USIOE SINGLE MOTHER
Anaandika, Robert Heriel
Baba
Onyo; andiko hili linaweza kuwa na Lugha Kali. Hivyo halitafaa kusomwa na watu wenye mioyo dhaifu, laini na wenye mihemko ya juu. Hivyo Kama upo hivyo ninakushauri uachie kusoma hapahapa. Kukaidi agizo hili ni kuonyesha upo tayari Kwa matokeo, na sitohesabika kuwa sehemu ya matokeo mabaya utakayoyapata. Bali ukaidi wako ndio utakuwa chanzo cha hayo madhara.
Usiwe limwanaume lijinga. Mimi Baba yako siku zote nimekufundisha kuwa hodari na roho ya ujasiri. Na hauwezi kuwa shujaa na jasiri kama utaendekeza ujingaujinga. Kuendeshwa na Hisia kuliko Akili ni moja ya ujinga.
Ikiwa utataka kuwa mtakatifu na Kuhani utaoa mwanamke mwenye sifa hizi;
i. mwanamke Bikra/msafi
ii. Mke mmoja
iii. Asiye mlevi,
iv. Asiye mjane au aliyeachwa Kwa talaka.
V. Asiye mshirikina na mchawi
Ikiwa hautataka kuwa mtakatifu Sana au Kuhani Ila unataka kuwa na familia yenye furaha na Amani, basi Oa mke mwenye sifa hizi;
i. Asiye na mtoto/asiye single mother
ii. Asiye limbukeni/ mwenye tamaa.
Asiyeendeshwa na mambo ya fasheni, mitindo ya kidunia
iii. Asiyependa vitu vya burebure.
Mwanamke anayependa vitu vya burebure lazima awe Malaya na lazima akuzalie vitoto vimalaya Malaya
iv. Mchapakazi.
Mwanamke Mchapakazi lazima awe na Akili sio limwanamke kama mdoli. Huyo hafai kuwa Mkeo. Huyo atafaa Kwa matumizi ya rejareja(STAREHE ya kununuliwa)
Ukioa mwanamke mvivu asiye Mchapakazi ninakuhakikishia utakufa kabla ya muda wako kwani atakuua Kwa namna mbili;
a) Atakuua Kwa Stresss na upumbavu wake.
b) Atakuua Kwa mikono yake au kukuombea Dua ufe baada ya ninyi kupata Mali.
Ninauhakika na nikisemacho.
Mwanamke mvivu anataka uendelee kuishi ili akunyonye na umsaidie kumlea yeye na watoto wake. Lakini mwanamke Mchapakazi anataka uendelee kuishi ili mipango mliyojiwekea akusaidie kuitimiza.
USIOE SINGLE MOTHER.
i. Elewa kuwa single mother ni mke WA mtu. Kuoa single mother ni kubet maisha yako na future ya kizazi chako.
Single mother atakuwa na misimamo endapo Mzazi mwenza hatakuwa na kipato cha uhakika. Lakini kama anakipato cha uhakika kukuzidi basi umekwisha.
ii. Elewa kuwa Mwanaume aliyemzalisha Mkeo anahaki Sawasawa na wewe.
Anayohaki ya kuwasiliana naye vyovyote atakavyo kujua Hali ya mtoto.
Zingatia; mwanamke hawezi kumzalia mtu asiyempenda, weka akilini hiyo.
Nadra Sana mwanamke aliyekamilika kubeba mimba ya mtu asiyempenda.
iii. Elewa kuwa Mkeo hawezi kukupenda zaidi ya anavyopenda m/watoto wake.
Hivyo huyo mtoto wa mwanaume mwenzako Mkeo anampenda mara elfu kuliko anavyokupenda wewe.
Hivyo wanawake wengi wapo tayari kuhatarisha hata ndoa zao Kwa sababu ya watoto wao.
iv. Elewa kuwa wewe ulitokea kama Ajali tuu katika maisha yake. Kama sio kugombana na Huyo aliyemzalisha basi wewe usinge-exist katika maisha yake.
Hivyo wewe ni Dependent variable wakati mzazi mwenzake ni independent Variable.
Hii itakuathiri Kwa namna hii, wewe ndiye utakuwa na hofu kuwa asije akawa bado anawasiliana na Mzazi mwenza ilhali Huyo Mzazi mwenzio Hana hofu na wewe. Sijui Kama unaelewa.
