Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?


  • Total voters
    244
They were both great Men. We don't need to fight who is the best. We can just accept the were true African greats and the very best of us.
 
Kama ulidhani USA ndio nchi yenye huduma bora na maisha bora kwa watu wake pole sana.

Sasa nimejua kuwa najaribu kumuelewesha mtoto wa elimu ya Shule za kata aliyefaulu kwa bahati mbaya. Kwa mtu mwelevu hawezi kuitaja USA kwenye nchi zenye huduma bora kwa watu wake au nchi yenye maisha bora kwa watu wake.

Libya ya Gaddafi mfano wake kidogo labda uilinganishe na Scandinavian countries like Sweden tena kwa mbali.

Rudi shule mkuu.
Mkuu umenifanya nicheke peke yangu kwenye gari, asante na pole mkuu.
 
Umenena vyema. Madiba ndio maana anapewa sifa sana na wazungu kwa kuwa hakugusa maslahi yao ya kiuchumi na kijamii huko SA. Wazungu waliendelea kuwa wamiliki wa uchumi na pia 1st class citizens.

Lakini kwa upande wa Africa hakuna hata nchi moja aliyowahi kuisaidia.sasa inakuwaje leo tumtaje kama HERO wa Africa!!!!
Ni somo pana sana mkuu kwa wabongo hawawezi kuuelewa. Vyombo ya mangaribi hasa media na viongoz wao wanampamba sana madiba kwa sababu hakugusa maslahi ya wazungu.

Uchumi wa SA unamilikiwa na wazungu, bado ubaguzi upo kuna sehemu black hawawez ingia sasa unajiuliza ni uhuru gani huo?

Ukweli mchungu cheki watu waliopiga kazi kama Nyerere, Gaddaf au Sankara uone kama kuna western media inayowataja!

Wabongo hawajafahamu role ya media wao wakisikia wanameza tuu bila kufanya utafiti.
Msamaha ni jambo jema ila madiba angefikiria zaid namna ya kuwainua waafrika wenzie sio kuacha hizo mizungu isiyokua na tija ikizoa mali ulaya tuu na kudharau waafrica.
 
Mbona uingereza na ujerumani waliua watu wetu na kututawala lakin Bado tunawashobokea, acha hizo wewe

..hold on.

..Wajerumani waliua watu wetu wakati wa vita vya Maji Maji.

..German Chancellor wakati huo alikuwa anaitwa Bernhard von Bulow.

..sasa hebu tueleze ni lini ulisikia waTz "wakimshobokea" Chancellor Von Bulow wa Ujerumani?

..UV-CCM someni kidogo kabla hajaanzisha thread.
 
..madai yangu ni kwamba Gadaffi aliuawa askari wetu wakati wa vita vya Kagera.

..na kwamba Mtanzania anayemuenzi Gadaffi hana uchungu na maisha ya wenzetu waliopoteza maisha wakipigana na majeshi ya Amin na Gaddafi.
Skia nikuambie mkuu kwa busara za Nyerere sidhani kulikua na haja ya kuingia vitani.
Unajua nini pamoja na kuvamia mkoa wa kagera na kuweka bendera yao bado naamin Nyerere angeweza kufanya diplomasia yule mhuni aondoke.

Pili ni dhahiri Nyerere alikua na mapenzi binafsi na Obote ndo maana baada ya kumtoa Iddi Amin, Miltone Obote alirejea nafsi yake.

Hii ilikua ishu binafsi zaid.
Sasa umepoteza wanajeshi zai ya 300 kuna lipi la kujipongeza? Uchumi chali ukizingatia taifa bado ni changa.

Nyerere katufanyia mengi ila hapa nampinga kidogo, sababu ya kuingia vitan ni chuki yake dhidi ya Iddi Amin.

Swala la Gaddaf kumsaidia Amin ni ishu ya love kwani walikua washkaji kitambo tuu ila Gaddaf alikuja kukiri na akaomba msamaha baadae kwa kitendo alichotufanyia watz.
 
Unajua sana sema udini umekujaa
Nilikuwa nahisi unachangia kutokana na dini ya wanaojadiliwa sasa kwa post yako hii nimeamini udini umekujaa, Rais wa tz kila siku akitoa mfano anaitolea libya na si SA
 
Ukisoma historia ya gaddafi utajua nini maana ya kiongozi!! mabeberu wa nchi za mangaribi ni watu hatari sana!!

Walibya hawatakaa wapate waliyoyapata kutoka kwa gadafi!! mpaka sasa Libya haijatulia!

Japo nimempigia kura gadaffi lakini hamna mtu anaweza itaja africa bila kuwataja mandela, nyerere, kwame nkuruma plus gadafi!!
Wazungu wame brainwash waafrika sana. Tunaibiwa halaf tunajipoingeza kwa kuibiwa et?
Bado tuna safar kubwa sana waafrika. God bless us.
 
Kuna watu wanajua Mandela alikaa tuu jela hakufanya kitu chochote...Mandela alipokua jela alikua anatuma ujumbe wa maandishi ambao ulikua ukisoma sana na mtoto wake wa kike au Winnie Mandela mpaka ilifikia maandamano makubwa yaliyokua yanatokea mauaji ya watu weusi 600 sophia Town ilikua hamasa ya Mandela na ilitangazwa kuwa ni kosa la jinai kuonesha picha ya Mandela..Mandela aliambiwa aache siasa apelekwe aishi USA aligoma aliwaambia atakaa jela mpaka kufa kwake au SA itakapokua huru na wafungwa wa kisiasa waachiwe ndio yeye atakua huru..wapo waliokaa jela muda zaidi ya Mandela kama Walter Sesulu lakini hawakupata adhabu kubwa au suruba sana kama Mandela ndio maana ana heshima kubwa sana pamoja na Stive Biko..
 
Toka atume askari wake Uganda wakati wa vita vya Iddi Amini, nimemtoa maana Gadaffi. Kazi yake kuu ilikuwa Islamization of Africa, hata misaada yake ilikuwa na mrengo huo. There is no way he can be an African hero.
 
Back
Top Bottom