Pombe, Viduku, Milegezo Vimini Chanzo cha Wengi kushindwa Usaili Serikalini

3 Angels message

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2017
Posts
5,589
Reaction score
16,336
Habarini wakuu
Nimeona hii habari ikieleza sababu za wengi kushindwa Usaili wa ajira mbalimbali zinazotangazwa serikali

Sababu hizo zilizotajwa ni pombe, uvaaji usiofaa na mitindo ya nywele kwa wale wanaoitwa hasa kwa usaili wa mahojiano

Nukuu kutoka kwa Waziri Simbachawene "Mwalimu anakuja amevaa jeans imekatikatika humu eti anakuja kwenye Usaili wa ana kwa ana. Njoo kwenye usaili umepiga katai kako na kashati kako. Mbona siku hizi kwenye masoko kuna hadi ka shati ka 1000 unamwona huyu ana haiba. Wengi wanashindwa kwa namna wanavyokuja"


Chanzo gazeti la Nipashe
 

Attachments

  • WhatsApp20Image202025-04-1720at2011.15.16.png
    280 KB · Views: 36
Sio sahihi Yani wote waliokosa ajira walikua kihuni hivyo?. Ni Bora kukaa kimya wala asidhihaki watu. Wasio na ajira ni wengi na serikali haitoweza kuajiri wote hivyo aache visingizio
 
kuna dada aliomba nafasi ya Nursing kwenye Hospitali yetu kubwa na huku ana GPA 4.7 akakosa kwa sababu barua yake ya maombi haikuwa na picha ya passport, pamoja na kwamba vyeti vyake vilikuwa nayo..wakaishia kuchukua mtu wa GPA sijui ya 3.4 aliyeweka picha ya passport kwenye barua ya maombi. Ukweli niliogopa sana...
Huko Serikalini wapo serious sana....japo niona viashiria vya kuwapa jukumu watu wasio makini
 
Hizo picha za hayo mavazi ziko wapi?, Wewe mleta mada umeyaona wapi mavazi hayo? Acha kuleta nada za kipumbavu na wapumbavu wako wa ccm.
Ha ha mkuu mbona una jazba hivyo ukitaka kuyaona kajipatie nakala yako ya gazeti la Nipashe
 
Kuna taaluma binafsi nikimuona mtu kaja na jeans na t-shirt na chini raba tu yakawaida kifupi yuko simple, na nywele amenyoa Tu kawaida yaani nywele fupi NAMPA KAZI HARAKA SANA, Kwa uzeofu wangu hawa huwa niwapiga kazi sana na wako real.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ha ha mkuu mbona una jazba hivyo ukitaka kuyaona kajipatie nakala yako ya gazeti la Nipashe
Nashanga unacheka hata pasipochekesha!!, Unakuja na hoja dhaifu dhidi ya mifumo iliyofeli kutengeneza ajira kwa vijana!!. Matahalani walioomba ajira za ualim walikuwa 200,000 waliokuwa wanahitajika ni 15,000!! Anamaanisha hawa WOTE waliokosa ajira walikuwa walevi na wavaa milegezo?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…