Pombe sio chai. Nililala mwenyewe nimeamka na Mama mwenye nyumba, tunashangaana!

Mimi hapa Niko kupambana na hangover aisee niache pombe nasoma message nakuta nimetukanana na Mama Kijacho wangu mwe [emoji134] aisee niache pombe
Nipo napitia machapisho mbalimbali kuhusu mbinu za kuacha pombe.

Tukumbuke madhila ambayo tumepata yakisababishwa na pombe, tuichukie kwa kutupelekea kupata madhila hayo.

Tuweke nia thabiti ya kuachana nayo kabisa.

Tukubali kutenga baadhi ya marafiki, kampani ya pombe.

Tukatae katu katu kwenda mazingira yenye ushawishi wa pombe (Bar, clubs etc)

Tutafute cha kufanya kama mbadala wa pombe mathalani kukaa idle humpelekea mtu kuwaza kwenda tena bar kusogeza muda hivyo ni vyema ukajikita katika usomaji vitabu, watching movies nk.

Tukumbuke pia madhara ya pombe kiafya.


Mimi naanza na kuwakataa marafiki wa pombe, maana ndo kikwazo
 
Kukataa kampani ya wana walevi ili uache huo ni udhaifu..... Ushujaa ni kuacha pombe ukiwa na Hela na uko bar na rafiki zako wewe unakunywa mahi wao unawanunulia pombe ukifanikiwa kuwa n hiyo courage umetoboa....

Sasa mkuu umeacha pombe unarudi home saa Moja jioni kufanya Nini? Kaa sehemu na wahuni ndiko tunakopeana pia deals......unaweza kuacha mtungi usave pesa na deals pia zinapotea

Me mwenyewe nipo kwenye battle ya kuacha matukio ya kijinga ninayo mengi sana
 
Nafikiria mkuu sana hili sina cha kufanya kingine Mama yangu hii tabia inamsikitisha Sana Changamoto unajua ni nini Kaka sisi wanywaji tunaona pombe ndo kila kitu hivi week iliyopita nilitapika balaa nikaapa naacha Jana nimerudia na kutukana watu balaa nasikitika Sana hii hali.
Hapa kama ulivyosema ni kukataa kampani ya ulevi na kutafuta kitu kingine cha kufanya
 
Mgeunganisha mbona ni kudra za Mungu ndio zimewakutanisha
 
Nilishawahi kuacha kwa style hiyo mkuu, kibunda kipo, napitia ka pub flani hivi kadogo dogo nakaa na wana nawanunulia, mimi nakunywa redbull, nilidumu kwa wiki mbili tyu!



Ndo maana naona bora kuepuka tu
 
Nahisi mimi ni tofauti na walevi wengi. Nikiamua huwa naacha hadi miezi mitatu wakati huo bar naenda kama kawaida.
Jana yenyewe kuna mwana alinipigia simu alikuwa ameagiza kitimoto kilo akawa anauliza tuweke ndizi au ugali!

Nilivyoenda nikakuta meza imechafuka bea yupo yeye na mshikaji, but nikaishia kula nyama tu nikasema tu ukweli kuwa napumzika kunywa kwa mwezi ili kuweka mwili sawa.

Jamaa waligonga maji na mimi pepsi 2, nikawaongezea round 3 wakawa washachoka wakaondoka na bia zilizobaki.
 
Pombe imeshusha sana heshima na hadhi ya wengi hatusemi tu. Pole mm yalinitokea makubwa zaidi ya hayo naogopa hata kukumbuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…