Pombe sio chai. Nililala mwenyewe nimeamka na Mama mwenye nyumba, tunashangaana!

Wa kwetu kila siku alikuwa anapotea nyumba wanamrudisha, pombe ikiisha akiulizwa Nini kilimpelekwa kwenye nyumba ile anajibu walimchukua kichawi wamemshindwa ndio wakamrudisha [emoji3][emoji3] tatizo sio nyumba moja karibu majirani zake wote wameshamrudisha nyumbani akilewa na ndio ulikuwa utetezi wake mkubwa. Ila mwenzio zimeshamtanguliza mbele ya haki

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Huyo kiboko, kumbe boko langu nililotoa jana ni dogo🤣🤣🤣🤣
 
Nilishawahi kuacha kwa style hiyo mkuu, kibunda kipo, napitia ka pub flani hivi kadogo dogo nakaa na wana nawanunulia, mimi nakunywa redbull, nilidumu kwa wiki mbili tyu!



Ndo maana naona bora kuepuka tu
Ila kiukweli mkuu Mungu atusaidie tu peke yetu hatuwezi..... Huu uraibu yataka moyo kuacha

Sent from my SH-01K using JamiiForums mobile app
 
Hongera umeshakua baba mwenye nyumba wa Lymo aisee kimzaha mzaha tu
 
Share experience mkuu ili tuongeze chuki dhidi ya pombe katika jitihada za kuelekea kuikataa kabisa
Kuna moja niling'ang'ania kulala kwenye chumba cha mpangaji wetu..... Hata sijui nilifikaje

Wana upande wao tunaupande wetu.... Maza hakuwepo.... Halafu huyo mpangaji mke wa mtu.... Na mumewe huwa hatuelewi anafanya kazi gani ila Dodoma

Walinichukua kunipeleka kwangu.... Naamka asubuh missed za mama Kama zote.... Najiuliza Kuna Nini? Nampigia ananiuliza Jana umefanya Nini? Ndiyo kumbukumbu zikanijia.. nikaenda kuomba radhi kwa aibu... Maana nilikuwa likizo ilibidi kuondoka kabla ya muda niliokuwa nimejipangia....

Sent from my SH-01K using JamiiForums mobile app
 
Hiki kisa chako kinafanana na cha kwangu kasoro mazingira flan flan tu.

Kisa hicho ndiyo kilichosababisha nikaacha pombe kabisa zaidi ya miaka 30 sasa!

Na humu jamvini nilishakisimulia hicho kisa.

Labda kama hukupitia huo uzi, nieleze tu kwa kifupi.

Nilikuwa na mtindo wa kuchanganya pombe kali na bia nikiwa na maana ya kubana matumizi.

Enzi nakaa "kota" kuna siku niliutwika kwa kuchanganya bia na "power", vikanifyatua akili nisiweze kukumbuka hata namna nilivyorudi.

Kufika nyumbani, nilikosea nikaingia nyumba ya jirani nadhani kwa ufanano wa majengo na apartment, nikaingia na kulala fofofo huku "nikiharibu" kitandani.

Baada ya tukio hilo kunibebesha aibu, pamoja na hatua zilizochukuliwa, nikaapa kutorudia starehe ya kunywa pombe na ndiyo ukawa mwisho wangu wa maisha ya ulevi.
 
Pole sana mkuu na hongera kwa kufanikiwa kuacha mululu.

Nimeianza safari rasmi hivi sasa, safari ya kukataa gambe, naamini kwa jina La Yesu nitatoboa!

Nimeshafanya vituko vingi sana ila hiki cha jana babkubwa.

1. Nilishawahi kutapika sana kitandani, wife akatoa shuka linanuka matapishi.
2. Nilishawahi kuamka usiku nikazunguka nyuma ya dressing table la wife nikijua ni chooni nikamwaga mkojo.
3. Nimeshawahi kuamka usiku badala ya kuzama toilet nikaenda kukojoa kwenye kochi sebuleni kisha nikarudi chumbani kulala.
4. Kuna kipindi wife kasafiri nilirudi home nipo ndwiii nikashindwa kuingiza gari getini nikalala hapo hapo kwenye gari mpaka alfajiri.
5. Gari nimeligongesha sana ukutani katika kupaki.
6. Nilishawahi kuchukuliwa hatua za kiutumishi za kinidhamu kazini baada ya kufika asubuhi nimelewa nikawaletea shida sana ofisini.
7. Nilishawahi kujihusisha na ugomvi Bar japo haukuwa wangu ni wa marafiki zangu nikauvaa.


Dah, Mwenyezi Mungu anijaalie tu katika safari hii ya kuacha pombe kipindi hiki nifanikiwe, maana kuna uwezekano huku ninapoelekea nikafanya tukio kubwa zaidi
 
Mkuu labda nikupe mbinu niyotumia kuacha:
Kwanza ni dhamira, pili ni kutafuta kazi za kufanya baada ya kazi zitakazokufanya muda wa ziada uwe bize.

Tatu ni kuzigeuza bar zote kuwa ni vituo vya polisi, usipite wala kusogelea.

Nne,itunze dhamira yako kama nadhiri usiivunje.

Ukiyazingatia yote hayo utafanikiwa.

Ila sasa ndoto za kuota umekunywa na kulewa zitakusumbua kwa muda mrefu sana kama ulikuwa umefikia hatua hiyo ya ulevi.
Na mwisho jihadhari kwenye masherehe, usije ukaonja hata kwa kuzugia, ulevi utarudi kwa kasi kama kansa.

Nikutakie heri na fanaka katika kutimiza dhamira yako hiyo.
 
Chai na mluzi ndio hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…