Ni Kweli, weng wanadhan hivi. Lakin sio Hivi.
Kufurahia maisha kila mtu na mtazamo wake, kila mtu na hobbies zake.
najua hata ww kuna kitu kinakupa furaha, bas hata wanaoenda Bar wanafanya hivyo ili waipate na sio Kwenda bar kila siku ndio kupatia maisha. (Hii dhana itoe).
Ila hapa ☝️☝️☝️ siko na ww.
vitu vingi vinaweza kusababisha hayo uliyosema juu, na sio pombe pekeyake.
Unaweza usinywe pombe na ukapoteza muda kwa vitu kadha wa kadha visivyo na msingi.
Unaweza usinywe pombe na ukaumwa figo, moyo Inni na Ukimwi.
Unaweza usinywe pombe na ukapoteza hela kwa wanawake na umalaya.
Unaweza usinywe pombe na bado ukawa hauna focus wala productivity.
kwahiyo vitu vyote ulivyotaja hapo juu Haviangalii unakunywa Pombe au haunywi.
Ingawa ukinywa pombe na ukawa Mvivu au huna uelewa basi inachangia zaidi kukupoteza.
But unaweza ukawa haunywi na bado ukapotea vile vile.
Maisha ni Jitihada/juhudi na kudra tuliojaliwa.