetolewa na kuletwa na mtu mwingine? Acha chuki zako binafsi
Lucas, usiwaone wanaokufa ni wapumbavu sana. Huu mfumo wa kuwaua watu kwa sababu wanamkosoa Rais au Serikali kuna siku unaweza kukufikia wewe au ndugu yako. Maana hujui kesho kutatokea nini ndani ya CCM. Kikiwa cha kukukera, ukakosoa tu, ujue na wewe yatakufika.
Hawa watekaji na wauaji wapo chini ya Ikulu, na wanaripoti Ikulu, sasa polisi wanaposema watu wawapelekee taarifa, si dhihaka kubwa hii!!
Halafu na wewe unamalizia kwa kusema eti Mama ametufikia, ilihali ni dhahiri haya mambo yana baraka za ikuli; ametufikia kwa kuua watu? Unasema kazi iendelee, kazi gani, hii ya kuua watu?
Tuache unafiki, tupingane kwa hoja lakini haya mambo ya kutekana na kuuana ni ya kishetani. Kwa bahati mbaya Rais Samia na watu wake huu mfumo wa utekaji na uuaji, wameukumbatia na wanaulinda, ndiyo maana wameweka mpaka sheria ya kuwalinda hao wauaji. Samia moja kwa moja, katika hili ni sehemu ya wauaji:
1) Sheria ya kuruhusu state agents kutoshtakiwa hata wakifanya jinai kama hizi za kuteka na kuua, mswada wake uliandaliwa na Serikali ya CCM, ukaridhiwa na Baraza lake la mawaziri, ukapitishwa na Bunge la CCM, na kusainiwa na Rais wa CCM.
2) Watu wanatekwa na kuawa, uliwahi kumsikia Rais akikemea, zaidi ya ile kauli kuwa hakuna utekaji, ni drama tu? Kwa hiyo Ali amefanya drama ya kujiua. Sativa amefanya drama ya kujipiga risasi!!
3) Kwangu mimi, uhai wa mwanadamu mwenzangu, uwe ni wa Lucas, Ali, Mbowe, Mpango, Zito, Tlaatlaah, au mwingine yeyote, una thamani kuliko Urais wa Samia au ubunge wa mtu yeyote. Maana kama uhai wangu ulivyo na thamani, ndivyo ulivyo wa mwingine yeyote. Tubishane, tukosoane, tutukanane, tudharauliane, lakini KUUANA HAPANA. Haya mengine ni makosa, lakini kuua watu ni ushetani. Hii sasa ipo chini ya mashetani, yanaonfoa roho za watu wengine kama yanavyochinja kuku. Sina ushirika na muuaji yeyote yule, hata angekuwa ni ndugu yangu.