Pongezi kwa Raia Mwema (Mtoa Taarifa) na Mkuu wa Mkoa wa Tabora

Dkt.gwajima Asante kwa ufafanuzi wako. Umefanya kazi nzurii unastahili pongezi kwa kweli.

Hongeraaaa sanaa kwa kuwepo humu jukwaani bila kificho na umekua msaada kwa wengi 🇹🇿
 
Nimeguswa na utendaji wako Shem Mhe. Dr. Doro. Hongera sana kwa jinsi unavyojitoa kuwahudumia Watanzania. Ni Mungu tuu atakulipia. Ubarikiwe sana. Salaam kwa Kaka.
P
Salaam kiongozi. Ahsante Sana. Ubarikiwe, salaam zimefika, mume wangu naye Adv. Gwajima anakusalimia🙏🏽
 
Pongezi pia zirudi kwako Mh Dkt. Gwajima D kwa kuchukua hatua za haraka na kwa jinsi ambavyo umekuwa ukitetea haki za wanyonge katika nchi hii.

Naomba kama hautajali nipate namba yako ili nikipata tukio lisiloeleweka nikuletee ujumbe. Ni viongozi wachache sana wenye moyo kama wako na walio tayari kutetea maslahi ya wanyonge. Mungu akubariki sana.
 
Tulikutumia ukapiga kimya, umeibukia Nzega😭
Ndiyo maana kuna mbadala pale ninapokuwa sijawahi kujibu. Tumetengeneza kabisa na simu 5 za kituo cha wizara na tumetangaza. Na pia kumbuka, wizara zote Zina mawasilino yao moja kwa moja. Na Mimi sijaja na namba zangu kutengua utaratibu rasmi bali kuongezea tu nguvu. Pai ukumbuke, admin wa simu zangu ni Mimi mwenyewe nami ni binadamu nina dharura zangu za kibinadamu kama wengine..

Hivyo, kabla ya kulaumu nikuulize, je ulichukua hatua zipi baada ya kuona kwangu kimya? Shukrani
 
Pongezi zaidi zikufikie wewe kwa kukubali kuwa karibu na jamii. Mwanzo nilikuwa sikuelewi lakini hv sasa kwenye list ya mawaziri 10 wanaofanya kazi zao bila makelele ya media, wewe ni wa kwanza hadi watano. Anayekufuatia yuko namba 6
 
Shukrani kwa ushirikiano wako. Namba zangu ziko wazi kwa kupokea ujumbe wa kuandika tu kama kupiga napiga mwenyewe. Nazo ni 0765345777 na copy 0734124191. Namshukuru Mungu huduma hii ninayo tangu mwaka 2003 bahati mbaya sikuwa na Majukwaa ya online. Nakushukuru kwa ushirikiano wako 🙏🏽 wape na wengine ila waambie waandike ujumbe pia watumie mifumo rasmi maana huwa napenda kwangu iwe rufaa Ili nijue pia nani hatimizi wajibu wake vema chini yangu au anatimiza vema🙏🏽

EDIT NAMBA hapo revised kulikuwa na error tpaul
 
Pongezi zaidi zikufikie wewe kwa kukubali kuwa karibu na jamii. Mwanzo nilikuwa sikuelewi lakini hv sasa kwenye list ya mawaziri 10 wanaofanya kazi zao bila makelele ya media, wewe ni wa kwanza hadi watano. Anayekufuatia yuko namba 6
Ubarikiwe tuendelee kushirikiana. Mambo Duniani humu ni mengi na mengi huwa hayaeleweki hadi wakati ufanye kazi yake. Tuendelee kushirikiana. Shukrani
 
Kwenye utekaji wa watoto wizara inajitahidi!
Watu wazima wakitekwa, ni wizara ipi tuwajulishe!
 
Da Dorice, ya the best
 
Hili nalo ulipiga kimya! Kisa huyu ni CDM!
Siyo kweli. Jiunge x uwe unafuatilia Dunia pande zote. Mbona nilichati na watu kibao kuhusu hili jambo Hadi wakani quote wengine tofauti na nilichomaanisha nikaanza tena kuelimisha siku nzima.

Ulimwengu wa kidigitali ni mpana Sana, unayedhani hayuko huku anaweza kuwa kule ambako na wewe haupo pia.
 
Nimelizambaza Jf, na hata Saa100 amepiga kimya kama mama na mlezi
Siyo Kila taarifa nitaiona, hakuna binadamu anafanya kwa efficiency ya asilimia mia moja ndugu zangu. Na ndiyo maana kuna mifumo rasmi na kuna additional. Labda tuanzie tu ulipoishia tuone tunaendaje. Aidha, poleni sana kwa tukio hilo ambalo sikuliona bahati mbaya . Shukrani
 

Kwa mara nyingine nikushukuru tena na zaidi sana kwa kutambua yote haya ni kwa nia njema.

Hata hivyo nikuombe kuzitambua pia frustrations zetu tunapowaona kwenye endorsements ambazo bila shaka nanyi zinawakwaza.

Nitambue kuwa wewe nyungu haikuwa yako, hukuwa msemaji wake na wala hukuwa na mamlaka juu yake.

Kuwahusu matapeli wa tiba na wenzao, natambua Roma haikujengwa siku moja. Kwa hili nikupongeze sana na mapambano yaendelee. Ni matumaini yetu siku moja wote wa aina yao hawatakuwapo mahali popote nchini kuwapotosha wengine kuhusu tiba.

Kufikia hapa lawama zangu na nyungu na wa namna hiyo si kwako tena, ila wahusika wake.

Ninaondoa hofu niliyokuwa nayo nawe, huko afya. Labda Kumbe inaweza kuwa nafasi nyingine kuturekebishia mengine kama haya huko au hata kumfikishia waziri Mhagama:

1. Gharama kubwa za matibabu hospitali. Uzi huu unahusika:

Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

2. Sokomoko la wahudumu mahospitalini kupigania maslahi yao binafsi ambapo:

a) Wenye nazo hugombewa (kama na wapiga debe stendi) kwa sababu hutegemea malipo kama % ya malipo ya mgonjwa mmoja mmoja. Kwenye hili wagonjwa ni wahanga zaidi ..

b) upendeleo kwenye upangiwaji majukumu kiutendaji ambapo wasiopangiwa kwenye wagonjwa wa pesa hulia njaa daima ..

c) Hospitali za umma kutumika kutibu wagonjwa kinyemela kama hospitali binafsi ..

Yapo mengi ila kwa hakika kwenye afya na kote kwenye haki, ikimpendeza mkuu wa nchi, mbona asingejilaumu?

Pongezi kwako mheshimiwa!
 
Biashara ya utumwa ipo Tanzania, tena imeshamiri sana.
 
Ubarikiwe, ahsante kwa mjadala mwema chanya na ushirikiano, nimepokea maoni yako, nitayafikisha. Shukrani
 
Mwaka 2025 mola akipenda tutafanya uchaguzi Mkuu, Mimi ninakuomba nikuchukulie fomu ya kugombea, kama itakupendeza.

Umekuwa ukifuatilia,kusikiliza kero za watanganyika bila kuchagua dini,kabila Wala umri.

Ninaomba ukubali ombi langu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…