POMBE ‘Ganzi yenye maumivu’ (Safari yangu ya kuacha pombe)

POMBE ‘Ganzi yenye maumivu’ (Safari yangu ya kuacha pombe)

Memtata

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
587
Reaction score
1,863
Kama ulishawahi kusoma nyuzi zangu mbili tatu hapa JamiiForum utagundua kabisa mimi ni cha pombe. Nikwambie tu mada zote nlizowahi kuzileta hapa ni za ukweli isipokuwa huwa nabadili kidogo maudhui ili kuepuka wazee wa kuunga dots, bado sijawa tayari kujiweka wazi mimi ni nani maana mengi ni ya aibu kwangu na jamii inayonizunguka na mengi nilikuwa nayafanyia gizani ukija mtaani kwangu mimi ni mtu mstaarabu na mpole sana.

Leo nimekuja tena na mada hii ya pombe lakini si kwa kuipa sifa za kijinga kama ilivyokuwa kwenye mada zile bali kuelezea jinsi nilivyoamua kuacha pombe, naamini sitarudi tena huko kwa bidii zangu na uwezo wake Allah (SW).

Kuna sababu nyingi zimenifanya kuacha pombe lakini kubwa zaidi ni madeni. Pombe iliniingiza kwenye madeni makubwa sana ambayo hadi leo hii bado kuna ambayo sijayamaliza, bado kuna watu nawalipa taratibu maana yalikuwa ni madeni haswa sio videni, kwa kipato changu kudaiwa 3,000,000 (milioni tatu) ya riba kubwa na mtu au watu ni jam kubwa sana na hapa sijaweka deni la taasisi ambalo natembea nalo mwaka wa pili huu sasa, nafikiri kwa sasa ngoma itakuwa bado inasoma kama 30 something million hivi au chini kidogo ya hapo.

Waajiriwa wengi na wafanyabiashara huchukua mikopo bank na huwa na manufaa sana kwao kwani husaidia kutimiza malengo yao kwa wakati lakini kwangu imekuwa kimeo sababu mkopo niliochukua nilitimiza malengo machache sana ya msingi na kubwa kuuza sura kwenye maeneo ya starehe na kulipa madeni (yani deni kwa deni!)

Mtu unaweza kujiuliza pombe inasababishaje kuingia kwenye madeni ya mamilioni?! Kama wewe ni mlevi, mpenda starehe na sifa bila kujali kipato chako huwezi kunishangaa ila kama wewe una sifa hizi na bado unanishangaa basi mshukuru Mungu kukupa uwezo huo wewe ni mlevi mwenye kujitambua. Hapa sijakataa kuwa wapo walevi wastaarabu wasiofuja pesa japokuwa hata kwao huwa haikosekani hata ile kidogo ya kujilaumu kutumia pesa tofauti na malengo.

Lakini usilewe sifa kimsingi walevi wengi ni wa hasara sema tu walevi huwa na tabia moja; Maumivu na mateso wanayopitia huwa hawapendi yawe wazi, maranyingi hupenda kuonekana wao ni watu wanaofurahia maisha kuliko yeyote hapa duniani na siku zote utawasikia “Basi pombe inamaliza hela ndugu yangu!... Mimi nikiwa hata na elfu kumi nalewa na nnarudi zangu nyumbani”. Weeeee!!!.... usijaribu ndugu yangu hakunaga mlevi wa hivyo na kama rafiki yako mlevi anakuambiaga yuko hivi anakudanganya.

Pombe imebeba mzigo mkubwa sana nyuma yake, usione mtu bar na bia yake mezani akinywa huku akitabasamu pekeake, akipiga story kwa uchangamfu na rafiki zake au akisimama na kucheza kwa furaha ukadhani mtu huyo ni mwenye kufurahia sana maisha na pombe inaishia hapo tu. Elewa kabisa nyuma ya pazia kuna mengi. Uzinzi, ufujaji pesa, kutoa ofa hovyo hata kwa usiowafahamu, kula hovyo (barbeque) hatakama huna njaa na kukopa hovyo ilimradi siku hiyo utimize lengo. Vyote hivi vipo nyuma ya pombe.

***Uko nyumbani kama mgonjwa sababu ya kuwaza pesa uliyoharibu jana kwenye pombe, huna raha kabisa maana unawaza ile pesa uliyochezea ungeweza hata kufanya kitu fulani cha maana. Mara inaingia simu toka kwa swahiba wako mlevi mwenzako.

“We Gee uko wapi?” inasikika sauti ya kilevi.

“Home Mazee” unajibu kinyonge kama mgonjwa sababu upo kitandani huna usingizi ila umelala na kujipindua pindua ukiwa umesongwa na mawazo.

“Aaaaah hahahaaa!!!.... we mjinga umelala nini? Acha ujinga wewe njoo hapa Machakani Lounge tupige vitu” anaongea jamaa yako akionekana mwenye furaha sana huku pembeni ukisikia shangwe la kutosha toka kwa wadau wengine.



Kwakuwa unajua shoo za mdau wako huyu unakurupuka kitandani bafuni fasta piga mswaki unaoga na kuvaa chap huku ukijiliwaza.

“Bora niende huko nipunguze stress maana nikikaa hapa nyumbani nazidi kuchanganyikiwa”

Unatoka ukimuaga mkeo na kumuomba akuazime 20 (toka kwenye hela za matumizi ya nyumbani) maana unaona kwenda mikono mitupu kabisa ni aibu lolote linaweza kutokea.

