POMBE ‘Ganzi yenye maumivu’ (Safari yangu ya kuacha pombe)

My dear bottle !

Chanzo cha yote ni pombe. Unaamka asubuhi unaenda kuoga uende kwenye mitikasi unashangaa kuona wapangaji wenzako wanakuangalia kwa huruma. Kumbe jana usiku ulikuja upo kiwingu ukaanza kumtongoza mama mwenye nyumba wako, mpangaji mwenzako wa kiume akakutoa.😁

My dear bottle!

Unakopa hela iende kwenye biashara, unasema wacha kwanza niende matako bar nistue moja baridi. Alafu nikadake mazaga, imeisha hiyoo.

Mpe pombe masikini asahau shida zake! Sababu bilion 1 madhara ya ulevi kupitiliza. Drink Responsibly!
 
Si muda mrefu sana ni miezi mitano tu sasa tangu niache naimani sitarudi tena
Ngoja niweke comment hapa ili mwakani tukuulize kwa mwaka mmoja pesa uliyookowa umefanyia nini? Itabidi utuoneshe nyumba au gari.
 
Nashukuru sana mkuu, kweli wanawake wanaoishi na walevi wanavumilia mengi sana hata wale wanaojiita walevi wastaarabu nao ni shida tupu nimekaa nao mimi unaweza kumuona mstaarabu sana kumbe kuna mambo ya kishenzi anayafanya gizani

Ni kwamba inapunguza ustaarabu wa wengi.

Wanasahau ahadi zao. Afya zao, familia zao, biashara, kazi zao, heshima zao. Wakipitiwa.

Wengi ni kero kubwa kwa familia, koo zao. Sababu wakilewa muda huo mchache unafuata wanafikiria pombe tu. Zikiisha ni watu wazuri. Tunaishi nao.
 
Mkuu Hongera sana.

Mimi pia kwa sasa namaliza mwezi wa pili baada ya kuachana na ulevi wa namna hiyo

Na naomba nikuunge mkono kuwa ni kweli pombe inaingiza watu kwenye matatizo mengi hasa Madeni, Uzinzi, migogoro ya ndoa, kupoteza kazi, kupoteza mali na kadhalika. Ni vigumu sana watu wengine kuelewa maana kuhusu ulevi it's all about levels, yaani mtu kafikia ulevi wa aina gani na amepata uwezo wa aina gani wa kujitambua.

Pombe ni mbaya sana. Tunywe kistaarabu kama tunakunywa , na imiwezekana tuache na tuwakimbie marafiki hawa wa pombe na tuwakemee

Asanteni sana
 
Umeongea ukweli 100% yaani hata wenye pesa nyingi za kuchezea, akichezea pesa kwasabab ya pombe na wanawake ni kawaida na lazima ataamka asubuh roho inamuuma nafsi inamsuta kwa upuuzi aliofanya jana yake...
Kuna watu humu mnajifanya walevi wastarabu lakini ukweli ni kwamba pombe inamaliza pesa, hata kama unakunywa bia mbili kusema kwamba unamatumiz mazuri ya pesa ni upumbav na kujipa moyo ujione unazimudu pombe...
All in all pombe ni tam sana ila zinatuCost sana kwa namna nyingi
 
Keleleee nyiingii, sasa mbona wanywaji pombe ndio wenye maendeleo?

Ndinga kali zinapaki bar sijawahi kuona vijiwe vyenu wacheza karata, bao na draft kuna mtu kapaki hata Sn Lg tu.

Sasa mtu unasema pombe inamaliza hela kwani kazi ya pesa ni nini?

Kila mtu na vipaumbele vyake, wengine pesa zao zinaliwa kwenye ushirikina, wengine pesa zao zinaliwa makanisani na mitume na manabii kwa kuwatishia moto feki ahera wakati wao wenyewe hawajui majaliwa yao ya life after death.

Umeacha piga kimya njoo baada ya miaka mitatu utupe ushuhuda uliacha pombe na umalaya ukafanikiwa kusave na ukafanya moja mbili tatu, au show us your Ferari tutakuelewa, otherwise hizi nyenyenyenye hatuzitaki hazina tija.
 
Kwa hiyo ukiwa na laki tano yote unaenda nayo bar mkuu badala ya kuchukua elfu 30 au 40 na nyingine kuacha home??
 
Mimi ndio maana baa huwa naenda kama mchawi huwa sipendi kampani za kidwanzi unawanywesha watu kwa pesa yako ila wao hawazungushi raundi
Au unakaa kaunta.. Ukiondoka kaunta unampa bia moja na mnakuwa marafiki hata siku ukisahau kitu anakutunzia na pia hata ulewe vipi hakuzidishii bili
 
Daaah lile lichupa likubwa ukalikata?? [emoji12] [emoji12] Haukuzima?? Maana ndiyo moja ya side effects za hiyo Kitu...
 
Allahuma Ameen.
Don't look back bruda.
 
Hii kitu ikiingia kwenye damu kuacha ni inshu,baada ya kujua mke wangu kazalishwa nje na mtoto sio wangu, hapa ndipo nilipoanzia kua chapombe, mwaka mmoja na nusu sijagusa pombe na sitaki tena.
 
Mkuu Mungu anitie nguvu nmeipiga chini sababu ya aibu inayoniletea ,nikirudia hakika ntakuwa nunda nmechoka na sumu acha niwe huru.
 
Allah azidi kukuongoza ndugu yangu katika imani fanya toba ya kweli kabisa na udhamirie haswa kuacha Pombe

Lakini ndugu yangu isijekua umeacha kisa mambo yapo kombo ila maisha yakirudi katika hali nzuri unarudi huko
Cha mwisho cha kukushauri tafuta darsa uwe unasoma ili ujiweke karibu na mola wako

kuhusu Madhambi ya Pombe uloyafanya usikhofu sana kwani Allah anasema maovu atayabadilisha kua mema soma aya 2 za chini hapo utaona
 
Bado muda utafika
 
Hongera Sana Mkuu Kwa hatua hiyo,ni uamuzi unaohitaji ujasiri mkubwa, Mimi mwenyewe ni mnywaji sana lkn sio mlevi maana nakunywa kwa viwango vyenye mipaka,na sijawahi kufuja pesa kiasi ambacho wewe umeelezea.
 
Daaah lile lichupa likubwa ukalikata?? [emoji12] [emoji12] Haukuzima?? Maana ndiyo moja ya side effects za hiyo Kitu...
sikuzima ,hata hivyo nilikunywa nikiwa nyumbani,aisee nilipoamka ndo hivo chakula chochote hakiliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…