Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?


  • Total voters
    244
Kuna watu wanajua Mandela alikaa tuu jela hakufanya kitu chochote...Mandela alipokua jela alikua anatuma ujumbe wa maandishi ambao ulikua ukisoma sana na mtoto wake wa kike au Winnie Mandela mpaka ilifikia maandamano makubwa yaliyokua yanatokea mauaji ya watu weusi 600 sophia Town ilikua hamasa ya Mandela na ilitangazwa kuwa ni kosa la jinai kuonesha picha ya Mandela..Mandela aliambiwa aache siasa apelekwe aishi USA aligoma aliwaambia atakaa jela mpaka kufa kwake au SA itakapokua huru na wafungwa wa kisiasa waachiwe ndio yeye atakua huru..wapo waliokaa jela muda zaidi ya Mandela kama Walter Sesulu lakini hawakupata adhabu kubwa au suruba sana kama Mandela ndio maana ana heshima kubwa sana pamoja na Stive Biko..
Mkuu hayo ni mambo ya kawaida sana tena sana. Umejiuliza watu waliopigana msituni huko bila chakula wala msaada wowote? Hapo jela madiba alikua akihudumiwa kama binadamu tuu na ugali na hakika alikula swala je angepigana msituni jee?

Mkuu kuna watu wamepiga kazi we acha tuu. Ukisikia mtutu we kaa mbali.
 
Mkuu mimi sina tatizo kabisa na Gadafi, tatizo langu ni kumlinganisha na Baba wa dunia mzee Madiba.
Unamchukulia MADIBA (Baba Mandela) kama Baba, kioo cha Afrika kwa yapi...! au Mazingira gani...!!

Kwa ustawi wa Afrika na Maendeleo ya Raia katika NCHI....Ghadafi ni mtu wa kupigiwa UPATU...!!

UKUBALI ama UKATAE...
 
1. Nyumba bora kwa kila mwanalibya. SA bado mamilioni ya watu wanaishi kwenye slum.

2. Kusomeshwa bure kwa kila mwanalibya. SA kila kitu ni kulipia.

3. Umeme wa bure kwa kila mwanalibya . SA unalipia kila kitu.

4. Apartments kwa kila graduate na kuozwa mke/Mme na utaanza kulipa rent ukipata ajira. SA hakuna hili.

5. Libya ilikuwa ikifadhili kwa pesa AU. SA haifanyi hivyo.

6. Libya ilikuwa inakopesha nchi za kiafrika bila riba na misaada ya kimaendeleo isiyo mikopo. SA haifanyi hivyo.

7. NK.
Haya mamvo uliyoorodhesha Walibya hawayafahamu.Watanzania wanayajua zaidi ya Walibya
 
Hiyo ni geopolitics Mkuu, kwani wewe una uchungu na Tanzania kuliko mwalimu Nyerere?, Mbona baadae Mwalimu na Ghadqfi walikuja kuwa marafiki na hata Hela za kujenga msikiti kule Butiama Mwalimu alipewa na huyohuyo Ghadafi?
Kuwa marafiki hakuoneshi umuhimu wake kwa Africa
 
Ni somo pana sana mkuu kwa wabongo hawawezi kuuelewa. Vyombo ya mangaribi hasa media na viongoz wao wanampamba sana madiba kwa sababu hakugusa maslahi ya wazungu.

Uchumi wa SA unamilikiwa na wazungu, bado ubaguzi upo kuna sehemu black hawawez ingia sasa unajiuliza ni uhuru gani huo?

Ukweli mchungu cheki watu waliopiga kazi kama Nyerere, Gaddaf au Sankara uone kama kuna western media inayowataja!

Wabongo hawajafahamu role ya media wao wakisikia wanameza tuu bila kufanya utafiti.
Msamaha ni jambo jema ila madiba angefikiria zaid namna ya kuwainua waafrika wenzie sio kuacha hizo mizungu isiyokua na tija ikizoa mali ulaya tuu na kudharau waafrica.
Wabongo wamelogwa na uchawi wa laboratory sijuwi kama mnalijuwa hilo baadhi ya midume imegeuka kama wanawake kwa USA wapo radhi kwa lolote kwa nchi za magharibi
 
Gadafi ni kidume wewe,ile nchi imejengwa kwa kukomaa kwake..pia alitoa pesa nyingi tu kwa ajili ya AU...nchi yake ilikuwa na waislam wengi lakini akakataa nchi kutawaliwa kiislam
 
wote!!

kila mmoja ana role yake na legacy yake

sons of africa!
 
Wazungu wame brainwash waafrika sana. Tunaibiwa halaf tunajipoingeza kwa kuibiwa et?
Bado tuna safar kubwa sana waafrika. God bless us.
Hatuibiwi,kuna MaPimbi ambao ni watu miongoni mwetu wanaowapa kibali hao wezi
 
Wabongo wamelogwa na uchawi wa laboratory sijuwi kama mnalijuwa hilo baadhi ya midume imegeuka kama wanawake kwa USA wapo radhi kwa lolote kwa nchi za magharibi
Kuna vitu inabidi uombe Mola asaidie tuu maana bila yeye Africa tulishaishia pabaya siku nying sana.
 
Back
Top Bottom