Pongezi kwa Rais Magufuli kusitisha Bomoa Bomoa kwa kuongeza kigezo cha "Human Face". He's so Human!

Pascal kinachosababisha rais aonekane ni mbaguzi ni matamshi yake. Anasema nabukuu kuwa msiwabomolee hawa kwani ndio walionichagua kuwa rais. Kuna walioumia kutoka mikoa mbali mbali hasa Dar na rais hakutoa hata tamko aliwaacha wakalia wakalala nje na familia zao. Na hata mahakama ilipotoa amri ya kusitisha rais alikuwa kimya. Ni sawa na alivyofanya kipindi cha wamachinga aliachia wamachinga kibao kubomolewa vibanda vyao na kunyanganywa vitu vyao. Baadae ndio akaenda mwanza na kusitisha. Kwa kweli rais wetu ni mbaguzi yote haya yanaonekana na kusikika kwa kauli zake. Hapendi demokrasia anataka Tanzania iwe na chama kimoja tu yaani ccm. Ila anajijengea mazingira magumu sana hapo atakapomaliza kipindi chake. Mambo ubadilika. Jiulize mbona waliobomolewa Dar ni upande wa Kimara eneo ambalo walichagua opposition. Walipotaka kubomoa maeneo mengine dar mkuu wa mkoa akahitokeza na kuzuia kwasababu malengo yao ya kuwakomoa waliyowapigia opposition ilitimia. Rais hatakiwi awe mbaguzi ni hatari sana yaani anatujengea taifa mbaya
 
Mmmh Paskali hii kali lakini ngoja nami niwe mtizamo kama wako.Nisiliangalie andiko lako literaly but the motive behind it.
Paskali,umetukanwa ukaenda kushtaki lakini kila anayekuja kukuhoji anakuuliza "alikutukana vipi" nawe unalirudia tena lile tusi.
Haya,vipi kuhusu hili la kumtoa mbunge wa Tunduru kumpeleka Mwanza nayo imekaaje?Si angeambatana na Lipumba tu mambo yaishe!!!
Hapa ndio kwetu ndugu yangu na JPM ndiye Raisi wetu!!!
 

Hapa tupongeze the human face au tupongeze open, daylight ubaguzi wa watu wako?

halafu wewe paschal of all people unasema kinafanywa kwa good faith. hebu inama chini peke yako halafu jiambie kuwa kuna good faith. fanya hivi ukiwa peke yako. au sijui kama utaweza maana you are too superstitious to do that.

Hebu jitahidi kumconvince zaidi kuwa kubomoa nyumba za kundi moja is perfectly legal and justifiable and kundi lingine you need to apply the human face.

you don't have to write anything that will taint your soul, if you have a soul.

just don't
 
Hahaha haya Mayalla
Umeniacha Hoi hapa ila nimekuelewa sana

"kupongeza kauli ya rais Magufuli kusimamisha bomoa bomoa ya nchi mzima, kabla bomoa bomoa yoyote haijatekelezwa, upembuzi yakinifu kwa kutumia kigezo kipya kiitwacho a human face, lazima kitumike kwanza"
 
Naww pia utakuwa ni msukuma
 
Kwani Rais alishindwa kusema nasitisha bomoabomoa nchi nzima, kama kweli alimaanisha hivyo? Ni mbinafsi, mbaguzi, mkabila na mtu wa visasi. Amedhihirisha kuwa yeye ni anaendesha nchi kwa misingi ya ubaguzi wa kivyama, kikabila na kikanda full stop.

Mkuu Pascal kamwelewa vizuri sana, na akaona kauli ya mh. ilikuwa na walakini kidogo, ndio maana ameamua kuongezea hayo maneno mengine kama kumshauri Rais indirectly.
Lengo likiwa moja tu, Rais asitafsiriwe vibaya kuwa ni mbaguzi kiaina. Hakuishia hapo kaamua kuwashtua wasaidizi wake wapaze sauti kuliweka hili jambo ktk mstari unaokubalika.
 
dah JF siku hizi imevamiwa, yan mtu anavuliwa nguo hapa afu nyie mnamlaumu paskali[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ........

huu uzi wa paskali umejaa kejeli kwa mkulu, na dhihaka lkn watu hawaelewi
 
mayala usijilazimishe kuwa MPUMBAVU. tumemsikia na tumemuelewa hatuitaji tafasiri maana akuongea lugha iliyohitaji tafasiri
 
Nauliza tu, kwani Pascal na Jerry Muro ni ndugu?
So na aliposema kwa Bashite kukamata madawa kwake ni cheti tosha, so napo ulimi uliteleza au? Kuweni makini jamani nchi inakoelekea si kwema. Tuache ushabiki ndizi na tutumie akili zetu kwa manufaa yetu na si kujipendekeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…