POMBE ‘Ganzi yenye maumivu’ (Safari yangu ya kuacha pombe)

Naungana na mleta mada. Nimekuwa chapombe kwa miaka 27 mnywaji wa kila siku. Hapa nina mwezi na nusu sijagonga tungi na hii ni baada yakutafutiwa dawa ya kienyeji kwani majaribio yote yakuacha yalikuwa yanashindikana.
Pombe ni hasara sana.
Imenirudisha nyuma sana kimaendeleo nakunywa hadi 30k kwa kutwa, kiwango kidogo cha matumizi yangu ya pombe ni 2-3k kwa kutwa nikiwa nimefulia. mixer migogoro isiyoisha.
Naomba Mungu nisirudi tena huko.
 
Hahahahahaha[emoji23][emoji28][emoji28]

Afuu kweli asee, sijawahi ona wanywa soda wamepaki X6

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Hii kitu ikiingia kwenye damu kuacha ni inshu,baada ya kujua mke wangu kazalishwa nje na mtoto sio wangu,hapa ndipo nilipoanzia kua chapombe,mwaka mmoja na nusu sijagusa pombe na sitak tena.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2][emoji1787][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Wamejaa porojo tu kufundisha watu maisha wakati kila miaka inavyokwenda ndio wanazidi kupigika tu.
kuna wasiokunywa pombe waliofanikiwa,pia kuna wanywa pombe waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa pia
 
Umeongea ukweli mtupu,achilia mbali hayo matumizi mabaya na uasherati,pia inashawishi hata kuiba sehemu yako ya kazi kama kuna hiyo mianya,lakini pombe ina madhara sana kwenye afya zetu,walevi wengi au wanywaji wasio na mipaka wameishia kuugua Pressure,kisukari,ini,Figo,uchizi n.k...
 
Amekudanganya nani? Hayo magonjwa ni life style za binadamu wenyewe, unywe pombe, usinywe pombe mtindo wako wa maisha utakufikisha hapo.

Mtu pombe hunywi halafu unakula hovyo kama nguruwe wewe unadhani kati yako na anayekunywa pombe nani mwenye hatari ya kupata hayo maradhi? Kwanza hicho kisukari ni magonjwa ya kurithi hayo.
 
InshaAllah!... Hii nimeacha kwa nia moja mkuu na sio kwamba namaisha magumu sasaivi, kama ni pesa ya matumizi hainipigi chenga kama ningekuwa na nia ya kulewa nisingeshindwa kunywa kila siku
 
Endelea tu kunywa babu yangu,fainali ni uzeeni,utanitafuta siku moja na kunipa beer moja ya baridi ya Carlsberg kuniunga mkono ninayoyasema...
 
Endelea tu kunywa babu yangu,fainali ni uzeeni,utanitafuta siku moja na kunipa beer moja ya baridi ya Carlsberg kuniunga mkono ninayoyasema...
Sasa si mpaka ufike uzeeni? Unaweza kufa mapema tu kwa pneumonia.
 
Usiache pombe sababu ya umaskini acha pombe sababu umeamua nakuhakikishia yeyote anaecha sababu amekosa pesa siku akizipata itakuwa hatari mara 11.....mimi mlevi hayo yote nayapitia sio siri ila life goes on......drink responsible
 
Usiache pombe sababu ya umaskini acha pombe sababu umeamua nakuhakikishia yeyote anaecha sababu amekosa pesa siku akizipata itakuwa hatari mara 11.....mimi mlevi hayo yote nayapitia sio siri ila life goes on......drink responsible
......mustakabar different.👏👏😄😄
 
Hongera sana mkuu.
Inawezekana kabisa kuacha pombe moja kwa moja na ukafurahia maisha kwa njia nyengine.
Nami nilikuwa mlevi pia ingawa sikufikia kiwango hicho ulichoelezea lakini bado hali haikuwa ya kujivunia hata kidogo na kwa namna fulani najutia maisha yale.
Namshukuru Mungu huu ni mwaka wa nne sasa nimeshaachana na pombe na kwa sasa najiona nipo huru sana.
Allah akusimamie katika maamuzi yako haya uweze kufanikiwa na akuongoze katika kheri.
Pia unapoleta uzi kama huu inabidi ujiandae kwa kejeli na dhihaka za kila namna kutoka kwa wale wanaojiita 'wanywaji'.
Hivyo wewe jikite kwenye maudhui ya uzi wako kwani naamini una faida kwa wengi ambao bado wamefungwa kwenye jela ya pombe na wanatamani kuachana nayo,na hao ndio wengi.
 
Pombe siyo jela ila pombe si kwa ajili ya kila mtu.

Kuna watu maisha yao yote hawajawahi kugusa hata pombe ila starehe zao ni hatari tupu, umalaya na kamari, huko kuna matumizi makubwa kuliko pombe.

Kwanza nieleweke mimi hapa sitetei pombe ila kuna wengi wanakunywa tu pombe kwa kuiga hao wanapaswa kuacha mara moja au kutumia kiasi kidogo tu.
 
Wewe jamaa kama vile ili bandiko ni lakwangu linanihusu kwa kila kilichopo kwenye hu uzi, nami nimekata shauri naelekea kufikisha mwezi Sasa. Kikombe noma sana wakuu kinaharibu future mazima
 
Pombe imenifanya nikajenga njoo kaskazini uone kama kuna mlevi maskini
 
Wewe inaonekana una stress za maisha, inaonekana umefeli shule hadi maisha, nyie ndio mkiwa bar mnatusumbua kuomba bia, na safar hii utapumuliwa sana mbwa wew. Jifunze kusoma na kuelewa hoja za watu sio unakurupuka tu
Umeandika pumba shehe ungejikita kujibu hoja zake na sio hizi taarabu uNazoleta acha ujinga jibu maswalibyake kama unaaweza
 
unachotetea hakieleweki mwishowe unaonekana mpuuzi tu wa mtaani mlevi asiye na mbele wala nyuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…