Pombe ni adui wa mafanikio! Ulevi unapoteza pesa, muda na Fursa

Pombe ni adui wa mafanikio! Ulevi unapoteza pesa, muda na Fursa

Mkuu sijui nikujibu, sijui niache....?

Kwa ufupi, nina historia mbaya na pombe, niliwahi kulala mahabusu miezi sita ijapo sikuhukumiwa kutokana na tukio nililolifanya...
Imepita miaka 28 sasa sijui kilevi kinaingia vp mdomoni
Ahsante kwa ushuhuda
 
Vijana wanapotea kwenye ramani kama utani,ni heri ambao wameajiriwa wanakunywa kwa nidhamu.

NB:Madogo wakikutwa wameukwaa wanatopea kwenye ulevi wa kupindukia,wanakuwa tegemezi na familia zinawashinda kuhudumia.
Mtu akiongea wanajibu " Usitufatilie"
 
Nilikunywa safari (ilikuwa ni miaka 2 tu tokea kuanza kutengenezwa) nikachanganya tusker pamoja na viroba vya no. 1, aisee nikarudi home, nilichokifanya kwa babangu mdogo, alikula kisu, utumbo huo njee, kakimbizwa ddh (hakufa)
Nakumbuka kauli ya mzee hadi leo "WE NGURUWE, MDOGO WANGU AKIFA NA WE UNAFIA JELA"
baada ya miez sita nilivyotoka habusu kwa kweli sitaki mazoea..ijapo nimetembea maeneo meng nje ya bongo, lakn nimekuwa nikijizuia.
Dah pole sana Mkuu, Je baba mdogo na Mzee Bado wapo hai Leo hii?
nimependa sana hapo Baba anapompigania uhai mdogo wake.ijapo wewe ni mwanae lakini hakutaka kuwa upande wako
 
Nikifikiria sana kwanini vijana wengi tumeingia kwenye mtego huu, huwa na hitimisha kwa kuamini shetani yupo kazini. Ulevi sio kuwa ni mtindo wa maisha tu, hapana! Ni mkakati wa kuzimu kufanikisha agenda yake ya kuwaongoza watu kwenda kwenye umasikini, magonjwa, zinaa na hatimaye jehanamu.(Ufunuo2:14)
Zinahitajika jitihada za makusudi za kiroho na kimwili kujinasua na kuwanasua wengine kutoka katika kifungo hiki cha giza.
Ulituomba mkopo wanywa pombe tutakunyima bwashee?
 
Sisi tunaopata michongo, connection na network Bar Tunaruhusiwa Kukupinga Kwa Fact?? sijui kwanini wasabato wanaichukia hivyo pombe.
 
Back
Top Bottom