V. Elewa kuwa Single mother ni Binadamu tena mwanamke ambaye kiasili mwanamke ni mtu wa kulinganisha, reference. Kila kitu atakuwa anakulinganisha na Mzazi mwenzake aliyemzalisha.
Elewa kuwa huwezi kumshinda mzazi mwenzake Kwa kila kitu.
Na elewa kuwa yapo mazuri mengi ambayo Mkeo atakuwa anayakumbuka kutoka Kwa mzazi mwenza.
Ikiwa Waisrael walikumbuka matikiti na matango ya Misri wakiwa wanaenda Canaan sembuse Hawa Dada zetu.
Hatuwezi kuwalaumu ndio nature ilivyo.
vi. Elewa kuwa unapooa single mother, sio wewe pekee unayemfanyia maamuzi Mkeo. Hata huyo Mzazi mwenza anamfanyia maamuzi indirect way. Ingawaje atakuwa anawasiliana naye Kwa Siri kubwa kama atakuwa anakuheshimu.
Elewa kuwa uliyemuoa ni alikuwa mke WA Mtu tena mwenye mtoto, hata ufanyeje huwezi futa hilo dunia hata igeuke.
Vii. Elewa kuwa single mother lazima awasiliane na Mzazi mwenza. Hata umpige labda umuue.
Asije akakudanganya kuwa hawasiliani na Baba watoto wake. Huo ni uongo wa mchana.
Wanaweza wasiwasiliane Kwa miezi au miaka miwili lakini elewa kuwa IPO siku isiyo na jina mahusiano Yao yatarejea upya hasa ujana unapoisha.
Hivyo sio ajabu wakakaa miaka mpaka 10 au 20 bila mawasiliano lakini utashangaa mara paaap! Hao.
Na hii ni pale huyo mtoto atakapofanikiwa na kuwa mtu Fulani,
Mbaya zaidi watoto wako wakiwa hawajafanikiwa[emoji23][emoji23].
Hii itamaanisha Mchanganyiko wa mbegu za wawili hao ulikuwa Bora na wenye Nyota Kali kuliko mchanganyiko wenu.
VIII. Elewa kuwa Mtoto wa single mother sio wako hata ungemfanyia nini kwenye Maisha yake. Hata ungemnunulia ticket ya Peponi bado hatakuwa wako.
Na Mkeo IPO siku atakuambia Kwa mdomo wake kabisa kuwa huyo mtoto sio wako akikuona umekuwa na mambo ya kibwege Bwege kung'ang'ania mbegu isiyo yako.
Ninachowapendea wanawake ni Akili zao za mahesabu, ukiona anakunyenyekea hata Kwa mambo yasiyo ya kweli jua kuna faida anapata. Akiona muda wako umeisha na umeshazeeka hawasiti kukuonyeshea rangi zao halisi.
Elewa kuwa mwanamke Hana huruma, isipokuwa huruma Kwa watoto wake wa kuwazaa na Kwa mbali kidogo Kwa mwanaume aliyempenda Sana.
Zingatia kuwa Upendo WA kweli WA mwanamke au mwanaume ni ule upendo WA awali(First love).
Sasa wewe ni Mpenzi upo table ya Tisa huko Nani akupende Kwa dhati.
Ogopa kupendwa Kwa sababu umemsaidia mtu au kumtendea wema. Huo sio Upendo.
Upendo WA kweli ni ule wa awali ambao mtu anakupenda pasipo sababu ya maana.
ix. Elewa kuwa ukioa single mother alafu ukaona mambo yapo shwari jua huyo Mwanaume aliyemzalisha Mkeo jua Hana time na Mkeo au busara na hekima zake ndio zinalinda ndoa yenu. Hasahasa huyo mwanaume akiwa amekuzidi kipato na hadhi.
X. Elewa kuwa single mother hawezi kukuheshimu Kama ambavyo alikuwa anamheshimu mwanaume aliyemzalisha. Ingawaje atakuwa labda anamchukia lakini kamwe hatokubali akusikie ukimuongelea vibaya Mwanaume aliyemzalisha hasa akiwa wakipato cha chini nawe ukiwa kipato cha juu.
Atajikuta anamuonea huruma.
xi. Elewa kuwa single mother hujivunia wakiona mafanikio ya wanaume waliowazalisha. Sio ajabu akiwa na rafiki zake akikuponda wewe uliyemuoa na kumsifu huyo aliyemzalisha na kumtelekeza.
