Habarini wakuu
Nimeona hii habari ikieleza sababu za wengi kushindwa Usaili wa ajira mbalimbali zinazotangazwa serikali
Sababu hizo zilizotajwa ni pombe, uvaaji usiofaa na mitindo ya nywele kwa wale wanaoitwa hasa kwa usaili wa mahojiano
Nukuu kutoka kwa Waziri Simbachawene "Mwalimu anakuja amevaa jeans imekatikatika humu eti anakuja kwenye Usaili wa ana kwa ana. Njoo kwenye usaili umepiga katai kako na kashati kako. Mbona siku hizi kwenye masoko kuna hadi ka shati ka 1000 unamwona huyu ana haiba. Wengi wanashindwa kwa namna wanavyokuja"
Chanzo gazeti la Nipashe