Unafika bar kweli jamaa wamewaka, vibe la kutosha kwenye meza ya duara kuna watoto wakali kama wanne hivi na washkaji wapo watatu tu, baada ya utambulisho unagundua kabisa mmoja umeachiwa wewe na kawaida ya walevi utasikia;

“We vuta kiti pale, wewe njoo huku alafu huyu akae hapa”

Unasogezewa zigo kiulaini bila hata kutumia nguvu, niwaambie tu jamani walevi maranyingi huwa hawatongozani mambo huwa yanajipanga yenyewe kama game tu. Ukiwa hujalewa vitendo hivi utaona vya kawaida kabisa wala havikuchukulii muda sana tena kuna wakati unajisemea moyoni

“Leo mimi nimekuja kulewa habari za wanawake sitaki, kwanza sina hela kabisa sitaki mambo mengi leo”

Ganzi ikianza kukuingia upuuzi unaanza pia. Dem ulikuwa unamuona wa kawaida mara unaanza kumuona Cleopatra na hivi wakati huo kakulalia pegani kichwa kinakujaa mwanaume unaanza kupiga hesabu kichwani. Mfukoni una 20 tu kuna watu wanakunywa wine hapo, 20 haitoshi. Fasta unamcheki mdau wako wa pesa za moto (za riba umiza) na walivyo hawa jamaa huwa wanaamini sana walevi (wenye vyanzo) hata ukimuomba laki3 wakati huohuo anakuletea, hii inanikumbusha jamaa mmoja aliwahi comment kwenye uzi wangu akisema kwamba alipokuwa mlevi alikuwa hakosi pesa kabisa tofauti na alipoacha. Huu ndio ukweli walevi huwa na mipango mingi ya pesa sema pesa zenyewe huwa za moto🤣 . Mzigo ukifika bata linaendelea....***

Unafikiri asubuhi utaamkaje tena? Juzi umechezea pesa ukaamka unajilaumu, jana rafiki zako wanakushawishi ukanywe unaona ni sawa ili upunguze mawazo lakini baada ya kulewa unajikuta unafuja tena pesa!! Umeamka pombe imeisha na pesa imeisha na deni juu! Kweli pombe ni ganzi yenye maumivu tena maumivu makali sana.

Hii ni sababu kubwa iliyonifanya kuacha pombe, rafiki zangu wengi hawajaamini kama nimeacha na wengine wanafikiri nimetumia dawa au nilipewa dawa na ndungu zangu bila mimi kujua lakini ukweli ni kwamba nimeamua mwenyewe kuacha na InshaAllah sitarudi tena huko. Ili kukaa mbali na pombe nikaamua kuwa karibu na Allah sasaivi nafanya ibada maana ibada hutuweka mbali na maasi. Ukiwa na hofu ya Mungu utafata maamrisho yake.

Makosa yetu na ya watu wanaotuzunguka yawe funzo na si kuzidi kujaza kurasa chafu kwenye kitabu cha maisha yetu.

Wasalaam.
syringe.jpg
 
Wewe ulikuwa mnywaji uchwara. Wanywaji uchwara wengi hujilaumu asubuhi baada ya pombe kuwapeleka puta jana yake. Yani wengi wanafanya mambo ya kitoto kitoto na hao ni bora wakae mbali na pombe. Wakinywa wanaweza hata kupumuliwa kisogoni au kutongoza mama mkwe!
 
Yaani nikope pesa kwa ajili ya pombe? Aisee mimi ni mlevi lakini siwezi kuingia madeni sababu niendelee kulewa, Nilijifunza kwenda bar na kiasi fulani cha pesa, kikiisha ni nduki home hata kama nina access ya kukopa labda kama kutakuwa na washkaji ambao watalendeleza libeneke.
 
Wewe ulikuwa mnywaji uchwara. Wanywaji uchwara wengi hujilaumu asubuhi baada ya pombe kuwapeleka puta jana yake. Yani wengi wanafanya mambo ya kitoto kitoto na hao ni bora wakae mbali na pombe. Wakinywa wanaweza hata kupumuliwa kisogoni au kutongoza mama mkwe!
Sema kila mnywaji anaonaga wenzake vichwa vya panzi.
 
Yaani nikope pesa kwa ajili ya pombe? Aisee mimi ni mlevi lakini siwezi kuingia madeni sababu niendelee kulewa, Nilijifunza kwenda bar na kiasi fulani cha pesa, kikiisha ni nduki home hata kama nina access ya kukopa labda kama kutakuwa na washkaji ambao watalendeleza libeneke.
Kwanza pombe inatakiwa ikupe starehe na kutuliza ubongo wako from stress na unaamka asubuhi vizuri unapata supu na kuendelea na maisha. Sasa ikiwa wewe unakunywa beyond limit mpaka kuingia kwenye madeni na kuitia familia kwenye shida huo ni upimbi wa hali ya juu.
 
Natamani kuacha kabisa ila huwa najikita nimepumzika tu
Kuna kipindi nilijifanyia tathimini nikagundua pombe ya wengi inatia hasara
Unajua kwa mfano umepata milioni moja from your mishemishe, cha kwanza ni kui deposit au kuacha home na mfukoni kubaki na at maximum elfu 50 kama kweli unataka kwenda Bar. Mimi nikiamua kwenda Bar nachukua pesa ya uwezo wangu wa kunywa say elfu 20 au 30 plus few extra basi. Kama najua leo nina pesa ya bia mbili tuu naenda kaunta sikai kwenye mambo ya kuzungusha...
 
Ukiifanya pombe kama starehe huku huna pesa lazimwa ubweke.

Pombe sio starehe ni kinywaji
Kwa ko uko sahihi lakini mimi naongelea aina hii ya walevi ambao ni wengi sana na hawako wazi kueleza shida zao, nimekuwa na rafiki zangu ambao wengi wana kipato lakini swala la ku overbudget na kuamka na mawazo ni kawaida sana kwao. Kujua siri hii inabidi awe mtu wako wa karibu sana ndio atafunguka
 
Back
Top Bottom