XII. Elewa kuwa single mother Kama ndiye alikuwa chanzo cha mwanaume aliyemzalisha kumuacha. Sio ajabu akawa anamtafuta Kwa Siri kujaribu kumuomba Msamaha kuwa hata kama hawatarudiana lakini wawe marafiki na waendeleze mahusiano Kwa Siri.
xiii. Elewa kuwa ni rahisi single mother uliyemuoa kuzaa tena na Mwanaume aliyemzalisha.
Elewa kuwa wanawake wengi walioolewa ni rahisi kuchepuka na Ma-ex wao kuliko kuanzisha mahusiano mapya. Wakati Kwa upande wa Sisi wanaume tukioa ni rahisi kuanzia mahusiano mapya.
Zingatia, wanaume tunapenda Wanawake wapya wakati wanawake wanapenda vitu vipya.
xiv. Elewa kuwa kadiri unavyomkataza Mkeo asiwasiliane na Mzazi mwenza ndivyo unavyozidi kumkera na kumpa hamu ya kuzidi kumtafuta Kama sio kupata hisia Kali za Mapenzi juu ya huyo mwanaume aliyemzalisha.
Mwanamke akiona unamkataza kataza akili yake inakuona Kama hujiamini na anaanza kufikiri kuwa unamhofia huyo mwanaume mwingine hivyo ataanza kuangalia Kwa jicho la wewe kuzidiwa. Na hatokosa mambo uliyozidiwa.
xv. Elewa kuwa kumpenda mtoto wa single mother sio Option Bali ni lazima ufanye hivyo.
Elewa pia hata umpende vipi huyo mtoto wa single mother bado hatakuwa wako. Elewa zaidi kuwa, Mkeo kwenye Akili yake hatofikiri unamfanyia hisani, Bali ataona amekukamata na yeye ni mzuri kama Malaika ndio maana umedata na anayohaki ya hayo unayoyafanya.
Jua kuwa Saikolojia ya mwanamke haipo mbali na saikolojia ya Paka.
Kumhudumia single mother na mtoto wake, yeye kwake haoni ni hisani Bali anaona uzuri wake na mambo anayokufanyia kitandani na vyakula anavyokupa ndio kiini cha wewe kumfanyia yote hayo. Kumbe wewe ni roho tuu ya kibinadamu umeamua kumsaidia yeye na wanawe lakini wao hawataliona Hilo.
Ndio maana niliandika usi usemao; usimuonee mwanamke huruma soma hapa[emoji117][emoji117]
Usimuonee huruma Mwanamke
Kumbe kimsingi hakuna utamu wowote wa maana isipokuwa ni tamaa zetu wanaume ambazo Mungu alituwekea.
Zingatia; Sio single mother wote wenye tabia mbaya Kwa maana wapo ambao walirubuniwa na kuchezewa hisia zao na wanaume washenzi, lakini pia wapo single mother waliopata watoto wangali wakiwa watoto wakiwa hawajitambui ingawaje nao siwezi watetea Sana kwani waliamua kukaidi na kutotii wazazi wao wakakimbilia mambo makubwa.
Nashauri,
i. usioe single mother Kama ndio ndoa yako ya Kwanza.
ii. Usioe single mother Kama upo below 40 yrs
iii. Usioe single mother ikiwa mwanaume aliyemzalisha bado ana-exist/anaishi.
iv. Kama utaoa single mother, mtoto apelekwe Kwa Baba wa mtoto.
Kwa upande wa wanawake;
i. Usikubali kuzaa na Mume WA Mtu.
Usisingizie alikudanganya kuwa Hana mke. Usimpe papuchi mpaka akakutolea barua ya Uchumba au Ndoa Kabisa.
No excuse katika hili.
ii. Usikubali ku-date na Mwanaume ambaye hatakuoa, ambaye hawezi kuwa Baba yako au Baba WA watoto wako.
Sio unatafuta masharobaro Kama kina Taikon, Sisi tunakujaza alafu utajua utaenda kumzalia wapi.
iii. Mambo ya ukipenda ua penda na Ua lake hiyo Kauli itumieni Kwa wanaume washamba. Mwanaume kamili hawezi lea mbegu ya mwanaume mwingine aliyemzalisha Mkewe. Hiyo kiroho haipo hata Kwa wanyama haipo. Labda katika Ulozi na misukule hiyo kanuni inaweza kutumika.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam